Somo la 3.
FREEMASONS NA IBADA YA SANAMU INAYOKUJA
NIREJEE
historia ya Socrates, Yule mwanafalsafa wa Ugiriki. Ndiye mwalimu wa Plato;
Plato ndiye mwalimu wa Aristotle.
Encyclopedia
Britannica, hutuambia kwamba, Aristotle (384-322 BC)ndiye mwanasayansi wa
ukweli katika historia ya ulimwengu.Hawa wanafalsafa wengine,wamufuatisha kile
alichofikiri yeye kwanza.
Socrates,
aliuliwa na mamlaka ya Athens,kwa kuwa aliwafundisha wanafunzi wake,akina
Plato, kwamba hakukuwa na miungu 391 juu ya kilele cha Mlima Olympus.
Alifundisha kwamba, kulikuwa na Mungu mmoja tu,naye aliishi mbinguni.
Kwamba,
magalaksi(galaxies) yoote aliyaumba yeye pamoja na nyota na sayari zote
ulimwenguni, na kwamba dunia haikutokea kwa bahati kwa njia uibukaji(evolution)
kama alivyofundisha Charles Robert Darwin katika karne ya 19.
Sokrati huyu,
alipewa alipewa rehema ya juma moja, ili ayakane mafundisho yake ya kuidharau
miungu ya taifa lake la Ugiriki; alikataa na mwisho wa siku alihukumiwa hukumu
ya kifo.
Alipewa sumu
ainywe mbele ya hao wanafunzi wake akina Plato, akianywa sumu hiyo,mwili
ulipopatwa ganzi akalala na kufunikwa shuka akiwa tayari amekufa-waliahidi
kumlipa posho ya chakula kila siku kama angeyakana mafundisho yake hayo.
Nataka kusema
kwamba, Sokrati alishikilia msimamo,mwisho akauawa mbele ya wanafunzi wake.
Naam, ukweli huandamana na hukumu ya mauti.
Msomaji,utambue
kuwa ibada ya miungu katika ulimwengu ule lilikuwa suala la maisha au la mauti
duniani,tangu Ulaya hiyo ya akuna Sokrati,Plato na Aristotle na ndivyo
itakavyokuwa tuendako.
Hao wazungu
wa Magharibi,hawakuwahi kuijua dini. Walikuwa washenzi na watambikia mizimu na
waabudu sanamu.
Unajua watu
wa kwanza kumwabudu Mungu mmoja ni Waisraeli wa kale? Unajua dini ya Ukristo
imekuja wakati wa Yesu na mitume?
Mitume kama
Petro, Paulo n.k ndiyo waliopeleka Ukristo Ulaya,hususan jijini Rome, na wakaishia
kukataliwa na kuuliwa kinyama?
Hata Afrika
ilitangulia kumjua Mungu kuliko hawa; tazama historia ya nchi kama Ethiopia,
Sudan, Misri n.k
Edward A.
McDowell, Profesa wa Agano Jipya katika Seminari ya Baptisti,Nort
Carilina,Marekani, ameandika katika kitabu kiitwacho The Meaning and Message of
Revalation,kwamba watawala wa Romi ya kale(emperors) walilazimisha raia
wawaabudu, ambao walijiona ndiyo miungu!
Rumi ya kale
kulikuwa na dini ya kuwaabudu wafalme waha wa Rumi. Julius Caesar, alitengeneza
SANAMU lake lililowekwa miongoni mwa masanamu mengine hekaluni mwake-hekalu la
Kaisari!
Kaisari
Augusto(27 BC-14 AD) alikubali cheo kiitwacho, “Augustus” kutoka katika Baraza
la seneti. Hiki ni cheo cha miungu.
Caius
Caligula( AD 37-41) aliwalazimisha raia wa milki hiyo ya Rumi dunia nzima
waiabudu sanamu yake. Jitihada zake za kuisimika sanamu hiyo katika hekalu la
mjini Jerusalemu zikapingwa vikali sana na Wayahudi; kwa kuwa wao walijua ibada
ni kwa Mungu tu ambaye huishi mbinguni,na hawakilishwi na masanamu!
