Monday, April 30, 2012

THE COMING WORLD CRISIS





Serikali moja itaanzishwa kwa awamu ikianza na marekani na ikifuata mfumo wa demokrasia chini ya umoja wa mataifa (tunashuhudia jinsi marekani ilivyoharibika, 2/3 ya bajeti ya umoja wa mataifa inalipwa na Marekani)
Dunia nzima itaingizwa kwenye mfumo huu wa serikali moja uliochini ya Occult- dini zote za kisenzi)
Vyovyote vile itakavyokuwa serikali moja itaundwa,mpinga kristo atafunuliwa na mwisho mfumo wa serikali  yake utaharibiwa na kurudi kwa Yesu mara ya pili. Kitu tusichokifahamu ni kuwa ni lini mambo haya yatatukia.

Kabla ya kuanzishwa kwa saerikali moja lazima kutakuwepo na sababu za kufanya hivyo .Watu wataelezwa kuwa ilituwe na amani dunia sharti tuwe na serikali moja kwani serikali zetu za nchi haziwezi kujilinda dhidi ya maadui.
Tumeshuhudia vita vikuu vya dunia vikipiganwa katika karine ya 20 na vita hivi vilihusisha dunia nzima na baada ya vita tunashuhudia mabadiliko  makubwa ikiwemo uanzishwaji wa umoja wa mataifa.
Leo hii umoja wa mataifa umekua ndio chanzo kituletacho karibu katika uanzishwaji wa serikali moja na unajumla ya wanachama zaidi ya 159

 Umoja wa mataifa umeanzisha miundo mbinu yake kutekeleza majukumu yake kama-:
Mahahama ya kimataifa
Umoja wa kutunza amani
Shirika la fedha duniani(IFM)
Shirika la afya duniani (WHO)
Shirika la watoto duniani (UNICEF)
Shirika la sayansi na teknolojia(UNESCO)
Haya yote yamekidhi kila idara ya maisha ya mwanadamu
Kitu kinachokosekana kwenye umoja huu ni nguvu ya kuanzisha na kusimamia mifumo walioiandaa katika nchi wanachama.
  
Je ni vita ya tatu itakayotufanya tukubali serikali moja? Kama ndio itaanzishwaje? Nani atakuwa kiini cha vita hii? Matokeo yake yatakuwa ni yapi?
Kujibu maswali haya tutaangalia matukio ya hivi karibuni na kuangalia kile ambacho biblia na roho ya unabii inatueleza.



Tunaami kuwa wahusika wataweza kuanzisha serikali moja pale ambapo watu watakupokuwa wamekubaliana kwa sauti moja
Wataweza kufanikiwa pale ambapo watahusisha serikali moja na matukio makuu yanayowapata wanadamu kama vile njaa, vita, madeni ,na kuhofu juu ya mazingira na hali ya hewa.
Tunasikia habari za vita mashariki ya kati ,vita ya silaha za nyukria, majanga ya kutisha katrina`,sunami ,
Pia hivi karibuni tumesikia vita ya kutisha dhidi ya ugaidi, kutafutwa kwa Osama Bin Laden, kunyongwa kwa Sadam Hussen matukio haya yote yameutikisa ulimwengu




Huu ni msemo wanaoutumia wahusika wa serikali moja.
Kila tatizo liwe dogo kiasi gani au kubwa m ara moja litakuwa ndio sababu ya kuhitaji serikali moja.lakini sababu kubwa itakuwa njaa, vita ,umasikini na kuzuia uharibifu wa mazingira.
Serikali moja itaonekana kama imeanzia chini ikionyesha kuwa kila kitu ambacho watu wote wa dunia wamekubaliana itakuja katika mfumo wa demokrasia, isiyodhohofu na mfumo ambao haukuletwa na wanasiasa, hivyo wakazo wa dunia wataamini kuwa wao ndio waanzilishi bila kujua kundi lililojificha nyuma yao( ndio maana leo katika siasa tunasikia nguvu ya umma)

Mpinga kristo atakaa juu ya umoja wa mataifa na wenye nguvu na hata kwenye mamlaka ya kidunia ilioanzishwa. Itaingia kwa haraka zaidi kwenye muundo wa uongozi chini ya misingi ya majimbo kumi.
Katiba ya duniaitabuniwa, bunge la kidemokrasia la dunia litaundwa na raia wa` dunia wataamini kuwawanayomaamuzi bila kugundua kwamba kuna nguvu za giza zilizojificha.
Ukuu wa nchi utakoma, mfumo wa kiuchumi duniani utaanzishwa na kila kitu kilichobaki katika mfumo wa zamani vitarithiwa kama lugha, utamaduni. Kila mamlaka halisi itakuwa chini ya utawala wa kimataifa unaongozwa na shetani  mwenyewe.








