Sunday, June 3, 2012

KITABU CHA MAAJABU

KUNAVITABU VINGI HUMU DUNIANI LAKINI HIKI NI YOTE KATIKA VYOTE.


Fungu la tafakari:- Majani yakauka au lanyauka, bali neno la Mungu wetu litasimama milele.” Isaya 40:8

Kusudi la somo hili:- Kuonesha kuwa Neno la Mungu lililoandikwa – Biblia, ni ufunuo wa Mungu kwa wanadamu.

UTANGULIZI:

Tunaye Mungu mmoja wa kweli aishie milele. Amejtambulisha kwa wanadamu kwa kuangalia kazi zake alizozifanya.

Tena tunazo njia za maana ambazo kwazo tunaweza kumfahamu kama fundisho hili linavyofundisha.

Je, Biblia inatambuliwaje na waandishi wake? Warumi 1:2; 2Timotheo 3:15

Inatambuliwa kama mafundisho au maandiko. Maana ya “Maandiko” ni Neno la Mungu.

Mungu ndiye aliyeongoza kazi yote ya uandishi, maana watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 2Petro 1:21

Maandiko haya yalitolewa na Mungu ili kutuonya sisi na kutuadibisha katika haki.

2Timotheo 3:16.

Watakatifu wa Mungu, waliohusika katika uandishi wa Biblia walitoka katika taifa la Kiebrania, taifa lililo chaguliwa na Mungu, kumwakilisha katika ulimwengu huu.

Mungu hakuwaacha waandike kwa kutegemea utashi wao pekee isipokuwa aliwaongoza kuandika kama alivyopenda.

Mungu ndiye aliyesema na manabii.. Ebrania 1:1; Ufunuo 1:1.

Wao walikuwa ni vyombo vya kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu.

Roho wa Mungu alinena na Manabii, nao wakayandika. Matendo 1:16; 2Samweli 23:2.

Kwa nini ni ktabu cha maajabu.

Watu arobaini waliandika Biblia. Na waliishi miaka 4000 iliyopita... Kunamaneno yaliyoandikwa na wafalme, wana wa kifalme, watunga mashahiri, wenye hekima, wenye elimu ya rugha, wavuvi, wenye maarifa ya utawala. Watu waliojifunza elimu ya Misri,

Walioelimishwa katika skuli ya Babeli, waliofundishwa mjini Yerusalemi. Liliandikwa na watu waliohamishiwa mbali kutoka kwao, katika mjangwa, katika mahema ya wachungaji, katika malisho ya kijani. Mbali na haya miongoni mwa wandishi tunaona wakusanyaji wa kodi, Wachungaji, wakusanyaji wa matunda, watu maskini, watu matajiri, watawala, wahubiri, majaji, watu wakila dalaja na wakila darasa wanakuwa mawakili wake katika ullimwengu huu. Biblia inayo kila namna ya maandiko, ni michanganyiko inayotengeneza idadi ya vitabu 66 vilivyoandikwa kwa watu wa kawaida.

Ajabu kubwa zaidi; wandishi wa Biblia hawakukaa nchi moja ama sehemu moja, lakini maandishi yao yalipounganishwa yakaoana, yakalingana kana kwamba yameandikwa na mtu mmoja. Huo ni utendaji mkuu wa Mungu mwenyewe.

Maandiko, yanatuhekimisha hata tunapata wokovu, 2Timotheo 3:15

Neno la Mungu linabadili na kugeuza mioyo yetu linaukali kuliko upanga ukatao kuwili.

Hakuna aliyekuja kwa Yesu akabaki kama mwanzo, lazima neno limbadilishe. Ebrania 4:12.

Kunauwezo unaoelimisha, Biblia haina mpinzani, katika Neno la Mungu akili hukutana na somo lenye hoja za kina, kirefu, matamanio ya juu. Biblia ni historia yenye mafundisho ambayo wanadamu wakiyafuata wanapata uzima. Ilikuwa safi kutoka kwenye chemichemi ya kweli yenye uzima, na mkono wa Mungu umeuhifadhi usafi wake katika katika zama zote.

Katika neno la Mungu tunauona uwezo ule ulioiweka misingi ya dunia na kuzitandaza mbingu. Hapa matatizo makubwa ya uwajibikaji, na hatima ya badaye yanafunuliwa.

Katika kutafakari kwa kicho ukweli kama ulivyoelezwa katika neno lake, mawazo ya mwanafunzi yanakutana na akili asiyo na kikomo katika ushirika wa karibu. Kujifunza kwa namna hiyo hakukuzi tu na kuboresha tabia, bali pia kutapanua na kuhamasisha nguvu za kiakili.

Tunasafisha njia zetu kwa kutii na kufuata neno lake, Zaburi 119:9,15.

NENO LA MUNGU LADUMU MILELE ISAYA 40:8

WITO TUSOME NENO LA MUNGU NA KUTII.

 

 

 


No comments: