Friday, May 4, 2012

UTAWALA WA FREEMASONS KATIKA BIBLIA TAKATIFU


Somo 1

UTAWALA WA FREEMASONS KATIKA BIBLIA TAKATIFU

ALFAJIRI, kuamkia Jumamosi, Desemba 30. mwaka 2006,mtawala wa nchi uliko Mto mkubwa, Frati,Saddam Hussein, akanyongwa kwa kamba hadi kufa.
Mahali walipomnyonga, panaitwa Camp Justice; walimnyonga kwa makosa ya ubinadamu,huko Kaskazini mwa Baghdad.
Saddam alinyongwa mbele ya Wairak wachache, na dunia ilishuhudia tukio hilo katika televisheni; akina Mouwafik al-Rubaie,Mshauri wa Usalama wa Irak, alikuwepo Camp Justice.
Nataka msomaji atambue jambo muhimu na la msingi sana. Kwamba, Marekani kuivamia Irak na kumpindua Saddam Hussein mwaka 2003, wakang’oa sanamu yake jijini Baghdad, ilikuwa kutimiza unabii muhimu sana.
Sababu zote walizosema juu yake kwamba alikuwa na silaha za kuangamiza,ulikuwa umbeya mtupu- mengi wanayosema Marekani dhidi ya viongozi wanaohitilafiana nao ni uongo tu; utaona hapa chini.
Ilikuwa kuashiria kuanguka kwa Dola lenye nguvu huko Mashariki, na kando ya mito miwili ya Tigris na Euphrates.Lilikuwa jambo muhimu katika historia ya dunia.
Kunyongwa kwa Saddam mbele ya kamera za televisheni,ilikuwa kuwaambia magamngwe wachache wasiotii mamlaka za Magharibi,kwamba dawa yao ni kitanzi,risasi na kifo!
Siku ya mauti yake,Saddam alikabidhi kitabu chake cha Koran alichokumbatia kifuani, akasali, wakamsomea sababu za kifo chake kwamba aliwaua Washia 148 huko Dujail mwaka 1982; akakubali kusalimu amri na kufa kistaarabu!
Ndivyo zilivyokoma enzi za Saddam ambazo wao waliziita, The Dark Period.
Gaddafi naye ameuliwa baada ya kusalim amri,akapigwa risasi huku akiomba msamaha,utadhani aliwakosea hao wauaji peke yao!
Feburuari mwaka jana, ikatangazwa kwamba Osama bin Laden ameuliwa huko Pakistan,juzi tukaona kwenye televisheni nyumba aliyoishi ikabomolewa na matingatinga,ili mahujaji wasifululize kwenda kuhiji mahali hapo!
Naam. Juzi tukatazama katika televisheni,ya kwamba eti mwaka 1988 huko Lockerbie, Scotland, siyo maofisa Usalama wa Libya, akina Megrahi waliolipua ile ndege ya Marekani ya Pan American Airways!
Nilimwona Al-Megrahi katika kitanda cha mauti anapougulia maumivu ya Saratani baada ya kuachiwa huru akisema, alifungwa kwa uonevu tu-Hao ndiyo Marekani Bwana!
Hata Syria watashinda,maana imeandikwa Marekani na washirika wake wataushinda Ulimwengu,kwa kuwa husaidiwa na Freemasons, Illuminanti na Ibilisi mwenyewe,Mfalme wa Dunia hii.
Dola la Kisovieti(USSR) lilishashindwa kusimama kijeshi kama dola kuu la dunia, akina Mikail Gorbachev walishajikabidhi Washington kitambo-Urusi imebaki kwa akina Putin watu dhaifu.
Nataka nikwambie msomaji. Dikteta wa zamani wa Yugoslavia,Slobodan Milosevic aliondoka kitini mwa enzi kwa ‘Nguvu ya Umma’ mwaka 2000, akamwachia kiti Vojislav Costunica huko Serbia ya sasa.