Lakini biblia inatueleza kuwa makini kuwa yamkini walio wengi ya wakazi wa dunia watadanganywa (Ufunuo 13, 2Thesalonike 2
Kanuni za serikali hii ya dunia tayari Zimeshaingizwa mpaka ndani ya makanisa na zimefanywa kana kwamba ndio mafundisho ya bibilia.
Mafundisho haya yatawafanya wengi wasimtambue kuwa ndiye mpinga kristo na kama angekuja akijitangaza kuwa yeye ni mtumishi wa shetani wapumbavu wachache ndio wangemfuata lakini atakuja kwa kutumia jina la Yesu na malaika wa nuru.



YESU AMETUONYA JUU YA KIPINDI HIkI
1YOHANA 2:18, MATHAYO 24: 24-25
Ukristo utawakilishwa na huyu mpinga kristo na hakika atajifananisha na kristo wa kweli ili kuwadanganya watu. Atakuwa amejaa mafundisho kuwa yeye ni Mungu wa kweli na atafundisha dini za mababu zetu.(umizimu)
Atakuwa na mafundisho ya kujitukuza mahali pa Mungu itakuwa dini ya watu wengi ikiwa na mafundisho ya ubinafsi 2wathesalonike 2:9-12
Mpinga kristo atakuja na nia ya kuleta amani ndipo wafuasi wake watakapo acha kuleta vita akiwasadikisha watu kuwa ni kweli.

  Ni kipindi cha kushikitisha kwani watu wengi watajitoa kumtumikia shetani asiye na sheria na mfano wake wakidhani kuwa ni Mungu. Atawafanya watu wajifikirie wenyewe akiwafundisha  kujinufaisha wenyewe na akiwafundisha kupokea nguvu ya asili
Ni kipindi hiki watu watakuwa chini ya mapepo kuliko kipindi chochote ambapo Mungu amewahi kutuonya, uovu utakuwa katika uweza wa miungu.
Biblia inatuonya juu ya tukio  hili ufunuo 12:12b
Ilikuhakikisha kuwa anaheshimiwa na kutukuzwa /kuabudiwa mpinga kristo atamlazomisha kila mmoja Ufunuo 13:13-16.

Alama hii itakuwa sawa na barcode system (Computerise) na kutumia computer scaner) na namba ya kuzalisha /kupaki  (universal production code) wale wote watakao kubali alama hii na Mungu atawachukulia wameamua kumwabudu shetani Ufunuo 14:9-11
Wale wote watakao kataa kupokea chapa ya mnyama watateswa Mathayo 24: 9-10
Wakristo waaminifu watakoishi kipindi hiki watachukuliwa kama waasi katika kuitafuta amani ya dunia, shida zote wao ndio chanzo . Ufunuo 13,14.

Familia zote ambazo zitakuwa huru na madeni watakuwa na mashamba yao kwa ajili ya kulima chakula na watakuwa na vipande kidogo vya chuma vitakuwa  ndivyo  vitu  vya kubadilishana ili kujipatia mahitaji yao na watakuwa wanajisikia vyema kuliko wengine pamoja kuna kipindi watajikuta katika hali ngumu ya maisha kwa kukataa kwao kupokea chapa ya mnyama. Na hawatakuwa na uwezo wa` kulipa kodi kwa sababu  malipo yote yatafanywa chini ya alama ya mnyama.
Unaweza kushangaa watu hawa watawezaje kuishi? Lakini Mungu aliyetuonya juu ya matukio haya atawapigania na kuwapatia tumaini.

Kwanza mateso haya ni yamuda kitambo . Daniel 13:5, Ufunuo 13:5
Wale wote watakao kuwa waaminifu kwa Mungu watapokea msaada toka kwa Mungu. Muda si mrefu walewaliopokea chapa ya mnyama watatambua makosa yao watakapoona serikali yao haitaki mapatano na wakristo wa kweli  ndipo watatambua kuwa mfumo huo sio wa Mungu wa mbinguni na ndipo watakapojaribu kuwasaidia wale wote walioteswa na serikali. Daniel 11:3
Ndipo wale watakao kaza kuelekeza macho yao na akili zao mbinguni watakaposhinda.
Ufunuo 7:14- 17
Ufunuo 14:13
Daniel 12:3-4
Biblia inatuambia kuwa muda wa mpinga kristo utakuwepo lakini kristo atakuja kuukomesha. 2thesalinike 2:1,3,8b
Yesu anatabiri kurudi kwakwe. Mathayo 24:29-31


 
 
 
 

No comments: