Basi, kabla ya sikukuu ya pasaka ,Yesu,hali akijua kwamba
saa yake imefika,atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba,naye
amewapenda watu wake katika ulimwengu,aliwapenda upeo,Yesu hali
akijua ya kwamba Baba amempa vyote mikononi mwake,na ya kuwa
anatoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,aliondoka
chakulani,akaweka kando mavazi yake,akatwaa, kitambaa akajifunga
kiunoni.Kisha akatia majia katika bakuli,akaanza kuwatawadha miguu
na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga….Basi alipokwisha
kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi
tena,akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? Basi ikiwa
mimi, niliye Bwana na Mwalimu,nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo
KUTAWADHANA miguu ninyi kwa ninyi...Kwa kuwa nimewapa kielelezo;
ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. YOHANA 13:1-151
Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,Naye akiisha
kushukuru akaumega, akasema,Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili
yenu; fanyeni hivi kwa UKUMBUSHO wangu. Na vivi hivi baada ya
kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya
katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa UKUMBUSHO
wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki,
MWAITANGAZA MAUTI YA BWANA HATA AJAPO WAKORINTHO 11:23-26
KUHUSU (EASTER)?
Easter Ni sherehe inayojulikana sana ambayo,inaadhimishwa na
makanisa yetu ya siku hizi. Walakini hii pia ilisherehekewa na
wapagani muda mrefu kabla ya ufufuo wa Kristo.
Siku zote
Pasaka inaangukia Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu (full
moon) mara tu baada ya jua kuwa kichwani kaskazini ya Ikweta
(Equinox ---March 2l).Wapagani wale wa zamani za kale waligundua
ya kwamba kila kitu kilionekana kupata uzima mpya mapema
katika majira yale ya kuchipua (Spring), mara tu baada ya jua
kupita mstari wa ikwinoksi (equinox) kaskazini ya Ikweta. Basi
wakachagua siku moja katika majira ya kuchipua [Machi, Aprili,
Mei] ili KUMHESHIMU mungu WA KIKE WA UZAZI. Siku ile ikatolewa
kwa ISHTA (ISHTAR), mungu wa kike wa uzazi, kwa sababu ya uhai
mpya na kukua kwa mimea ya asili.
Neno lilo hilo ISTA
(EASTER) limeandikwa kwa herufi nyingine zisizokuwa za lugha
yenyewe kutokana na jina la mungu huyo wa kike ISHTA (ISHTAR),
ambaye ibada yake iliwekewa ukumbusho wake kwa kutumia sikukuu ya
Ista (Easter) [Pasaka]. Mara nyingi Wakristo walei [wa kawaida]
wameuliza ya kwamba ule mkate mdogo kama sungura (bunny rabbit)
na yai la Ista (Easter egg) vina uhusiano gani na ufufuo wa
Kristo. Kusema kweli, havina uhusiano wo wote na [ufufuo] huo.
Sungura alichaguliwa kwa sababu alikuwa anazaa sana. Yai pia
lilichaguliwa kwa sababu lilikuwa nembo ya kuzaa sana. Hata
nembo hizo zenyewe, mkate mdogo kama sungura na mayai,
vinatunzwa kama ukumbusho wa asili yake ya kipagani [ya siku
hiyo]. Mifano hii imetolewa ili kuonyesha tu jinsi ilivyokuwa
rahisi kwa Mwovu kulazimisha mawazo yale ya kipagani juu ya
kanisa lile. Swali linakuja mawazoni mwetu, Hivi
ni kweli tunaifuata Biblia katika mafundisho yetu yote ya dini?
Iwapo MAPOKEO na DESTURI za kipagani zimeweza kuteleza kwa
urahisi na kuingia kanisani, ni vipi kuhusu mafundisho mengine
ya dini?
Hatuna amri yo yote kuhusu uadhimishaji wa ufufuo au
kuzaliwa kwa Kristo. Tunaweza kutafakari juu ya ufufuo Wake na
kuzaliwa Kwake kwa wakati wo wote ule na katika siku yo yote
ile ya mwaka. Macho yetu na yafumbuke ili tupate kuyatambua
mafundisho hayo ya uongo na kuendelea kuwa watiifu kwa ile kweli
halisi katika mfumo wake wa asilia.
No comments:
Post a Comment