Domitian,
alikuja kupunguza mgogoro mkubwa kati ya Wakristo na makaisari wa Kirumi
waliotaka kuabudiwa na watu wote,na wale waliopingwa, waliuawa kwa kuraruliwa
na wanyama katika viwanja ambavyo siyo tofauti sana na stadium za sasa hivi.
Kaisari Nero
alitaka raia wa makaloni yote chini ya dola hii wawaone wao kama miungu.
Hatimaye masanamu yaliingizwa kanisani,wakati Wakristo wakitaka kujikomba kwa
hawa makaisari walioanza kujifanya wameongoka na kuwa wakristo.
Aina hii ya
madhehebu ya ibada ya wafalme ni maarufu hata Asia; na ilidhaniwa kumwabudu
Mfalme ndiyo ‘Patriotism’ yaani uzalendo kwa taifa lako.
Dola ya
Waislam wa Ottoman(Uturuki) ambayo sasa imejisalimisha NATO, walijaribu kuzuia
uhalifu huu, lakini kama tulivyoona katika makala zilizotangulia, dola hii ya
Ottoman ilianguka katika karne ya 16 AD.
Kwa hiyo,
zama za Ukristo,watu waliokataa kuwasujudia ma-emperor wa Rumi walionekana
waasi, watukutu na wasio wazalendo-waliuliwa,kufungwa jela na wengine
walifukuzwa wakawa wakimbizi huko uhamishoni,wengine ndiyo waliokimbilia
Marekani wakiogopa mateso Ulaya.
Wakristo,
walilazimishwa kuwaabudu makaisari,kuwatolea sadaka katika sanamu zao huku
wakitamka maneno haya, “Kyrios Kaisar” maana yake, “Bwana Mungu wangu
Kaisari”!!
Lilikuwa
zoezi dogo tu; lakini lenye kukudai uaminifu wako wewe
mkristo,Muislam,Budha,Hindu n.k kwa Kaisari badala ya Yule Mungu wako
unayemwabudu wewe kwa kicho na kutetemeka.
Wakazi wa
Afrika Mashariki wanajua mambo haya ya “Kasinge Mwombeki” kumbe yalianzia
Ulaya. Kiongozi wa kidunia alikuwa nawinda heshima ya kimungu,ili mwanadamu
apate kumwabudu yeye.
Nimeleta kisa
hiki ili tujue maana hasa ya kukufuru. Mwanadamu anapojiita Mungu,ndiyo
kukufuru,anapowalazimisha wanadamu wenzake kumwabudu yeye badala ya Mungu wa
mbinguni-ndiyo kukufuru.
Msomaji mmoja
anataka kujua,namna mamlaka(Mnyama) ya Danieli 7:23-25 na Ufunuo 13:1,4-8 na
pia Ufunuo 17:3-11 itakavyojigeuza kutoka mamlaka ya siasa na kuwalazimisha
watu wa dunia nzima kuiabudu,kama alivyoabudiwa Kaisari wa Rumi na SANAMU
yake,sawa sawa na Wakristo ama Waislam wanavyomwabudu Mungu.
Mamlaka
itakayofuata duniani baada ya Marekani na washirika wake kuitiisha dunia
nzima,itatengeneza sanamu(Ufunuo 13:14-15).
Sanamu hii
itadai kila raia wa dunia nzima(sensa ya dunia nzima ipo,na kila raia wa dunia
anajulikana) kutoa heshima yake kwa Mtawala huyu mpya wa dunia, ambaye atarithi
enzi zote za tawala za Kaisari. Watu watadaiwa kuonesha kifo kwa huyu mtawala
ili kuonesha uzalendo wao kwa kutamka maneno, “Kyrios Kaisar” yaani Bwana Mungu
Kaisari badala ya kutamka,”Kurios lesous” yaani Bwana Yesu ama kwa Waislam,
‘Allah Akbar”!!
Ugomvi wa
sasa wa Marekani,Ulaya, Israeli na washirika wao wengine, ni kitu gani kama
siyo kutaka dunia iwe na mtawala mmoja, na taifa la Kiislam kama Iran linagoma?
Hivi leo,kuna
vitu vya kijesi(Military Base) nyingi za Marekani huko Ghuba ya Uajemi. Na vita
vikianza, tayari Iran iko kati kati-mataifa mengi ya Kiarabu kama Kuwait,Qatar,
UAE wameruhusu vituo hivi vya kijeshi vya Marekani,ili Waislam wenzao wakileta
jeuri,wananyeshewa mvua kali ya mabomu na risasi za rashasha(automatic rifles).
Huu ndiyo
ulikuwa ugomvi wa Wakristo na Makaisari wa Rumi zama zile.Wakristo wengi
waliteswa Ulaya kwa kugoma kumsujudia Kaisari na sanamu zake,na ndivyo
itakavyokuwa,kwamba tunakwenda kulazimishwa kuiabudu sanamu ya Kaisari
mamboleo, ambaye ndiye Marekani na washirika wake wanamwandalia barabara
kuelekea ‘Zulia Jekundu’.
Kati ya Mungu
na Kaisari wa Rumi,kulikuwa na ugomvi,mmoja akidai kuabudiwa na mwanadamu. Kuna
nguvu mbili duniani zinashindana kutaka kuabudiwa,na kutolewa sadaka, lazima
mmoja apewe heshima na kicho. Ukikataa kuiabudu mamlaka,unauawa.
Juma
lililopita,nikamwona Waziri Mkuu wa Israeli, Benyamin Netanyahu,akimwambia Rais
Obama wa Marekani huko White House:
“Iran
wanatuita sisi Shetani mdogo; na ninyi Marekani wanawaita Shetani mkubwa! Kwa
nini wasishambuliwe na vinu vyao vya Nyuklia kuharibiwa,kabla hawajaanza
kutushambulia sisi?” Alisema Netanyahu.
Iran wanaiita
Israeli na Marekani kuwa Shetani. Tabia ya Shetani ni kujiinua mahali alipo
Mungu na kudai kuabudiwa-na tabia hii imeonekana wazi katika siasa za dunia.
Marekani ni Baba wa dunia, Israeli wanafanya wapendavyo, hawaguswi.
Ujinga ni
watu kudhani Israeli ni taifa teule la watu wa Mungu-tuwasaidie, Israeli
walikoma kuwa taifa teule la watu wa Mungu walipomuua Yesu,Mitume na Manabii na
mashahidi kama Stephano,wakasema damu zao ziwe juu ya vichwa vyao na vichwa vya
watoto wao.
Unajua
Yerusalem ulibomolewa na majeshi ya Kirumi mwaka 70 AD? Unajua W aisraeli wamekuwa wakimbizi katika nchi
yao, Waarabu wakaikalia hadi huo mwaka 1948 waliporejeshwa kwa msaada wa Umoja
wa Mataifa? Marcus Mpangala ameandika jambo hili kwa kina.
Taifa la
Israeli lilisha mwasi Mungu; leo wamekaribia kumalizwa na Adolf Hitler, damu ya
manabii iko juu ya vichwa vyao, isipokuwa Muisraeli mmoja mmoja akitubu kwa
kiburi chao hiki na ukatili dhidi ya mitume na manabii wa Mungu.
Ni kwa sababu
hii, Israeli,Ulaya,Marekani na Vatican wamekubaliana kutengeneza mfumo mmoja wa
dini,ili “Kaisari” mmoja miongoni mwao aabudiwe na dunia nzima.
Huku sasa ni
kuondoa UHURU WA DINI,Demokrasia na haki za binadamu. Siku hizi haki za
binadamu ni ushoga, usagaji na wanawake kutaka kuoa wanaume zaidi ya mmoja!
Waliosikia siku ya wanawake duniani wanajua tuendako.
Haki za
Binadamu!! Haki hizi zinaletwa na miungu ya Ulaya na Freemasons na Illuminati.
Mwandishi
mashuhuri hapa nchini, William Shao, amepata kuandika katika jarida la Rai juu
ya sanamu ya mwanamke aliyeketi juu ya mnyama huko Makao Makuu ya Umoja wa
Ulaya(EU) mjini Brussels.
Shao,
aliandika kwamba sanamu hiyo inayofanana sana na kile kinachosemwa katika
Ufunuo 17:3-11 iko mbele ya Ofisi za European Union huko Brussels, Ubelgiji.
Nimewahi kuongea na Shao siku za karibuni juu ya kitabu chake kuhusu
Freemasons.
Sasa,kama tunabahatisha,kama
wengine wanavyodhani, ni suala la kila mmoja kutafiti na kuamua. Tunawaandikia
wenye hekima; hatuna shida na wapumbavu!
Mwanamke
aliye sawa na huyu wa mjini Brussels, ni Yule aliyemwona Mtume Yohana katika
Ufunuo 17:3-11. Anaitwa jina la siri, “Yezebeli”.
Naam, nataka
tumjadili Yezebeli. Yezebeli anabebwa na Umoja wa Ulaya(EU) na washirika
waao,Israeli na Marekani.
Yezebeli huyu
alikuwa muumini wa kanisani Thiatira(Ufunuo 2:20-24) na alijiita
Nabii,alifundisha waumini watu wa Mungu ili kuwapoteza,ili wazini(kuabudu
miungu) na kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na masanamu ya makaisari
wa Rumi.
Naam,
Yezebeli hataki kutubu,ni mzinzi,nusu yuko kwa Mungu,nusu ibada ya
sanamu.Uzinzi wa kiroho ni watu wa Mungu kutambikia mizimu na miungu na
kusujudia sanamu(Hesabu 25:1-3).Yezebeli anatufundisha sasa kutambikia miungu
ya Misri, Babeli,Uyunani na Rumi,na somo hili tumejifunza katika makala
tulizotangulia kuona.
Yezebeli,
anavaa nguo za rangi ya zambarau na nyekundu(Ufunuo 17:4).Mwandishi Gidion M.
juzi aliandika kwamba nguo hizi za rangi ya zambarau na nyekundu walivaa
wafalme wa Babeli na makuhani wa miungu.
Labda, ndiyo
maana mama huyu ana jina linguine la siri-‘BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA’!!
Huyu Yezebeli
anayebebwa na wafalme hukoo Umoja wa Ulaya(EU) anao watoto ambao pia ni
makahaba.Watoto wa changudoa nao huwa changudoa kwa sababu ya mivuto mibaya.
Sasa mama huyu ni nani? Amewazaa akina nani? Tafakarini.
Yezebeli,
alikuwa Malkia aliyejifanya mlinzi na Mfadhili wa manabii wa Baali na Ashtorethi
zama za Nabii Eliya(1Wafalme18:19).Ashtorethi alikuwa mungu mkuu mke wa
Wafoeniki na Baali alikuwa mungu mkuu mume.
Nani mungu
mkuu mke-Ashtoreth? Gidion M. AREJEE SOMO HILI, ili wasomaji waelewe.
Tunajifunza,Yezebeli alikuwa adui mkuu wa Eliya,Nabii wa Mungu, na alitaka
kumuua Eliya. Hapa Yezebeli anafananishwa na mtu ama kikundi cha watu wanaotaka
kuwaua watu kwa sababu wamekataa kuabudu Baal na Ashtoreth. Kwani kuabudu dini
ni lazima?Hata Mungu halazimishi.
Yezebeli wa
kanisani(Thiatira) anawaongoza waumini ‘kuzini’ yaani kula vitu vilivyotolewa
dhabihu kwa masanamu(Ufunuo 2:20).
Yezebeli
alikuwa mke wa Mfalme Ahabu,aliyehamasisha Waisraeli wa kale kumwacha
Mungu(hata sasa wamemwacha Mungu) na kuabudu Baali na Ashtoreth,kitu hiki
huitwa uzinzi. Waisraeli wa sasa wanamwabudu Baali,mungu mume wa Ufoeniki na
mungu mke ndiye Ashtoreth, na mataifa mengi watalazimishwa kumwabudu huyu,na
wanamwabudu Ashtoreth hata katika siku kuu zijazo za Pasaka, Krismasi,MWAKA
Mpya n.k
Wapendwa
wakristo,someni 1Wakorintho sura 8 MTAONA jambo hilo lililoanza kutokea AD 95.
Uzinzi ni kumwabudu Kaisari,ni ibada ya sanamu, ibada ya sanamu ni kinyume na
AMRI 10 ZA MUNGU,ni kinyume cha amri ya Pili(Kutoka 20:4-6).
Tuijadili
kidogo miungu hii.
Zeus,
mwaka 29 BC
hekalu lilijengwa na Kaisari Augusto,LIKAWEKWA WAKFU kwa ajili ya Kaisari huko
Pergamo,na mjini Rome sanamu hilo liliwekwa makau makuu ya Sinodi ya Kanisa.
Tumeona
maofisa wa serikali ya Rumi wakilazimisha watu kumwabudu Kaisari has huko
Pergamo. Huyu Zeus(Jupiter) sanamu lake lipo Olympia na ni moja ya MAAJABU SABA
YA DUNIA.
Huyu Zeus ni
mfalme wa miungu na anaketi katika kiti cha enzi.Sanamu hili limejengwa mwaka
457 BC na linaabudiwa dunia nzima kwa njia anuwai.
Utaona sasa
Yezebeli wa leo akiwa amebebwa na Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels,Ubelgiji,
tunalazimishwa kumwabudu na kumtolea dhabihu. Yohana anasema Wafalme wa dunia
wamezini naye na wafanyabiashara wamepata mali kwa nguvu ya kiburi chake(Ufunuo
18:1-3).
Unataka
utajiri? Yezebeli ni jibu lako,utauza maua wakati wa siku kuu zake, utauza
pombe kuliko wakati wowote, utauza miti ya Krisimasi n.k
Nimegusa jiji
la Rome lililojengwa miaka 2765 iliyopita, watawala wake maarufu sana ni Julius
Caesar, Augusto, Tiberio, Gaius,Claudio,Nero,Galba, Vespasianus,Titus orodha ni
ndefu.Hawa walitengeneza masanamu yao ili yaabudiwe. Hata masanamu ya Nyerere
yapo mengi-hatujaambiwa kuyasujudia.
Freemasons ni
hatari. Ugiriki imeathiri dunia nzima kwa maarifa yake,tamaduni zake, miungu
yake na ustaarabu wake. Demokrasia imeanzia Ugiriki,lakini leo ni nchi
masikini, wanapewa msaada na Eurozone!
Mataifa ya kiarabu yanazimwa
yasiwe Super power. Afrika utajiri wake ullikwenda wapi? Niliwahi
kuhoji,kwanini Ashanti
isiendelee kuwa dola ya Ghana
ya Mwafrika, eti siku hizi ni kampuni ya Mzungu ya kuchimba dhahabu hata hapa Tanzania?
Unaweza
kusema sisi ni mafala! Lakini, Babeli ama Iraki,Misri, Wamedi na Waperizi na
Wagiriki wako wapi?
Nani alianza
kuandika? Nani alianzisha hesabu? Viwanda vya kufua chuma havikuwa Afrika?
Zbigniew
Brzezinski,mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani enzi za Jimmy Carter
alisimamia Mradi wa kutengeneza Virsi vya Ukimwi huko kilomita 75 kutoka
Washington miaka ya 70.Lengo lilikuwa kupunguza watu duniani kwa sababu
rasimali zinazidi kuwa chache.
Ukimwi ni
silaha ya kupunguza idadi ya watu,chakula ni kidogo, watu wengi,makazi yanazidi
Wazungu wamekwenda hata mwezini,Mars ili kutafuta nishati.
Sasa,lazima
kuwepo na mkakati wa siri kuwapunguza,wanaobaki ni wale watakaosujudu miungu
yao-hawa ni mawakala wa shetani. Tutafanyeje? Mtafuteni Mungu wa
kweli.
MWISHO.
2 comments:
Inatisha kama si Yesu kutuokoa itakuwaje?
Erisha - Musoma.
Sasa kama hali ni hivyo tutaokolewa kweli? ama wote tutapotea!!!
Ashery Nipo Arusha.
Post a Comment