Marekani na washirika wake walimpeleka Milosevic huko Hague kujibu mashitaka ya uhalifu wa vita na haki za binadamu.
Amini usiamini,ndani ya kampeni kali ya Haki za Binadamu, Ibilisi anaongoza harakati dunia nzima=haki za mashoga, haki za akina mama hata kuwachapa makonde akina baba, kampeni za kunyimana unyumba, n.k
Watawala wa nchi za ‘Mrengo wa Kushoto waliopinduliwa na Marekani,ni wengi sana akina Noriega huko Amerika Kusini.
Korea Kaskazini,haitashambuliwa tena kijeshi. Bada ya kifo cha Kim Jong Il, akaingia mtoto,”Chekechea” Kim Jong Un katika siasa za Ulimwengu, bila shaka Korea itaacha kutengeneza Nyuklia kwa kupewa mafuta na fedha taslim,na itaachana na kuabudu miungu yao na kujiunga na ‘Dini Maalum’ basi,hakutakuwa na maneno tena.
Tatizo ni Iran. Juma lililopita,tuliona kitisho cha vita huko Iran ikizidi kuishupalia Israeli na kukomaza shingo yake kukabiliana na Marekani na Washirika wa Magharibi.
Tumejifunza katika makala zilizotangulia kwamba Marekani na washirika wake na Israeli, Vatican wanaandaa mfumo mpya wa utawala na ibada(Soma Ufunuo wa Yohana 17:1-17).
Mataifa yenye nguvu duniani, yatakuwa yanabeba mgongoni mwake madhehebu Fulani ya kidini,ambayo kila mtu analazimika kuyakubali mafundisho yao na falsafa yao ya kumpinga Mungu muumbaji.
Turejee katika unabii wa Ufunuo wa Yohana 13:1-10.Kuna wasomaji wananiuliza Dini itabadilikaje na kuwa mamlaka ya siasa?
Ufalme wa mwisho duniani, baada ya Marekani kuitiisha dunia nzima kwa kushirikiana na iliyokuwa dola ya Rumi, ni ule unaomkufuru Mungu. Kumkufuru Mungu ni binadamu kujiita Mungu; ni mamlaka ya ibada,kuabudu dini Fulani na mtu Fulani anayesema yeye siyo mwakilishi wa MUNGU tu,bali ni Mungu.
Shetani mwenyewe ataipa dini hii mamlaka yake(Ufunuo13:2).Freemasons,Illuminanti wataipa nguvu Marekani na washirika wake,Ulaya na Israeli, watampa mfalme wa kidini mamlaka yao yote na viti vyao vya enzi na uwezo mwingi na dunia itashangaa kwa mamalaka na uwezo wake.
Katika Unabii wa Biblia,mnyama ni ufalme,mamlaka Fulani na siyo mtu binafsi.(Danieli 7:17),mnyama huyu anayezungumzwa na manabii Yohana na Danieli atainuka Ulaya,mahali palipokaliwa na watu wengi tangu zama za Yohana mwaka 96 AD.
Marekani na washirika wake, wakipewa nguvu na nguvu za giza za Ibilisi, Freemasons,Illuminanti n.k watampa mamlaka yao mfalme ajaye, baada ya Marekani kuitiisha dunia na kuondoa demokrasia kwa Sheria –NEW World Order (Ufunuo 13:13).
Ajenda ya hawa wote ni kumpinga Mungu muumbaji wa dunia. Tabia ya ufalme huu ujao duniani imezungumzwa vizuri kabisa.
Ufalme huu wa Ufunuo 13:2 UNASEMWA kwamba ulikuwa mfano wa CHUI, huyu chui alikuwa na miguu ya DUBU, kichwa chake kilikuwa cha SIMBA na aliwabeba madikteta 10 ambazo ni mihimili 10 za mataifa ya Ulaya leo, katika eneo lile la dola ya Rumi ya kale.
Turejee katika ndoto ya Mfalme Dikteta Nebuchadnezzar, zama za Nabii Danieli katika sura ya Pili na Saba ya kitabu cha Danieli. Kuna historia ya dunia,zamani hata siku hizi. Nabuchadnezzar alioneshwa njozi kwamba baada yake kungekuja falme nyingine nyingi.
Kwa mhtasari, sura ya saba ya kitabu cha Danieli,tunaambiwa kwamba mnyama SIMBA ni ufalme wa Babeli(603-538 BC).
Ufalme huu wa Babeli (siku hizi Irak) ulipinduliwa Oktoba 13,mwaka 539 na Cyrus The Great, unaweza kusema Koreshi.
Ufalme wa Pili baada ya Nebuchadnezzar,ulikuwa UMEDI na UAJEMI waliunda serikali ya mseto, na wanafananishwa na DUBU aliyejiinua upande mmoja wa mshirika wa utawala huu wa mseto.Wakawashinda wafalme watatu ndizo mbavu tatu mdomoni mwa dubu huyu mkali, ulianza kutawala 538 hadi 331 BC.
Ufalme unaofananishwa na CHUI ni Ugiriki ya sasa iliyoitwa Uyunani. Siku hizi Ugiriki ni dhaifu inayochangiwa fedha na ukanda wa Euro zone, ili wasifilisike. Ugiriki ilianza kutawala dunia mwaka 331 wakati wa Alexanda Mkuu, wakaja kupinduliwa na Rumi Oktoba 13,mwaka 168 BC.
Dola ya Rumi inafananishwa na MNYAMA wa ajabu!! Alikula na kuponda kwa mkono wa chuma, na ulianza kutawala dunia Januari 22 mwaka 168 BC hadi kupinduliwa na kugawanyika katika falme ndogo 10 za Ulaya leo, na nitazitaja. Ulikuwa mwaka 476 AD. Dola hii ilitawala kwa karne zaidi ya sita. Soma pia Danieli 2:41.
Baada ya hapa,tumeona akina Napoleon Bonaparte ,Julius Caesar, Adolf Hitler na wenzao wakijaribu kuiunganisha Ulaya,na dunia nzima wakashindwa vibaya.Tumeona vita vya dunia juma lililopita.
Sasa, tutazame tabia za falme hizi nne za Nabii Danieli ambazo yule Mfalme wa Ufunuo 13:1-10 ana nasaba nazo.
Mfalme wa Ufunuo 13 ana fanana na CHUI, ana tabia ya ufalme wa Ugiriki ama Uyunani.
Tunawajua Wagiriki, sifa yao ni FALSAFA.Wale “Great Thinkers” wametokea Ugiriki. Socrates, Plato, Aristotle(384-322, BC) hawa wametuachia maarifa ya sayansi. Masomo kama Biology, Chemistry, Geology, Zoology, Physics, Psychology, Astronomy n.k yametoka kwao.
Kwa hiyo, Mfalme huyu wa Ufunuo 13:1-10 ana vaa ‘ngozi’ tabia za CHUI-Ugiriki, sayansi,usomi,falsafa,ujanja ujanja.
Wagiriki, wanajulikana kwa academy zao na ibada ya masanamu. Eti kulikuwa na miungu 391 iliyoishi katika kilele cha Mlima Olympus. Socrates akaipinga hiyo miungu,akasema kulikuwa na Mungu mmoja Mbinguni, wakampa sumu ainywe baada ya kukataa kutubu. Socrates alikufa kwa kuipinga miungu ya mlima Olympus!
Yako mengi Ugiriki, michezo ya Olimpiki hiyo itakayochezwa London Juni mwaka huu,na mbio za Marathon. Siku nyingine nitaandika juu ya hili,leo niliache.

Mfalme ajaye atakuwa na mwenendo kama Ugiriki, ataleta maarifa na falsafa na ibada ya miungu nitakayotaja kitambo.
Atakuwa na miguu(mwendo) kama wa UMEDI na UAJEMI, serikali ya mseto iliyoanzisha duniani SHERIA.Sheria za kwanza zimetungwa na Wamedi na Wajemi na hazikubadilika(Danieli 6:15,17)na pia ibada ya sanamu iliyomtupa Danieli katika tundu la samba wakali wenye njaa.
Mfalme huyu atakuwa na kinywa kama na kinywa kama SIMBA, atanena kama BABELI, kutengeneza masanamu na kulazimisha kila mtu kuyasujudia. Masanamu ni kinyume cha Amri ya Pili ya Mungu.
Danieli 3 na 6 KUNA HADITHI ya Ibada ya masanamu.
Mfalme wa Ufunuo 13:1-10 atakuwa na tabia za Rumi ya kale. Tuujadili kidogo ufalme wa Rumi.
Ibada ya sanamu na miungu iliyorithiwa kutoka Babeli,Umedi, Misri,Ugiriki n.k. Baadhi ya miungu ya Rumi, Aphrodite ambaye ni VENUS.
Mfumo wa sayari,nyota na mwezi viliabudiwa na Warumi. Mars ndiye Ares kwa Wagiriki, Artemy ndiye Diana, chimbuko la kumwabudu Bikra Maria siku hizi. Athena, Saturn,Pluto,Mercury,Uranus,Zeus ndiye Jupiter kiongozi wa miungu-orodha ni ndefu.
Kila mungu alipewa siku maalum ya ibada.
Saturday, ni kwa ajili ya mungu Saturn, Sunday ni siku ya mungu Jua yaani Sun’s day!
Ibada ya jua ni Mithras, Isis wa Misri,Demeter wa Ugiriki,orodha ya miungu ni ndefu.
Mfalme huyu wa Ufunuo 13:1-10 atapewa mamlaka na shetani, atapewa kiti chake cha enzi na uwezo mwingi, soma fungu la pili. Sasa, Urusi ama Iran watatawala wapi dunia?
Tumejifunza kuhusu ‘donda la mauti’kupona Feburuari 10 mwaka 1929 na kwamba utawala huu uliwahi kutiwa jeraha Feburuari 11 mwaka 1798 wakati wa maasi ya Wafaransa.
Dunia nzima itashangaa kuona mfalme ajaye anasujudiwa kama Mungu kwa lazima na hakuna demokrasia tena na uhuru wa dini-Religious Liberty.
Ufalme wa kidini utaongoza dunia na kutoa amri(sheria kali) wale wasiosujudu sanamu wauawe ufunuo 13:15,17. Sitafsiri unabii kama nipendavyo,tusome Danieli 7:17 hadi 24.
Mnyama huyu atamkufuru Mungu-kumkufuru Mungu ni mwnadamu kujiita Mungu Danieli 17:17,18 NI ‘Pembe Ndogo’ ya Danieli ambayo ni mamlaka hii ya ufunuo 13:1-10. Pembe yenye macho(Intelligence) na mdomo wa kumkufuru Mungu yaani utawala wa dini.
Mataifa ya Ulaya yanayosemwa kuwa ni vichwa saba yaani falme saba ni Anglo-Saxons(Uingereza),Alemanni(Ujerumani),Visigoths(Hispania),Franks
(Ufaransa),Lombards(Italia),Suevi(Ureno) na Heruli, Ostrogoths na Vandali, walipinduliwa na utawala wa 538 hadi 1798 AD, YAANI MIEZI 42, SIKU 1260, Wakati nyakati mbili na nusu wakati.
Usikose toleo lijalo uone AJENDA YA SIRI ya Ulaya,Marekani kuunda Dola la mseto wa dini na serikali duniani kwa ufadhili wa Freemasons,Illuminanti na Ibilisi.

No comments: