Saturday, June 23, 2012

KWA NINI KUNAMAHANGAIKO DUNIANI?


Sehemu ya mwisho.


Wewe nami tumekutwa katikati ya pambano linalochanganya la ulimwengu, ugomvi kati ya mamlaka na uasi, kati ya Muumbaji na Shetani, muasi wa kwanza.! Sisi si watazamaji. Tunahusika, tupende tusipende.
Dhana kwamba Shetani ni hadithi tu ama mvuto fulani tu, hutuacha tukiwa hatukujiandaa kabisa kukabiliana na kiumbe mwenye akili kama alivyo.
Kitabu cha Ufunuo kinasema: Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.! Ufunuo 12:12.
Kwa sababu hiyo, furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba siku zake zilizobakia ni chache.
Petro aliandika onyo hili: Muwe na kiasi na kukesha kwa adui, Ibilisi,  mshitaki wenu kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ammeze. akitafuta mtu ammeze. 1 Petro 5:8.
Lakini hata ingawa Shetani hutenda ubaya zaidi, Mungu wa uumbaji anao mpango wa kuumba upya ambao umjumuisha Mwana wake Yesu- Mwana wake wa thamani aliyekuwa hiari kufa ili kulipa deni letu ili tuwe na uzima wa milele.
Shetani alitenda kazi kupitia kwa Mfalme Herode ili kumuangamiza mtoto Kristo (Akashindwa).
Shetani alikuja kwa Yesu jangwani, akijifanya kuwa malaika kutoka mbinguni akiwa na majaribu makuu matatu (Akashindwa).
Shetani alichochea halaiki ya watu ili wamwangamize Yesu pale Kalvari (Alikuwa adui aliyeshindwa milele).


Ingawa kulikuwa na Kalvari, kulikuwa pia na ufufuo! Mungu Asifiwe!!
Hivyo ndivyo ilivyokuwa ya kwamba Mungu alimtoa Mwanae; na Mwana akajitoa mwenyewe, ili kubatilisha hatima yako na yangu.! Ilikuwa ni saa ya ushindi, siku ya kutamka uhuru kwa ajili ya wafungwa wote wa mwovu katika Sayari Dunia.
Siku hiyo Shetani akawa adui aliyeshindwa! Kristo kwa mauti yake akapata haki ya kuangamiza uovu wote na mateso.! Paulo aliandika katika Waebrania 2:14: Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi.
Shetani alidhihihirisha mbele ya wenye ufahamu wote wa ulimwengu kuwa yeye ni kiumbe wa jinsi gani. Na bado anaendelea kudhihirisha jinsi ambavyo angeuendesha ulimwengu.! Vimbunga, matetemeko, mafuriko, uhalifu, maradhi, huzuni, na maumivu!! Haya tunayaona Lakini nguvu isimamayo nyuma ya yote haya bila kuonekana kwa macho ni ile kazi ya Shetani ipitayo akili ya mwanadamu.
Haya maafa siyo matendo ya Mungu- haya ni matendo ya mwovu.
Waweza kuwa unashangaa juu ya masikitiko, huzuni, na matatizo katika maisha yako binafsi. Waweza kuwa unashangaa juu ya kifo cha mtoto ama mpendwa na kuuliza Yu wapi Mungu?
Biblia inafundisha ya kuwa Mungu yupo. Yupo katikati ya huzuni zako masikitiko, na matatizo.! Na atakuja muda si kitambo kushughulikia tatizo la dhambi na mateso.
Habari njema ni kwamba sayari hii nzuri, iliyotekwa na Shetani, i karibu kuokolewa.! Ufahamu huu wapaswa kunyamazisha hofu za abiria wenye shauku, juu ya sayari inayokwenda kombo!! Mungu anao mpango wa kumwangamiza Shetani-- mwovu mdanganyifu.
Hebu tuone kile ambacho Biblia inasema juu ya Shetani: .....Nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye....... Basi nimetokeza moto kutoka ndani yako; nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi... Ezekieli 28:16,18! Dhambi na taabu vitapotea milele.
Ndiyo, rafiki, Yesu anakuja upesi! Siyo kama mtu wa chini wa Galilaya, siyo kama aliyetukanwa, aliyetemewa mate, na aliyekataliwa. Siyo kama mtu anayening'inia msalabani, bali kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana akiwa na haki ya kutawala! Lazima tuwe tayari kukutana naye maana kama tukikosa hilo, tumekosa kila kitu
Utii wako uko wapi? Swala leo ni, Ni nani tutakayemwamini? Ni nani tutakayemfuata? Mungu mwenye upendo -au malaika aliyeanguka?
Mistari inachorwa;  Ulimwengu nzima unagawanywa katika sehemu
mbili. Wewe uko upande wa nani?
Kwa kila moyo usiotulia, moyo mpweke, kwa kila roho inayoumia, yenye hatia, kwa watoto wake wote katika sayari dunia iliyo katika uasi, Yesu anatoa mwaliko wa upendo:
Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Wote anipao Baba watakuja kwangu; ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe! Yohana 6:37 Je, hii si habari ya ajabu? Mathayo 11:28.
Katikati ya misiba ya maisha, simanzi, huzuni na kukata tamaa, Yesu yuko hapo.! Anaelewa simanzi uliyo nayo sasa hivi. Yesu anaelewa unachokipitia mwili wako unaporaruliwa na ugonjwa. Anajua maumivu. Aliyapitia wakati watu wakatili walipopigilia misumari yenye kukwaruza katika mikono Yake. Anajua upweke Aliupitia wakati aliponing'inia peke yake katika giza msalabani. Anajua umaskini.
Aliupitia alipotembea katika barabara zenye vumbi za Palestina akiwa na chakula kidogo tu huku akiwa hana mahali pa kupaita nyumbani.
Njoo kwake leo.
Atakupatia tumaini jipya na moyo mkuu. Hapa kuna habari nzuri kuliko zote. Siku moja hivi karibuni Yesu huyu atakuja tena na kukomesha taabu zote za maisha. Atakuja tena kuanzisha ulimwengu mpya.  Dhambi na wadhambi wataangamizwa. Hatimaye Shetani, atashindwa kwa ujumla kabisa. Yesu anatamani kukurejesha wewe kwa familia ya Mungu, kukupatia wewe uzima wa milele kwenye sayari iliyofanywa mpya.
Lakini uamuzi lazima ufanyike--Ni nani atakayekuwa Mkuu na Bwana wako ?
Rafiki, uamuzi huu ni swala la kufa na kupona Je, hutachagua sasa hivi kumruhusu Kristo awe Mfalme wako? Anasubiri. Mikono yake imefunguliwa wazi. Anasema, Njoo! Njoo! Njoo!!

Je, waweza kuinamisha kichwa chako tunaposali na kusema, Naam, Yesu, ninakuja.

AHSANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI KATIKA MFULULIZO WA MASOMO HAYA.
                    ***MWISHO***


Tuesday, June 19, 2012

KWANINI KUNAMAHANGAIKO DUNIANI?


Sehemu ya 3

Shetani ndiye aliyeleta taabu kwa sayari hii na ndiye ambaye amekuwa akisababisha dhambi na mateso tangu hapo. Yesu alimfichua mwovu na jinsi anvyotesa watu.
Siku zote yeye amekuwa akiwafunga watu kwa magonjwa ya ajabu na ajali vita majanga ya kila namna Shetani ndiye kiongozi.
Katika Biblia tunaona kisa cha mwanamke aliyefungwa na Shetani miaka 18, Yesu alibainisha kuwa amefungwa na shetani, yampasa kufunguliwa. Yesu akamponya yule mwanamke. Luka 13:16

Pengine hakuna mahali katika Biblia tuwezapo kuona mkakati wa Shetani kwa wazi zaidi kuliko ulivyo fichuliwa katika sura ya kwanza ya kitabu cha Ayubu, katika mazungumzo kati ya mwovu na Mungu.
Ilikuwa wakati fulani baada ya kuanguka kwa Shetani kwamba wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana. Shetani naye
akaenda kati yao.! Fikiria hili! Mkutano wa wana wa Mungu, na Shetani akaja bila kualikwa! (Fungu: Ayubu 1:7)

BWANA akamwuliza Shetani, 'Umetoka wapi wewe?' ! Ayubu 1:7
Kwa maneno mengine,ni nani aliyekualika? Una haki
gani ya kuwa hapa? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Ayubu 1:7 Shetani alidai miliki juu ya Sayari Dunia.

Alikuwaamenyakua nafasi ya Adamu! Adamu anaitwa mwana wa Mungu (Angalia Luka 3:38), kama tu wale wengine waliokuja siku ile kwa ajili ya mkutano na Mungu.
Je, yawezekana ya kwamba walikuwa ni viongozi wa dunia zingine, kama jinsi ambavyo Adamu alikuwa awali kiongozi wa ulimwengu wetu?! Kwa vyovyote vile, dai la Shetani la kuwakilisha Dunia halikupita bila kupingwa. Bwana akamwuliza Shetani; (Fungu: Ayubu 1:8,9,11) ..... 'Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu?

Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je, huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako'

Ni changamoto kubwa kiasi gani! Siku hiyo Shetani alidai ya kwamba sababu pekee ambayo kwayo Ayubu alimtii Mungu ilikuwa ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu alimtendea, na si kwa sababu alimpenda na kumtumaini Mungu. (Fungu: Ayubu 1:12)
BWANA akamwambia Shetani,' Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake mwenyewe.'Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA. Ayubu 1:12. Shetani aliondoka, akiwa na shauku ya kutia mikono yake katika mali ya Ayubu.

Mara mapigo yakaanza kuanguka: Kwanza: Waseba wakaiba ng'ombe wa Ayubu na kuwaua wafanyakazi wake.

Pili: Radi ikapiga, na kua kondoo wake na wachungaji wake.






Tatu: Wakaldayo walikuja na kuteka nyara ngamia wa Ayubu.







Nne (habari ya kuvunja moyo mno): kimbunga kiliipiga nyumba ya kijana mkubwa wa Ayubu. Karamu ilikuwa ikiendelea, na watoto wote kumi wa  Ayubu waliokuwemo wakauawa

Maskini Ayubu alidhani kwamba Bwana alikuwa amechukua mali yake na kusababisha msiba wote huo. Hakuelewa ya kwamba mwovu ndiye alikuwa ametenda hiyo Hata ingawa alizidiwa na huzuni, uaminifu wa Ayubu kwa Mungu haukubadilika.
Akasema, ....BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Ayubu 1:21
Ingawa hakuelewa misiba iliyoangamiza mali zake na watoto, Ayubu alidumu tu kutumaini wema wa Mungu. Lakini Shetani alikuwa hajamaliza. Akampa Mungu changamoto tena akisema, Ayubu 2:4-6
...Naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Ayubu 2:4-6.
Lakini sasa nyosha mkono wako,uuguse mfupa wake na nyama yake,naye atakufuru mbele za uso wako.
Jaribu lilikuwa tayari limeanza Je, Ayubu angesalia kuwa mwaminifu kwa Mungu wakati makali yatakapozidi kuwa makali, ama atamwacha Mungu?
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa. Ayubu 2:7.

Kama umewahi kupata na jipu, unajua jinsi ambavyo jipu moja tu linavyoweza kuuma.Fikiria sasa kitendo cha kufunikwa na majipu toka utosini hadi wayo wa mguuni.

Hata ingawaje Shetani alikuwa amempokonya Ayubu mali yake, watoto wake, na afya yake, Ayubu alisalia mwaminifu kwa Mungu. Mtu wa namna gani huyu! Biblia inasema, Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu. Ayubu 1:22.

Ni nani aliyemuumiza Ayubu? Ni nani aliyemletea mapigo Ayubu?
NI SHETANI.

Ni nani aliyeiba mifugo yake na kuua watumishi wake? Ni SHETANI!

Ni nani aliyeleta kimbunga kilichoteketeza wana na binti zake! Ni SHETANI.


Bwana anaweza kuruhusu matatizo yaje ili kujaribu utii na upendo wetu, bali SHETANI ndiye mwenye hatia kwa ajili ya uovu wote uliopo kwenye Sayari Dunia!

ITAENDELEA...

Saturday, June 16, 2012

KWA NINI KUNAMAHANGAIKO DUNIANI?


Sehemu ya 2.

Mungu anampa kila mtu uwezo wa kutii ama kutotii.! Kutokana na haki na upendo, Mungu amemruhusu Shetani kueleleza kwa ulimwengu jinsi ambavyo angeuongoza ulimwengu.! Hatuelewi jinsi yote haya yalivyotokea wakati Mungu alikuwa mwema na mwenye upendo kwa wote.

Pambano lililoanza mbinguni halijaisha, limebadilisha tu viwanja!!
Sasa Dunia ni eneo ambamo pambano kuu kati ya wema na uovu lingepiganwa, ambapo shetani angeeleleza aina yake ya serikali na jinsi ambavyo angeliiongoza dunia.

Lakini kwa nini Dunia? Kwa nini sayari yetu ikawa ....
(Fungu: 1 Wakorintho 4:9)! .... tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu. ! 1Wakorintho 4:9.

Dunia ilikuwa ndipo tu imetoka mikononi mwa Muumbaji, ikiwa inang'aa na ikiwa kamilifu, nzuri kuliko maelezo.! Ni wazi Shetani alifikiri vivyo pia, kwani aliiona dunia hii kama tunu ufaayo kuikamata.!
Angejaribu kuikamata sayari hii ikiwa katika uzuri uwezao kuvunjika - dunia ambayo ndipo imezaliwa.

Ingawa Adamu na Hawa, baba na mama wa wanadamu, waliumbwa wakamilifu, hawakufanywa wawe juu kuliko uwezekano wa kutenda makosa.
Walikuwa huru kuchagua kumpenda na kumfuata Mungu ama kutojali maelekezo Yake.! Lakini utii wao ulipaswa kujaribiwa, na jaribu hilo lingewekwa kwenye mti. Mungu alionya, (Fungu: Mwanzo 2:16,17)!
Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula; walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula
matunda ya mti huo utakufa hakika.! Mwanzo 2:16,17.!
Hilo laonekana kuwa lilikuwa ombi la busara. Lazima walijihisi salama kabisa. Lakini mtu yuko katika hatari kubwa akutwapo bila kujilinda kwa sababu hujihisi yu salama.

Hicho ndicho kilichotokea kwa Hawa.! Shetani alitumia uwezo wake upitao akili ya mwanadamu ili kumdanganya.! Shetani hutenda kazi hadharani kwa nadra. Yeye ni mdanganyifu sana.! Anatumia mifumo ya jamii, watu, au hata nyoka!

Kwa sababu hiyo Paulo anasema: (Fungu: Waefeso 6:11-12)!
Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Maana vita vyenu si kati ! yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.! Waefeso 6:11,12.

Hawa alidanganywa.! Hakudhani maneno yaliyotoka kwa nyoka yalitoka kwa Shetani.! Mwovu, akinena kupitia kwa joka, alimwambia,
(Fungu: Mwanzo 3:1)! ....Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?! Mwanzo 3:1. (Fungu: Mwanzo 3:2-4)!
Hawa akajibu, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini atunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, 'Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Nyoka akamwambia mwanamke, 'Hakika hamtakufa.' ! Mwanzo 3:2-4

Hawa alipokuwa akimsikiliza joka, lazima lilipita wazo ghafla kichwani kwamba alikuwa akinena tofauti na na jinsi Mungu alivyowaambia.! Pengine kwa kuhisi ya kwamba alionekana kuchanganyikiwa, joka kwa upesi aliongeza, (Fungu: Mwanzo 3:5)! Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema
na mabaya.! Mwanzo 3:5.

Mwovu alipendekeza ya kwamba Mungu hakufanya haki, kwamba alikuwa akizuia kitu fulani kizuri.! Kuwa kama Mungu ilikuwa tamaa kubwa iliyomla Shetani na kuwa chanzo cha maanguko yake. Sasa
Hawa pia aliliona kuwa wazo zuri pia; na kwa  haraka bila kufikiri, aliuzika. (Fungu: Mwanzo 3:6)!
Mwanamke alipoona kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala...! Mwanzo 3:6.

Akampa na mumewe, naye akala.
Adamu na Hawa wakashindwa jaribio la Mungu la upendo na utii, na haikuchukua muda mrefu kwa wao kugundua ya kwamba kuna jambo limeharibika.

Shetani alikuwa ameteka nyara dunia iliyozaliwa karibuni! Tangu wakati huo, akadai cheo cha , Mfalme wa Dunia hii.! Mtawala wa sayari iliyo katika uasi!! Adamu na Hawa walikuwa wameisikiliza sauti ya mwovu.

Kadiri siku hii ya msiba mkubwa ilipokuwa inafikia mwisho, Mungu akaja jioni wakati wa jua kupunga kama kawaida yake, akiwaita Adamu na Hawa.! Hadi sasa, huu ulizoeleka kuwa wakati wa furaha
mno wa siku - fursa ya kutembea na kuzungumza na Mungu moja kwa moja Yeye aliyewaumba. Lakini katika siku hii walikimbia na kujificha vichakani!
Hatimaye Adamu akachomoka pole pole kutoka nyuma ya vichaka katika bustani na kukiri kosa.

Muhtasari (Fungu: Mwanzo3:10)! ....Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi, nikajificha.! Mwanzo 3:10.

Muhtasari Adamu alikuwa hajapata kuogopa kabla ya hapo, lakini hicho ndicho dhambi inachofanya.! Inamfanya mtu amuogope hata Mungu. (Fungu: Mwanzo 3:11)! Mungu akajibu, ...Je! Umekula wewe matunda ya mti niliokuagiza usiyale?! Fungu 11.! Adamu akajibu: (Fungu: Mwanzo 3:12)! ...Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.! Mwanzo 3:12!
Saa chache kabla ya hapo, Adamu alikuwa tayari kufa pamoja na Hawa.! Sasa alimlaumu na pia akamlaumu Mungu kwa kumuumba. Jinsi gani dhambi inavyovunjavunja upendo uliomkamilifu!

Lakini Hawa naye hakushindwa kushitaki. Mungu alipomuuliza juu ya kile alichokuwa ametenda, alijibu, Muhtasari (Fungu: Mwanzo 3:13)!
....Nyoka alinidanganya, nikala.! Mwanzo 3:13.! Hawa alimshutumu Mungu pia! Kwa maneno mengine, alikuwa anasema, Ni nyoka uliyemuumba  ndiye aliyeniingiza taabuni.

Siku ile ile Adamu na Hawa wakawa chini ya kifo! Ili kuwazuia Adamu na Hawa wasile matunda ya mti wa uzima, Mungu akawaondoa kutoka kwenye nyumba yao ya bustani. ! Mwovu alisema ya kwamba wasingekufa, bali Biblia yasema, Muhtasari (Fungu: Mwanzo 5:5)!
Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. Mwanzo 5:5! Wakiwa wamechelewa kabisa waligundua ya kwamba mwovu alikuwa…... ni mwongo na baba wa huo.


Ni rahisi kumlaumu Mungu kwa sababu ya huzuni za ulimwengu na uharibifu, lakini ukweli ni kwamba Shetani ndiye anayewajibika na kuleta maangamizi.

ITAENDELEA...





Wednesday, June 13, 2012

KWA NINI KUNA MAHANGAIKO DUNIANI?


Yawezekanaje Mungu wa upendo akayaruhusu?

SEHEMU YA 1.
Clara Anderson alikuwa mjakazi jijini San Francisco, na Clara alikuwa mwanamke muungwana sana - na pia mwaminifu sana.! Siku moja baada ya kuwa mtendakazi kwa muajiri mmoja kwa miaka 15, alitoweka.! Muajiri wake hakujua alipokwenda. Alikuwa tu kama aliyetokomea toka machoni pa watu.! Kisha kwa namna ya ajabu, baada ya siku za kutafuta, idara ya jiji ya ustawi wa jamii ikampata.! Clara alikuwa katika mpango wa 'mgomo wa kula hadi kufa' katika kificho cha mlima nje ya San Fransisco. Akasema, Nataka kufa. Niacheni. Wakati mwandishi wa habari aliyemkuta alipomhoji, Clara
alisema,! Tazama , hakuna anayenijali. Mimi ni kijakazi tu - mmoja tu kati ya maelfu katika jamii watendao kazi za kinyonge. Maisha yangu hayana thamani. Sina ndugu wa karibu, sina jamaa, sina marafiki. Mimi ni mpweke kiasi kwamba sihitaji kuishi. Hakuna ninaye mdhani kuwa wa karibu nami - sina niwezaye kuzungumza naye, hayupo niwezaye kufungua moyo wangu kwake. Hivyo niacheni tu nife, kwa sababu hakuna kwa kweli anayejali.

Hakuna anayejali! ndicho kilio cha wanaume na wanawake katika sayari iliyo pweke.!
Hivi karibuni katika utafiti kuhusu Mungu, watu waliulizwa, Kama ungemuuliza Mungu swali moja, hilo swali lingelikuwa lipi?!
Vipi wewe? Kama ungemuuliza Mungu swali moja, lingelikuwa lipi? Tazama jinsi ambavyo mamilioni wangeuliza:! Mungu , je, kweli unanijali? Kama wewe ni mwema hivyo, kwa nini kuna maradhi mengi kiasi hiki? Mbona mahangaiko na mauti duniani?! Mbona kuna kuvunjika moyo hivi na huzuni?! Mbona kuna njaa, mafuriko, maafa yatokanayo na nguvu za asili, na vita?

Tuanatazama mazingira na tunatambua nguvu za kiovu zilizomo duniani.!
Kila mahali kuna maafa ya kutisha yanayotokea kila siku.

Ni nani anayewajibika kwa sababu ya maafa, shida, na taabu katika dunia?! Watu wengi humlaumu Mungu kwa matatizo wanayopitia.! Mara kwa mara utawasikia wakiuliza swali, Kwa nini Mungu alitenda hivi kwangu?
Hebu tutizame kile ambacho Biblia inasema juu ya pambano kuu linaloendelea kati ya nguvu za wema na zile za uovu.! Waweza kuuliza, Kama Mungu haleti shida zote hizi na huzuni duniani, ni nani anayewajibika kwa maafa yote haya tunayoyashuhudia?

Biblia inasonda kundi lenye makosa!! Yesu alieleza 
kisa juu ya mkulima alliyepanda mbegu ndani ya shamba, lakini mimea ilipokua, kulikuwa na magugu ndani ya shamba. (Fungu: Mathayo 13:27) !
Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, "Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako.
Sasa magugu yametoka wapi?" ! Walitaka kujua, magugu yalitokea wapi.

(Fungu: Mathayo 13:37) ! Yesu akawaambia, Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao ufalme wa mbinguni ni wao,lakini yale magugu ni wale watu wa yule mwovu. Adui aliyepanda yale magugu ni ibilisi.
Mathayo 13:37-39! Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.

Unaona, wakati Mungu anapojaribu kuonyesha wema kwa kila mmoja, kuna nguvu nyingine itendayo kazi duniani iletayo maafa, misiba, mauti, na maradhi kwa maisha ya wana wa Mungu.

Kitabu cha mwisho cha Biblia, Ufunuo, kinatuambia jinsi mambo yalivyoanza ili tuwe na ukweli hakika juu y kile kilichotokea mbinguni na kusababisha taabu kubwa namna hii katika Sayari Dunia.! Tutagundua chanzo cha uovu. Waweza kushangaa,lakini kulipata kuwa na vita mbinguni!

