Saturday, June 16, 2012

KWA NINI KUNAMAHANGAIKO DUNIANI?


Sehemu ya 2.

Mungu anampa kila mtu uwezo wa kutii ama kutotii.! Kutokana na haki na upendo, Mungu amemruhusu Shetani kueleleza kwa ulimwengu jinsi ambavyo angeuongoza ulimwengu.! Hatuelewi jinsi yote haya yalivyotokea wakati Mungu alikuwa mwema na mwenye upendo kwa wote.

Pambano lililoanza mbinguni halijaisha, limebadilisha tu viwanja!!
Sasa Dunia ni eneo ambamo pambano kuu kati ya wema na uovu lingepiganwa, ambapo shetani angeeleleza aina yake ya serikali na jinsi ambavyo angeliiongoza dunia.

Lakini kwa nini Dunia? Kwa nini sayari yetu ikawa ....
(Fungu: 1 Wakorintho 4:9)! .... tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu. ! 1Wakorintho 4:9.

Dunia ilikuwa ndipo tu imetoka mikononi mwa Muumbaji, ikiwa inang'aa na ikiwa kamilifu, nzuri kuliko maelezo.! Ni wazi Shetani alifikiri vivyo pia, kwani aliiona dunia hii kama tunu ufaayo kuikamata.!
Angejaribu kuikamata sayari hii ikiwa katika uzuri uwezao kuvunjika - dunia ambayo ndipo imezaliwa.

Ingawa Adamu na Hawa, baba na mama wa wanadamu, waliumbwa wakamilifu, hawakufanywa wawe juu kuliko uwezekano wa kutenda makosa.
Walikuwa huru kuchagua kumpenda na kumfuata Mungu ama kutojali maelekezo Yake.! Lakini utii wao ulipaswa kujaribiwa, na jaribu hilo lingewekwa kwenye mti. Mungu alionya, (Fungu: Mwanzo 2:16,17)!
Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula; walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula
matunda ya mti huo utakufa hakika.! Mwanzo 2:16,17.!
Hilo laonekana kuwa lilikuwa ombi la busara. Lazima walijihisi salama kabisa. Lakini mtu yuko katika hatari kubwa akutwapo bila kujilinda kwa sababu hujihisi yu salama.

Hicho ndicho kilichotokea kwa Hawa.! Shetani alitumia uwezo wake upitao akili ya mwanadamu ili kumdanganya.! Shetani hutenda kazi hadharani kwa nadra. Yeye ni mdanganyifu sana.! Anatumia mifumo ya jamii, watu, au hata nyoka!

Kwa sababu hiyo Paulo anasema: (Fungu: Waefeso 6:11-12)!
Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Maana vita vyenu si kati ! yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.! Waefeso 6:11,12.

Hawa alidanganywa.! Hakudhani maneno yaliyotoka kwa nyoka yalitoka kwa Shetani.! Mwovu, akinena kupitia kwa joka, alimwambia,
(Fungu: Mwanzo 3:1)! ....Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?! Mwanzo 3:1. (Fungu: Mwanzo 3:2-4)!
Hawa akajibu, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini atunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, 'Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Nyoka akamwambia mwanamke, 'Hakika hamtakufa.' ! Mwanzo 3:2-4

Hawa alipokuwa akimsikiliza joka, lazima lilipita wazo ghafla kichwani kwamba alikuwa akinena tofauti na na jinsi Mungu alivyowaambia.! Pengine kwa kuhisi ya kwamba alionekana kuchanganyikiwa, joka kwa upesi aliongeza, (Fungu: Mwanzo 3:5)! Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema
na mabaya.! Mwanzo 3:5.

Mwovu alipendekeza ya kwamba Mungu hakufanya haki, kwamba alikuwa akizuia kitu fulani kizuri.! Kuwa kama Mungu ilikuwa tamaa kubwa iliyomla Shetani na kuwa chanzo cha maanguko yake. Sasa
Hawa pia aliliona kuwa wazo zuri pia; na kwa  haraka bila kufikiri, aliuzika. (Fungu: Mwanzo 3:6)!
Mwanamke alipoona kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala...! Mwanzo 3:6.

Akampa na mumewe, naye akala.
Adamu na Hawa wakashindwa jaribio la Mungu la upendo na utii, na haikuchukua muda mrefu kwa wao kugundua ya kwamba kuna jambo limeharibika.

Shetani alikuwa ameteka nyara dunia iliyozaliwa karibuni! Tangu wakati huo, akadai cheo cha , Mfalme wa Dunia hii.! Mtawala wa sayari iliyo katika uasi!! Adamu na Hawa walikuwa wameisikiliza sauti ya mwovu.

Kadiri siku hii ya msiba mkubwa ilipokuwa inafikia mwisho, Mungu akaja jioni wakati wa jua kupunga kama kawaida yake, akiwaita Adamu na Hawa.! Hadi sasa, huu ulizoeleka kuwa wakati wa furaha
mno wa siku - fursa ya kutembea na kuzungumza na Mungu moja kwa moja Yeye aliyewaumba. Lakini katika siku hii walikimbia na kujificha vichakani!
Hatimaye Adamu akachomoka pole pole kutoka nyuma ya vichaka katika bustani na kukiri kosa.

Muhtasari (Fungu: Mwanzo3:10)! ....Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi, nikajificha.! Mwanzo 3:10.

Muhtasari Adamu alikuwa hajapata kuogopa kabla ya hapo, lakini hicho ndicho dhambi inachofanya.! Inamfanya mtu amuogope hata Mungu. (Fungu: Mwanzo 3:11)! Mungu akajibu, ...Je! Umekula wewe matunda ya mti niliokuagiza usiyale?! Fungu 11.! Adamu akajibu: (Fungu: Mwanzo 3:12)! ...Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.! Mwanzo 3:12!
Saa chache kabla ya hapo, Adamu alikuwa tayari kufa pamoja na Hawa.! Sasa alimlaumu na pia akamlaumu Mungu kwa kumuumba. Jinsi gani dhambi inavyovunjavunja upendo uliomkamilifu!

Lakini Hawa naye hakushindwa kushitaki. Mungu alipomuuliza juu ya kile alichokuwa ametenda, alijibu, Muhtasari (Fungu: Mwanzo 3:13)!
....Nyoka alinidanganya, nikala.! Mwanzo 3:13.! Hawa alimshutumu Mungu pia! Kwa maneno mengine, alikuwa anasema, Ni nyoka uliyemuumba  ndiye aliyeniingiza taabuni.

Siku ile ile Adamu na Hawa wakawa chini ya kifo! Ili kuwazuia Adamu na Hawa wasile matunda ya mti wa uzima, Mungu akawaondoa kutoka kwenye nyumba yao ya bustani. ! Mwovu alisema ya kwamba wasingekufa, bali Biblia yasema, Muhtasari (Fungu: Mwanzo 5:5)!
Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. Mwanzo 5:5! Wakiwa wamechelewa kabisa waligundua ya kwamba mwovu alikuwa…... ni mwongo na baba wa huo.


Ni rahisi kumlaumu Mungu kwa sababu ya huzuni za ulimwengu na uharibifu, lakini ukweli ni kwamba Shetani ndiye anayewajibika na kuleta maangamizi.

ITAENDELEA...





No comments: