Somo la Pili
UTAWALA WA FREEMASONS KATIKA BIBLIA
TAKATIFU
JUZI, mashoga
na wasagaji wa Afrika ya Kusini, walifanya tamasha la kukata na shoka ili
kusherehekea haki zao; naam Haki za Binadamu !!
Wanawake kwa
wanawake na wanaume kwa wanaume waliooana Afrika ya Kusini, walikuwa wakisherehekea
kwa kupigana mabusu ya tashtiti, kulembua macho na kulegezeana macho
mabarabarani mchana kweupe!
Naam, wao
wanaita ilikuwa, ‘Gays Pride Festival’ na huu ndiyo uhuru ambao Marekani, Uingereza
na washirika wao wa Ulaya wanataka tubadili katiba zetu na kuufuata,la sivyo
hatupati msaada!
Afrika ya
Kusini,iliruhusu ndoa za mashoga mwaka 2006.
Kituko
kingine kinachodhihirisha uhai wa Freemasons na Ibilisi kuua watu kwa ajali za
ndege,meli,milipuko ya maghala ya silaha kama ya Mbagala na Congo-Brazaville,
ni kile cha yule ‘shushushu’ wa Libya, Basset Ali al-Meghri,kuhukumiwa kifo
Januari 31 mwaka 2001,kwamba alilipua ndege ya Pan American World Airways(Pan
Am), halafu juzi wakaja kusema alionewa!
Ilisemwa
kwamba, ile ndege ya Marekani Flight 103 ya Pan Am mwaka 1988 huko Lockerbie,
Scotland, haikulipuliwa na akina Basset al-Meghri, walisingiziwa tu.
Ulikuwa
uongo,bila shaka wa Marekani na ‘Mkono wake msaidizi’ Freemasons, kutungua
ndege ile na kuua mamia ya watu,kasha kutafuta ‘mbuzi wa kafara’ aitwaye kwa Kiingereza,
Scapegoat, ili kumtwisha dhambi ile, kwa lengo la kutaka kuishambulia
Libya,kwamba iliwatuma hao magaidi!
Ukitaka
kujikomba kwa Ulaya na Marekani, utawala wa Marehemu Saddam Hussein ulitaka
‘kufunika kombe mwanaharamu apite’ kwa kumkabidhi al-Meghri katika mahakama ya
Uholanzi,ili akashitakiwe kwa sheria za uholanzi kwa kosa la kulipua ndege,
kosa ambalo leo tumeambiwa hawakulifanya hata chembe!
Ilikuwa
Aprili 5 mwaka 1999 utawala wa Gaddafi ulipomkabidhi al-Meghri,ili kuepuka
kipigo cha mbwa mwizi kutoka Marekani na washirika wake.
Utaona,kumbe
Freemason wanapoua watu kwa ajali za ndege,boti,moto na meli, halafu
anasingiziwa mtu Fulani, anafungwa jela ama anauliwa-hatujasahau uongo kwamba
Irak kulikuwa na silaha za maangamizi,kumbe umbeya tu.
Al-Meghri
ameachwa huru na yuko Libya ambako anagugumia maumivu ya saratani, katika
kitanda cha mauti akisubiri mauti yanayomkodolea jicho la bashasha.
Ndivyo dunia
inayotawaliwa na Ibilisi ilivyo-Libya yenye utajiri wa mafuta, taifa la kale la
Waberiberi, iliwahi kutawaliwa na Kathago, Rumi, Wavandali na Utawala wa
Ottomans.
Italia,
iliitawala Libya tangu mwaka 1912. Uingereza na Ufaransa waliitawala Libya
baada ya Vita vya Pili vya Dunia; ikapata uhuru wa bendera Januari Pili mwaka
1952,kisha Muammar Gaddafi akaja kupindua mwaka 1969.
FREEMASONS NA
UTAJIRI WA MAFUTA
Nataka kusema
kwamba, Ulaya wameitawala Libya,wanajua utamu wa utajiri wake wa mafuta. Ulaya
na Marekani ndiyo wenye makampuni makubwa, “Supermajors” ya mafuta hapa
duniani.
Utawala wa
Gaddafi ukitaka kubinafsisha mafuta yote yawe kwa maslahi ya Walibya,
ooh…wakamkosea Mzungu. Freemasons wanatafuta kumiliki chumi za dunia nzima na
mafuta ni ‘damu’ inayobeba uhai wa dunia na mataifa yao.
Siku nyingine
nitajadili jambo hili kwa kina.
Sasa, twajua
kwa nini Freemasons waliingiza Libya katika Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil)
wapate kuishambulia na kumuulia mbali Gaddafi na wapinzani wa sera zao.
Na kwa
misingi hii hii tujue kwa nini Iran itashambuliwa baada ya Marekani kukamilisha
Uchaguzi Mkuu,Novemba mwaka huu.
Uingereza,
Ujerumani, Hispania, Ufaransa, Italia, Ureno, Uswisi hawa ni vichwa saba katika
mnyama wa Ufunuo 13, ufunuo 17, Danieli 7.
Marekani, ni
mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-18 na hawa wote wanahaha kuhakikisha wanafanya
kampeni kali na propaganda kupitia mashirika yao ya habari yenye nguvu duniani,
kuwapaka matope watu wasiopendwa,ili wapinduliwe kijeshi na AJENDA YAO YA SIRI
itekelezwe.
Katika unabii
wa Biblia, katika kitabu cha Danieli 2:43 mataifa haya ya Ulaya yameoneshwa
yakiwa yanabebwa na historia ya iliyokuwa Dola ya RUMI.
Mataifa haya
hufananishwa na vidole vya sanamu ya Nebuchadnezzar, katika sura ya Pili ya
Danieli. Ni sawa na pembe 10 za mnyama wa ajabu ambaye ni Rumi katika Danieli
7:7.
Hizi dola 10
za Ulaya, zilizoinuka baada ya dola ya Rumi, zina tabia ile ya Rumi ya Washenzi
wa kale(Danieli 7:24).
Pembe
ndogo(Danieli 7:24,25) ni nguvu isiyo mamlaka ya kisiasa ambayo ilizifukuza
Ulaya tawala tatu za Wavandali, Waheruli na Ostrogoths. Nguvu hii ilianza
kuitawala Dunia mwaka 538 AD.
Huu ndiyo
utawala uliohuishwa baadaye na utaitawala dunia nzima na kulazimisha watu
kuuabudu(Danieli 7:24,25).
Utawala huu
utapewa mamlaka na shetani na mawakala wake,Freemasons,Illuminati,Marekani na
washirika wake wa Magharibi, wataunganisha siasa na dini, watalazimisha Mfalme
aabudiwe, watakaokataa watawekewa vikwazo vya kiuchumi, watafungwa jela ama
kuuliwa.
Sasa,
demokrasia wanayojidai kueneza iko wapi? Kama watu watalazimishwa kuabudu dini
moja, wakikataa wanafungwa, mtu kwa kuwa ni mtawala anajiita Mungu(Danieli 7:25
na Ufunuo 13:1-10) ndiyo demokrasia gani hii?
Utawala
uliozuka baada ya dola ya Rumi kusambaratishwa na washenzi wa Kaskazini,
ukafukuza dola tatu za Wavandali(mwaka 454 AD),Heruli(493 AD) na Ostrogoths(538
AD) na kuanza kutawala dunia kwa jumla ya miaka 1260.
“Pembe Ndogo”
yenye macho kama mtu mwanaume, huwakilisha mamlaka itakayoongoza serikali ya
Dini na Siasa- Religio-Political Power.
Mtawala huyu
anaitwa, ‘Mpinga Kristo’ ama Chukizo la Uharibifu lililonenwa na Nabii
Danieli(Mathayo 24:15).
Katika Ufunuo
wa Yohana 17: 5 upo mfano wa utawala huu wenye nguvu na wa ina yake
unaoandaliwa kuitawala dunia,kidini,kiuchumi,utamaduni na kila nyanja.
Yohana wa
Ufunuo wa Yohana 17:5 ,katika mwaka 96 AD alioneshwa utawala huu wa mseto wa
dini na siasa.
Akaoneshwa
Jiji liitwalo “Babeli ya Siri” likiwa limebebwa na malaka(mnyama) za serikali
za Ulaya na Marekani.
Babeli, ni
Jiji la kale sana, zama za Dikteta Nebuchadnezzar, mwaka 6060 BC. Siku hizi,
Babeli ni moja ya Maajabu saba ya Dunia,kutokana na utajiri wake wa dhahabu
ulioporwa katika mahali walikopindua na kuua, bustani zenye kuning’inia katika
kuta ndefu zenye futi za mraba 400.
Bustani hizi
zilikuwa juu kutani kiasi cha futi 75 kutoka ardhini.
Hii ni nchi
ya Wakaldayo wa zamani waliokula nguruwe na kunywa mvinyo kwa wingi. Na kabla
ya kula vyakula hivi vya kitajiri, walivitoa sadaka kwa miungi yao mikuu, Bel
na Murdoch.
Danieli na
vijana wenzake wa Kiebrania waligoma kula chakula hiki na pombe zilizotolewa
dhabihu kwa miungu kabla ya kuliwa eti ili kumfanya mlaji awe na nguvu za
miungu hii mwilini mwake!
Wakasema,
kula nguruwe hizi na kunywa pombe ilikuwa kujitia unajisi na chakula cha
Mfalme(Danieli 1:1-8).
Babeli,
mabaki yake yangalipo hata leo huko kando ya Mito miwili ya Tigris na Euphrates,
mchangani-na unaweza kufika kwa treni, ni eneo la utalii siku hizi, sasa ni
makao ya mashetani na ndege wachafu kama popo, bundi n.k
Jiji hili la
siri hufananishwa na mwanamke, katika Ufunuo wa Yohana 17:5-9.
Hata jiji la
Mwanza, huitwa, “Jiji-Dada” la Wurzburgh, Ujerumani. Kumbe mji hupewa heshima
ya mwanamke?
Babeli wa
mafumbo katika Ufunuo 17:5-9 ni Jiji la Siri, litakalobebwa na Ulaya siku za
karibuni,ili kuua watu watakaokataa kumsujudia shetani na Freemasons-ndiye
mtawala atakayefuata baada ya Marekani na washirika kuitiisha dunia.
Mwanamke
huyu, “Babeli” ndani yake kuna waabuduo sanamu, wala nguruwe,walevi, waabudu
jua na mfumo wa sayari zote, wenye imani za kuongea na mizimu(spiritualism) n.k
Mwanamke
huyu, amezaa watoto, anaitwa ‘MAMA WA MAKAHABA’ na machukizo ya nchi.
Katika
Biblia, ukahaba ni pale watu wa Mungu wanapo anza kuungana na waabudu sanamu na
miungu,ulevi, ibada ya mizimu na uongo na kuacha usafi na kicho kwa Mungu
muumbaji(Hosea 1:2)
‘Uzinzi’ ni
kumwacha Mungu na kuabudu sanamu na miungu(Hosea 1:2). Mji huu Babeli, katika
Ufunuo 17:3-11 unabebwa na Ulaya na Marekani, “SUPER POWERS” zenye nyuklia na
uchumi mkubwa na wana sera moja.
Iran
watapigwa na Marekani, Israeli na Ulaya kwa sababu wakiachwa, wakawa na
Nyuklia,watapinga kuibeba Babeli hii!!
Mji huu
Babeli wa siri una ‘Meya’ wake anajiita Mungu duniani na ahera, VICARIUS
FILIIDEI na nyumerali hizi za Kirumi huwakilisha nambari 666.
Mji dada wa
Babeli umebeba kikombe cha ulevi wa mafundisho,ndiyo propaganda za uongo
duniani,ni uchafu katika imani ya kidini,Kiislam,Kiyahudi ama Kikristo.
Mji huu
Babeli uliua wapinzani wake,maana ulikuwepo zamani,mwaka 538-1798 AD.Ulikoma
Feburuari 10 mwaka 1798 baada ya miaka 1260 ukawa mwisho wa Dark Ages.
Mwanamke huyu
ambaye ni ‘Mji Dada’wa Babeli ya kale, wakati wa Nabii Yohana akiandika kitabu
cha Ufunuo(mwaka 96 AD) haukuwepo, na ukafufuka toka kuzimu Feburuari 11 mwaka
1929 AD.(Ufunuo 17:8-9)
Mji dada wa
Babeli uko juu ya milima saba. Mji ulikoko katika vilima saba Ulaya! Tazama
Ufunuo 17:9 UONE SIRI hii, na milima saba pia huwakilisha falme saba za kale,
Babeli, Wamedi na Waajemi katika serikali ya mseto, Wagiriki, Rumi ya kipagani,
Rumi ya Kikristo, Pembe Ndogo na Serikali Mpya duniani yenye Dinina
siasa(Ufunuo 17:9-11)
Naam,
Marekani na washirika wanajiandaa kuleta duniani dini mpya ya muungano wa
Freemasons,Illuminati n.k
Ni mfumo wa dini(system of
religion) ambao ni bandia. Bidhaa bandia(counterfeit) zinaigiza zile bidhaa
halisi.Bidhaa feki hufanana na feki, lakini ubora wake ni duni na utazitambua
kwa alama yake ya biashara-trade mark- kwa mfano bidhaa feki za Panasonic
huitwa,Panasoanic,hukosa ubora wa Panasonic,tujihadhari!
Dini
counterfeit ina alama(ALAMA YA MNYAMA) mnyama ni mpinga Kristo yaani utawala
bandia wa Kristo Duniani.(2Wathesalonike 2:3-4).
Kwa kawaida
utawala wa Mungu siyo wa kidunia, kwa nini dini zianze kuwaandama akina Kikwete
na kutaka kuwapindua kwa kampeni kali makanisani?
Utawala
bandia wa YESU unapinduaje serikali za dunia wakati utawala wake uko mbinguni?
Utawala wa
Mungu utaanzaje kuua watu wanaoupinga hapa duniani? Ufunuo 13 na 17 hutwambia
kwamba dini feki itaua watakaoipinga na ulishaua zamani wapinzani zaidi ya
milioni 50 yaani zaidi ya waliokufa wakati wa vita kuu ya kwanza nay a Pili.
Mnyama yaani
Mpinga Kristo ni mtawala bandia wa dunia hii(2 Thesalonike 2:3-4)
Mpinga Kristo
anajifanya Mkristo(1Yohana 2:18,19)Wapinga Kristo hutokea miongoni mwa
wakristo, na wana tabia kama za Babeli ya zamani,ulevi, ibada ya sanamu,ulaji
wa nguruwe,kiu ya utawala duniani, ibada ya jua nyota na sayari n.k
Wapinga
Kristo wameacha Injili na kuhubiri siasa makanisani,ili kuwapindua viongozi
waliopo kote duniani-wanajidai kuhamasisha demokrasia, na hujihusisha sana na
ushoga,ulawiti na ufisadi wa kiroho,ingawa wao hukazania sana watu waache
ufisadi!!
Mpinga Kristo
ndiye Pembe Ndogo ya Danieli 7:25 na ni mnyama wa Ufunuo 13:1-10. Mfumo wa
Ibada bandia, humbeba Mpinga Kristo wa Ufunuo 13,17 Danieli 7:25 na
2Thesalonike 2:2-4.
Msomaji mmoja
akanitumia SMS iliyoandikwa:
“ North Korea
na itikadi yao ya Kikomunisti watakubali kwelikuwa Allied(kuungana) na
Magharibi? Nina wasiwasi watakuwa upande wa Russia na China ili kuitetea Iran!
Pia nilitaka kuweka kumbukumbu sawa katika makala ya Gidion M kuhusu Jewish
Revolution ni 1948 na siyo 1848”.
Iran lazima
washambuliwe kijeshi,baada ya uchaguzi mkuu wa Mareni Novemba mwaka huu,la
sivyo Israeli na Ulaya watachukua jukumu hili wenyewe?
Waziri Mkuu
Benyamin Netanyahu hivi niandikapo yuko Washington kuomba kibali ili
kuishambulia Tehran. Obama anaogopa kuiingiza Marekani vitani wakati huu wa
karibia uchaguzi mkuu.
Hata hivyo,
imetangazwa kwamba Korea Kaskazini wamepewa msaada wa chakula ili waachane na
mradi wao wa Nyuklia wa Yongbyon.
Nimemwona
juzi, Hillary Clinton akiwa Pyongyang kuzungumza na yule rais kijana wa
Korea,baada ya kifo cha babaye, Kim Jong Il.
Korea
imeshatiwa kabali,haina tena ubavu wa kuipinga Marekani na washirika wake na
haina kitu,itaachana na mradi wa nyuklia na kuruhusu wakaguzi wa silaha wa
Umoja wa Mataifa ambao ni mawakala wa CIA, Mossad n.k
Maskini
Tehran wameachwa kwenye mataa,na watashambuliwa peke yao baada ya muda mfupi
ujao,ili kuandaa njia kwa Freemasons kuunda mfumo wa dini na siasa duniani.
Itaendelea.....
No comments:
Post a Comment