Kunakisa
katika biblia, huwa nashangaa sana..bwana Yesu katika pita pita yake
alikutana na watu 10 wenye ukoma wakasimama mbali, wakapaza sauti
wakisema Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! ...akawambia enendeni
mkajionyeshe kwa makuhani.
Wakiwa njiani ndipo muujiza wa uponyaji ulitimia. Viungo vyao vikarejea
sawasawa.
Luka 17:12-19
Sitaki nielezee saana mtu mwenye ukoma yukoje..nataka tujifunze thamani
ya kushukuru. Watu 10 waliponywa ukoma lakini ni mmoja pekee ndiye
alikumbuka kurudi kushukuru..! Kitu ambacho kilimshangaza sana Yesu,
(..hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi?)
Unaweza kudhani pengine wamesahau maumivu na athali za ugonjwa wa ukoma.
Wapendwa, naomba tujifunze kitu kutoka kwa yule mmoja (msamalia)
aliyekumbuka kurudi kushukuru. Kushukuru ni kutambua thamani ya fadhira
ulizotendewa..kushukuru ni kumpa moyo yule aliyekusaidia, kushukuru ni
kuonyesha utu. Kushukuru ni kutambua msaada uliofanyiwa.
Kumbuka kuwashukuru waliokusaidia ulipoumwa, ulipotingwa na jambo
fulani. Kumbuka kuwashukuru waliokulipia ada yako ya masomo hadi
ukamaliza masomo yako.
Kunawatu wamekuwezesha kwenye biashara yako hadi ikasitawi, acha dharau, usiwasahau
ukadhani ni kwa juhudi zako, kumbuka kuwashukuru waliokusapoti hadi
biashara yako ikasitawi.
Hata kwenye familia hatulingani, yupo aliyebeba familia, anajitoa kwa
hali na mali..mtieni moyo na kumshukuru.
Ipo nguvu kwenye kushukuru, tujifunze kushukuru kwa kila jambo.
No comments:
Post a Comment