Kisha kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake. na joka hilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa na nafasi tena juu mbinguni kwa ajili yake na malaika wake.
Basi joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia ibilisi au shetani. Ndiye anayeudanganya ulimwengu wote;
Naam, alitupwa duniani, na malaika wake pamoja naye.! Ufunuo 12:7-9.
Sasa, tazama jinsi huyu joka, au mwovuanavyotambulia katika Ufunuo 12:3,4:

Ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.
Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani...
Ni wazi kwamba theluthi moja ya malaika wa mbinguni walimfuata mdanganyifu katika uasi wake dhidi ya Mungu.!
Lakini hebu tuchunguze zaidi juu ya huyu malaika aliyeanguka aitwaye Lusifa.! Katika Agano la Kale anatajwa kama Mfalme wa Tiro, na yasema hivi juu yake: Ni wazi kwamba theluthi moja ya malaika wa mbinguni walimfuata mdanganyifu katika uasi wake dhidi ya Mungu.! Lakini hebu tuchunguze zaidi juu ya huyu malaika aliyeanguka aitwaye Lusifa.! Katika Agano la Kale anatajwa kama Mfalme wa Tiro, na yasema hivi juu yake: (Fungu: Ezekieli 28:12 -14)!
Bwana MUNGU asema hivi: Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.! Ezekieli 28:12.

Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako....! Ezekieli 28:13.
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye...ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu; umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.! Ezekieli 28:14

Lusifa alikuwa malaika mkamilifu, aliyeumbwa kwa ukamilifu kwa namna zote.! Alikuwa malaika aliyesimama mbele za Mungu kama kerubi afunikaye.

Lusifa alishikilia nafasi iliyotukuka huko mbinguni. Katika pande zote mbili za kiti cha rehema au cha enzi cha Mungu kulikuwa na malaika wawili-mmoja kulia na mmoja kushoto. Mmoja wa hawa alikuwa Lusifa.
Hakuridhika kwa kuwa karibu hivyo na Mungu.! ALITAKA KUWA MUNGU!! Kitu kilitokea kwa Lusifa katika uhusiano wake wa karibu na Mungu. Mungu alimwambia Lusifa, (Fungu: Ezekieli 28:15)!
Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.! Ezekieli 28:15. (Fungu: Ezekieli 28:17).
'Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako...;! Ezekieli 28:17.

Huyu malaika mzuri, aliyetukuka akajipenda nafsi. Alitamani utukufu na heshima iliyomstahili Mungu pekee. Akawa na uchu wa madaraka. Akawa na ujasiri wa kumpa changamoto Muumbaji hata katika swala la utawala wa ulimwengu! Sikiliza kwa makini: Fungu: Isaya 14:12-14)!
Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa..........

Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu... .....Nitafanana na Yeye Aliye juu.! Isaya 14:12-14.

Maneno haya ya kiburi yalipoendelea kumiminika toka midomoni mwa Lusifa, upendo ulio kamili na amani ya mbinguni vikavunjwa vunjwa katika mamilioni ya vipande vidogo vidogo vya uchoyo.

Haikuchukua muda hadi Lusifa alipoanza kusambaza roho ya kutoridhika kati ya malaika wengine.! Pole pole bali kwa uhakika, aliharibu upendo wa Mungu na haki yake.


Kama tunda lililooza kwenye tenga, uasi wake ulienea kwa malaika wengine mbinguni.!
Pengine unashangaa kwa nini Mungu hakumuangamiza Shetani wakati ule.! Mungu angeweza kuwaangamiza Lusifa na malaika
waliojiunga naye katika uasi kwa muwako mmoja tu wa kupofusha, lakini kama angefanya hivyo, viumbe wote wangemtumikia kwa hofu.
Mungu ni Mungu wa upendo. Aweza tu kuwa na furaha katika mahusiano ya upendo na viumbe Vyake ambapo wanamwabudu kwa sababu wanampenda na kumuamini.
Shetani alikuwa ametoa changamoto kwa sheria za Mungu na haki yake, lakini Mungu hakuwa ameweka sheria hizi kwa mabavu ili aonyeshe ni nani aliye mkubwa! Aliziweka kulinda viumbe Wake,
kuhakikisha amani yao na furaha.

Sheria zake ni kama taa na alama zionyeshazo mwendo kasi ulio salama vyote vikiwa vimepangwa kwa ajili ya usalama wetu na kwa ubora wetu.! Bali huyu aliyeheshimika kati ya malaika wote alidhani ya kwamba angeweza kuendesha ulimwengu kwa ubora kuliko Mungu Muumbaji wake!

Shetani, adui wa Mungu , alijifanyia 'mwovu' ndani yake!






ITAENDELEA KATIKA SOMO LIJALO...............