Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Wakolosai 3:21.
Wakolosai 3:21.
Changamoto nyingi za watoto zinatokana na wazazi/walezi wengi kuwachokoza watoto wao. Mtoto anahitaji malezi mema, huduma zote za msingi kama mavazi, chakula, malazi bora n.k. Mtoto anatakiwa kufundishwa maisha na kuishi vizuri na watu wengine.
Makosa yanayofanywa na wazazi na walezi wengi, kumtukana mtoto pindi akikosea..hii inatafsiliwa ni sawa na kuchokoza mtoto. Mtoto anapaswa kuonywa na kukemewa pindi akikosea na siyo kutukanwa.
Unavyomwambia mtoto wako mbwa wewe, kichwa chako kinafanana na ng'ombe, muone kwanza unatembea kama gari bovu, bongo lala, mlafi wewe n.k. Hayo ni maneno ya laana yanayotamkwa na wazazi wengi..unaweza kujiuliza ikiwa mtoto ni mbwa maanayake mzazi ndiye mbwa mkubwa, kitendo cha kumfananisha mtoto wako na vitu visivyo na uhai na kumfananisha na wanyama na vinyago, ni kumchokoza mtoto na kuharibu tabia yake, ni kupandikiza tabia mbaya kwa mtoto wako.
Wazazi na walezi wengine wameshindwa kuwalea na kuwalinda watoto wao, wengine wanawafanyia watoto vitendo vya ukatili, vitendo viovu na adhabu zisizo za kibinadamu. Mtoto wako akikata tamaa ni hatari sana.
Tabia mbaya huaribu ubongo wa mtoto, wazazi/walezi msiwalawiti, kubaka, kuwaonyesha picha chafu watoto wenu. Mtoto anapaswa kulindwa, kupendwa na kuthaminiwa.
Msaidie mtoto wako muelekeze njia bora ya kufanya kazi, kuwa mwalimu mzuri nyumbani. Mfundishe mtoto wako kufanya usafi wa mazingira, kusafisha nyumba, mavazi yake na usafi wa mwili wake. Mfanye mtoto wako kama rafiki yako wa karibu.
Yale unayomtendea mtoto wako ndo huwa tabia yake ukubwani.
Mungu akubariki unapotafakari somo hili.
Usimchokoze mtoto wako..!!
TAVE'S BLOG
TAVE'S BLOG
1 comment:
Yes
Post a Comment