“Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani” Zaburi 106:19,
20.
Wakati Musa akiwa hayupo, mamlaka ya kufanya maamuzi
yalikasimishwa kwa Haruni, na umati mkubwa ukakusanyika kulizunguka hema
lake, wakiwa na dai hili: “Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda
mbele yetu, kwa maana Musa huyo… hatujui yaliyompata.” Kuhusu lile
wingu, walisema, . . . sasa limetulia kabisa pale
mlimani; na lisingeendelea tena kuelekeza safari zao. . . . Zahama kama
hiyo ilimhitaji mtu thabiti, mwenye uamuzi imara, na ujasiri usioyumba;
yule ambaye ameinua juu heshima ya Mungu kuliko umaarufu wa kupendwa na
watu, usalama binafsi, au uhai wenyewe. Lakini kiongozi huyu wa Israeli
hakuwa na sifa hizi za kitabia.
Haruni alipingana na watu hawa kinyonge, lakini tabia yake ya
kutetereka na woga katika wakati huo hatari sana uliwafanya tu watu hao
kuwa washupavu zaidi…. Wapo baadhi walioendelea kuwa waaminifu kwa agano
lao pamoja na Mungu, lakini sehemu kubwa sana ya watu hao ilijiunga
katika uasi….
Haruni alihofia usalama wake mwenyewe; na badala ya
kusimama kwa uadilifu ili kutetea heshima ya Mungu, alikubaliana na
madai ya umati huo. . . .
Alitengeneza sanamu ya ndama wa
kuyeyusha, kwa kuiga mfano wa miungu ya Misri. Watu hao wakatangaza,
“Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”
Na Haruni kwa uovu akaruhusu tu fedheha hii dhidi ya Yehova. Na alifanya
zaidi ya hili. Baada ya kuona jinsi mungu huyo wa dhahabu
alivyopokelewa kwa ridhaa, alijenga madhabahu mbele yake, kisha
akatangaza akisema, “Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana.”
Tangazo hili lilienezwa kwa matarumbeta toka kundi moja hadi lingine
katika mahema yao yote…. Chini ya kisingizio cha kuadhimisha “sikukuu
kwa Bwana,” walijiingiza katika shamrashamra za ulafi na ufisadi.
Ni mara nyingi kiasi gani, hata katika siku zetu, ambapo kupenda anasa
kunafunikwa kwa “mtindo wa utauwa!” Dini inayowaruhusu wanadamu
wajihusishe katika uendekezaji wa ubinafsi au tamaa za kimapenzi, huku
wakiendelea kufanya taratibu zao za ibada, huwavutia watu wengi sana
wakati huu kama ilivyokuwa katika siku za Israeli.
No comments:
Post a Comment