Tuesday, June 19, 2012

KWANINI KUNAMAHANGAIKO DUNIANI?


Sehemu ya 3

Shetani ndiye aliyeleta taabu kwa sayari hii na ndiye ambaye amekuwa akisababisha dhambi na mateso tangu hapo. Yesu alimfichua mwovu na jinsi anvyotesa watu.
Siku zote yeye amekuwa akiwafunga watu kwa magonjwa ya ajabu na ajali vita majanga ya kila namna Shetani ndiye kiongozi.
Katika Biblia tunaona kisa cha mwanamke aliyefungwa na Shetani miaka 18, Yesu alibainisha kuwa amefungwa na shetani, yampasa kufunguliwa. Yesu akamponya yule mwanamke. Luka 13:16

Pengine hakuna mahali katika Biblia tuwezapo kuona mkakati wa Shetani kwa wazi zaidi kuliko ulivyo fichuliwa katika sura ya kwanza ya kitabu cha Ayubu, katika mazungumzo kati ya mwovu na Mungu.
Ilikuwa wakati fulani baada ya kuanguka kwa Shetani kwamba wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana. Shetani naye
akaenda kati yao.! Fikiria hili! Mkutano wa wana wa Mungu, na Shetani akaja bila kualikwa! (Fungu: Ayubu 1:7)

BWANA akamwuliza Shetani, 'Umetoka wapi wewe?' ! Ayubu 1:7
Kwa maneno mengine,ni nani aliyekualika? Una haki
gani ya kuwa hapa? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Ayubu 1:7 Shetani alidai miliki juu ya Sayari Dunia.

Alikuwaamenyakua nafasi ya Adamu! Adamu anaitwa mwana wa Mungu (Angalia Luka 3:38), kama tu wale wengine waliokuja siku ile kwa ajili ya mkutano na Mungu.
Je, yawezekana ya kwamba walikuwa ni viongozi wa dunia zingine, kama jinsi ambavyo Adamu alikuwa awali kiongozi wa ulimwengu wetu?! Kwa vyovyote vile, dai la Shetani la kuwakilisha Dunia halikupita bila kupingwa. Bwana akamwuliza Shetani; (Fungu: Ayubu 1:8,9,11) ..... 'Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu?

Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je, huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako'

Ni changamoto kubwa kiasi gani! Siku hiyo Shetani alidai ya kwamba sababu pekee ambayo kwayo Ayubu alimtii Mungu ilikuwa ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu alimtendea, na si kwa sababu alimpenda na kumtumaini Mungu. (Fungu: Ayubu 1:12)
BWANA akamwambia Shetani,' Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake mwenyewe.'Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA. Ayubu 1:12. Shetani aliondoka, akiwa na shauku ya kutia mikono yake katika mali ya Ayubu.

Mara mapigo yakaanza kuanguka: Kwanza: Waseba wakaiba ng'ombe wa Ayubu na kuwaua wafanyakazi wake.

Pili: Radi ikapiga, na kua kondoo wake na wachungaji wake.






Tatu: Wakaldayo walikuja na kuteka nyara ngamia wa Ayubu.







Nne (habari ya kuvunja moyo mno): kimbunga kiliipiga nyumba ya kijana mkubwa wa Ayubu. Karamu ilikuwa ikiendelea, na watoto wote kumi wa  Ayubu waliokuwemo wakauawa

Maskini Ayubu alidhani kwamba Bwana alikuwa amechukua mali yake na kusababisha msiba wote huo. Hakuelewa ya kwamba mwovu ndiye alikuwa ametenda hiyo Hata ingawa alizidiwa na huzuni, uaminifu wa Ayubu kwa Mungu haukubadilika.
Akasema, ....BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Ayubu 1:21
Ingawa hakuelewa misiba iliyoangamiza mali zake na watoto, Ayubu alidumu tu kutumaini wema wa Mungu. Lakini Shetani alikuwa hajamaliza. Akampa Mungu changamoto tena akisema, Ayubu 2:4-6
...Naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Ayubu 2:4-6.
Lakini sasa nyosha mkono wako,uuguse mfupa wake na nyama yake,naye atakufuru mbele za uso wako.
Jaribu lilikuwa tayari limeanza Je, Ayubu angesalia kuwa mwaminifu kwa Mungu wakati makali yatakapozidi kuwa makali, ama atamwacha Mungu?
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa. Ayubu 2:7.

Kama umewahi kupata na jipu, unajua jinsi ambavyo jipu moja tu linavyoweza kuuma.Fikiria sasa kitendo cha kufunikwa na majipu toka utosini hadi wayo wa mguuni.

Hata ingawaje Shetani alikuwa amempokonya Ayubu mali yake, watoto wake, na afya yake, Ayubu alisalia mwaminifu kwa Mungu. Mtu wa namna gani huyu! Biblia inasema, Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu. Ayubu 1:22.

Ni nani aliyemuumiza Ayubu? Ni nani aliyemletea mapigo Ayubu?
NI SHETANI.

Ni nani aliyeiba mifugo yake na kuua watumishi wake? Ni SHETANI!

Ni nani aliyeleta kimbunga kilichoteketeza wana na binti zake! Ni SHETANI.


Bwana anaweza kuruhusu matatizo yaje ili kujaribu utii na upendo wetu, bali SHETANI ndiye mwenye hatia kwa ajili ya uovu wote uliopo kwenye Sayari Dunia!

ITAENDELEA...

No comments: