Wednesday, June 6, 2012

UUMBAJI.


HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI!
Fungu la tafakari: “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea Utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliye viumba vitu vyote, na  kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.” Ufunuo 4:11.

Makusudi ya somo hili: Kujifunza ni nani aliumba  ulimwengu na uliumbwa kwa nanna gani.

UTANGULIZI…
Ingawa wana sayansi wengine hujaribu kueleza kwamba Mungu hakuumba binadamu na dunia, Biblia hutufundisha kwamba “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbigu na nchi” (Mwanzo 1:1) na kwamba binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Katika somo la leo tutajifunza ukweli huo na kuona kuwa dunia na vyote vilivyomo havikutokea kwa njia ya mabadiliko ya polepole ya vitu asilia, Bali “ kwa Neno la Bwana” Zaburi 33:6.

Utatu Mtakatifu ulihusika kikamilifu katika Uumbaji wa ulimwengu huu. Mwanzo 1:1,2,26; Yohana 1:1-3; Waebrania 1:2.
Biblia hufundisha kuwa Umoja wa nafsi tatu za milele ulishirikiana kuanzisha historia ya mwanzo wa binadamu na ulimwengu. Mungu Mwana (Kristo) alikuwa ndiye wakala nkuu wa uumbaji, sababu hakuna kiumbe chochote kilichoumbwa pasipo yeye. Mungu Roho Mtakatifu alikuwa na sehemu ya kufanya.

Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Zaburi 33:6-9;
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Ebrania 11:3.

Neno la Mungu halikuwa tu na nguvu ya kuumba ulimwengu, bali lina nguvu pia ya kuutegemeza (Waebrania 1:3)
Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. Isaya 45:18; Zaburi 19:1-4.

Siku sita za Uumbaji:
Siku ya 1: Mungu aliamurisha mwanga kuwepo kwa kutenganisha nuru na giza. Hii ndiyo asili ya kuwepo mchana na usiku. Mwanzo 1:2-5.

Siku ya 2: Mungu aliamuru anga kuwepo kwa kuyatenganisha maji. Mwanzo 6:6-8.

Siku ya 3: Mungu aliamuru nchi kavu, bahari, miti, mimea na majani kuwepo. Mwanzo 1:9-13.

Siku ya 4: Mianga mitatu (Jua, Mwezi na Nyota) viliamrishwa kuwepo. Mwanzo 1:14-19.

Siku ya 5: Ndege , Samaki na wanyama wa baharini na ziwani pamoja na viumbe wengine wanaoishi majini waliamrishwa kuwepo. Mwanzo 1:20-23.

Siku ya 6: Wanyama wa kufugwa, wanyama wa porini na vyote vitambaavyo juu ya nchi viliwekwa. Binadamu aliumbwa siku hiyo pia. Mwanzo 1:24-27.

Siku sita za uumbaji zilikuwa siku halisi kabisa, kila siku ikiwa na saa 24.
Siku hizi hazikuwa mifano ya kuwakilisha maelfu au mamilion ya miaka, kama wengine wanavyofikiri.

Baada ya siku sita za uumbaji kumalizika tunaona siku nyingine ya muhimu sana na ndiyo chimbuko la ibada zote duniani. Maana tumeubwa tukiwa na asili ya kuabudu ndani yetu. Haijarishi unaabuni nini, ama unamwabudu nani. Lakini makusudi ya Mungu anataka tumwabudu yeye peke yake.

Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Mwanzo 2:1-4.
HIVI NDIVYO MIMI NA WEWE TULIVYOUMBWA NA MUUMBAJI WETU NA VYOTE VINAVYO ONEKANA. NA SI VINGINEVYO. NDO UKWELI WA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA).
 






























AHASANTE KUWA PAMOJA NAMI KATIKA SOMO HILI.

No comments: