Ziara ya Vijana wa AY katika kundi la Kifanya, ilikuwa ni safari iliyojawa na furaha tele kwani Jemadari wetu Yesu alikuwa mbele yetu, akituongoza safarini.
Wakwanza kulia (waliosimama) ni Mkuu wa SS kanisa la Njombe. aliye simama katikati ni Mkuu wa AY kanisa la Njombe, yeye ni mfupi kuliko wote waliosimama. wapili toka kushoto ni Karani wa SS kanisa la Njombe, Picha ya pamoja baada ya kuwasiri Kifanya.
Kijana wa Yesu akiwa tayari kuingia nyumba kwa nyumba, kama unavyo muona katika picha
Waumini wa kundi la Kifanya pamoja na Vijana wa AY wakiwa kwenye ibada ya Shule ya Sabato, kwakweli ilikuwa ni Sabato ya pekee, furaha ilitawala.
Wanafunzi wa shule ya Kifanya wakiongoza Shule ya Sabato, ilikuwa ni Sabato ya pekee maana walitembelewa na Vijana wa AY toka Njombe.
Ukawadia wakati mzuuuri wa masomo katika madarasa, mbele ni mwalimu Meshack akiwa na baadhi ya watoto, pamoja na mwalimu Toba Kayombo. aliyeshika tama ni (Samwel Kenzeva) ni miongini mwa vijana wa PF toka Njombe.
Vijana pia hawakuwa nyuma kwenye mjadala wa Lesson, aliyesimama ni mwalimu Daniel Dickson, akisimamia dalasa hilo, pembeni ni gari walilosafiria, maarufu kama Majalada Trans, chini ya Dereva mahiri Zaward mwana wa Lupenza.
Aliye simama ni mwalimu wa Lesson maarufu kama (MSULE) ndiye msimamizi wa hilo. wa kwanza benchi la tatu ni Mwalimu wa Shule ya serikali, huko Kifanya anajulikana kwa jina la (Nyalusi).
wanadalasa wametulia wakitafakari somo katika Lesson, ya robo hii. Inayoitwa (Kumjua Mungu wetu).
Mzee wa Kanisa la Njombe (Erasto Mligo) aliyesimama mbele, yuko makini akihakikisha dalasa la Maandalio la Kundi la Kifanya wanaelewa kile wanachojifunza. Dalasa lilikua na mwitikio na usikivu wa hali ya juu.
Ibada kuu ikawadia, Vijana wamejipanga sawasawa kuhakikisha Bwana anainuliwa.
Wakwanza kushoto ni Mhazini wa Kundi la Kifanya anaitwa (Konrad Chengula) anayefuata ni mwalimu wa PF toka Njombe (Meshack Sanga)
Wakwanza kulia ni mwanadada (Anyesi Sanga) anaye fuata ni Mkuu wetu wa AY Njombe (Steven Kalinga) Ndiye aliyetoa neno la uzima siku hiyo.
Vijana wa AY, wakijipanga vema kuhakikisha wimbo wa kumkaribisha Mhubiri unaimbwa bila kukosea. wimbo wao ulikua ni mzuri ajabu, wenye ujumbe.. (Hatuna sababu ya kuogopa). naupenda sana!!
Mkuu wa AY Njombe, ndiye aliyekuwa Mhubiri siku hiyo, watu walibarikiwa sana na neno lake. kichwa cha somo (Urithi wa Mtoto wako ni nini?)
Vijana wa AY, na wimbo wao wa kuhitimisha Ibada ya mchana kwa siku hiyo. Vijana walijiandaa vyakutosha, sijawahi kumuona Mr.Daniel Dickson, akiimba kwaya, mwenyewe siunamwona pale nyuma? nahisi anatwanga sauti ya nne. hongera Daniel na vijana wa AY.
Ukawadia wakati haswaa, ambao ndo lengo la Vijana kwenda Kundini humo. walitawanya vijuzuu nyumba kwa nyuma, kulikuwa na changamoto za hapa na pale, lakini daima Yesu ni mshindi.
Wakwanza kulia ni mwenyeji wao toka kundi la Kifanya, anayefuata ni (Faraja Moses) toka Njombe. katikati ni (Rachel Castor) akiwa na binti yake wa kazi, wote kazini mwa Bwana.
Vijana wa AY wakigawa vijuzuu nyumba kwa nyumba, kama unavowaona wakimpa kijuzuu huyokijana hapo.
Vijana mahiri kazini mwa Bwana, wanaweka kola zao vizuri ili wawe na mwonekano mzuri. kulia ni (Steven Kalinga) sambamba na (Meshack Sanga)
Haya kijana wa Yesu, huyo ni (Meshack Sanga) nikama anahisi kitu fulani, mimi nadhani anatazama zaidi mbele na kuona niwapi aanzie kazi ya Bwana. hana wazo lingine zaidi ya kugawa vijuzuu kwa watu
Mrs,(Meshack) katika picha ya utulivu, akijiandaa kwenda nyumba kwa nyumba, nikama anafuraha kwani anaamini Bwana atamwongoza.
Haya, Vijana hao wakionyeshana njia ya kupita, ukitaka uone kuwa vijana wanaweza washirikishe kazini mwa Bwana. maana wananguvu.
Kazi ya Bwana lazima ifanywe na kila mtu haijarishi unaumri gani.
Mwenye suti nyeusi ni kijana (Samwel Kenzeva) akiwagawia vijuzuu baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi.
Katika kazi ya Bwana mwitikio ni wa muhimu, iwe kanisani au kwenye mikutano ya hadhara, kile unachokihubiri kinakuwa na thamani iwapo kunamwitikio. wanafunzi hao waliitikia mwito kwa kupokea vijuzuu vilivyotolewa na Kijana (Samwel)
Katika ufanyaji wa kazi ya Bwana hatupaswi kubagua, wasomi kwa wasio na elimu wate wanahaki ya kupata neno la Mungu.
Kulia ni (Meshack Sanga) akimgawia kijuzuu mwanafunzi wa sekondari ya Kifanya.
Kila kazi inachangamoto, hata kazi ya Bwana pia, unaweza ukampa mtu kijuzuu akakataa lakini watu wa Kifanya ni waungwana, walionyesha mwitikio. sifa na utukufu ni kwake aliye juu.
Baada ya dhiki ni faraja, baada ya mizunguko mingi ya nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa, katika mazingira yenye jua kali, maji ni muhimu. vijana wamesimama kwa utulivu wenye sura za tabasamu.
Picha ya kulia ni (Makonge) Picha ya kushoto ni Meshack)
Kuagana ni huzuni, lakini haina namna. hii ni picha ya pamoja Vijana wa AY na waumini wa Kundi la Kifanya, baada ya kazi ya kugawa vijuzuu.
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, Vijana wanajiandaa kurudi nyumbani. hilo ni gari walilolitumia siku hiyo.
Kwayote ashukuriwe Baba wa Mbingu na nchi kwa ulinzi wake na kwa yote aliyotutendea.
Picha zote kwa idini ya Idara ya Vijana Njombe.
Zimewekwa mtandaoni na JONAS TAVE. http:/jonastave.blogspot.com
2 comments:
Mlipendeza sana Bwana awabariki!!!
Ahsante mpendwa, ubarikiwe nawe pia.
Post a Comment