Monday, December 31, 2012

MILANGO MIWILI NA NJIA MBILI



(Na Pr. Nziku Herbert)


                    Fungu La Maandiko: Mathayo 7:13, 14
 
“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”
  1. Yesu alitumia vielelezo viwili katika kufikisha ujumbe kwa wasilikizaji wake, MLANGO na NJIA.
    Alizungumza juu ya milango ya aina mbili, Mlango mwembamba na Mlango mpana.
    Alizungumza kuhusu njia za aina mbili, Njia iliyosonga na Njia pana.
    Alisema Mlango mpana na Njia pana huelekea UPOTEVUNI
    Aliendelea kusema kuwa Mlango ulio mwembamba na Njia iliyosonga huelekea UZIMANI
    Yesu aliwaona watu WENGI wakishika njia pana na kuingia kwa mlango mpana, yaani kuelekea UPOTEVUNI.
    Aliona kundi lingine la watu WACHACHE wakishika njia iliyosonga na kuingia kwa mlango ulio mwembamba, yaani kuelekea UZIMANI.
    Wanaoiona njia iendayo uzimani ni wachache.
    Akatoa wito kwa wasikilizaji wake kwamba, “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba”


    Mpendwa mgeni na msafiri juu ya nchi pamoja nami,

    •          Maneno haya ya Yesu yaliandikwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita na bado ujumbe wake kwetu ni wa muhimu.

    •            Ni ujumbe unaomweka wazi kile kinachoendelea katika ulimwengu yaani pambano kuu kati ya wema na uovu.
      •  Ni ujumbe unaomtaka kila mwanaume na mwanamke aliye hai chini ya jua kutafakari na kuchukua hatua, ama kuingia kupitia njia iliyosonga na mlango mwembamba, au kushika njia pana na mlango mpana.
      • Aidha ni ujumbe unaomtaka kila mwanadamu kuamua na kuchagua ni wapi anakotaka kuelekea, UPOTEVUNI au UZIMANI.
      •  Ni ujumbe wenye wito ndani yake, kwani yeye asiyekosea, yeye anayeyafahamu maisha yetu na mwisho wake, anatuagiza kwamba, Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba.
      •  Kwa sababu hili ni suala la kufa ua kupona, na kwa sababu Yesu anajua gharama aliyotumia kukukomboa wewe na mimi; anahitaji tupate uzima, ndiyo maana anasema, “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba”
       
    ITAENDELEA.....