FREEMASON NA VIONGOZI WA TANZANIA
Sir Andy Chande akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
...Andy akiwa na Mzee Mwinyi.
...Chande na Karume.
....Chande na Sumaye.
Na Elvan Stambuli---Wa Gazeti la Uwazi.
JAMII ya Siri (Secret
Society), Freemason, imedaiwa
kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa
nchi yetu,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Madai hayo,
yametokana na
kile kinachoonekana kwamba Kiongozi
Mkuu wa Freemason, Afrika
Mashariki, Sir Andy
Chande, amekuwa akijiweka karibu na viongozi wakuu
wa nchi hii kila awamu, hivyo kuonesha kuwa kuna
kitu
anakitafuta. Kikubwa
kinachodaiwa ni kuwa Chande
anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba
kila
kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya
siri.
Inazidi
kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za
hali ya juu kujiweka karibu na
Ikulu, ikiwa na mpango
wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni
memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi wa Uwazi umeonesha kuwa Chande
amekuwa karibu na Ikulu
tangu Awamu ya Kwanza
chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius
Nyerere
na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi
mpaka awamu hii
ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Wakati inabainishwa hivyo
nchini, wachambuzi wa
mambo ya jamii za siri, ikiwemo Illuminati na
Skull &
Bones, wamekuwa wakiitaja Freemason kuwa na njama
za
kuitawala dunia kwa kuhakikisha kwamba kiongozi
mkuu wa kila nchi
duniani anakuwa memba wa jamii
hiyo.
MKAPA
Uchunguzi wa gazeti hili
umebaini kuwa Rais Mstaafu,
Benjamin Mkapa alipokuwa madarakani aliwahi
kualikwa akiwa na mkewe katika shughuli ya
Freemasons kutimiza miaka 100
nchini, sherehe
iliyojumuisha wageni waalikwa 350 kutoka nchi
mbalimbali duniani japokuwa hapa nchini haikutangazwa sana.
Kwa
mujibu wa Sir Andy Chande katika mahojiano yake
na mwandishi mkongwe nchini, Ernest C. Ambali wa
Gazeti la The Guardian, lililokuwa mitaani
Oktoba 8,
2004 alitaja waziwazi kuwa mgeni rasmi katika
shughuli yao ni
Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama
Anna Mkapa. Katika shughuli hiyo pia
walikuwepo
wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia, mawaziri n.k.
NYERERE
Sir Andy Chande akiwa nchini
India katika Mji wa
Chennai kuzindua hekalu lao la East Star, alieleza
kwamba marais wawili wa kwanza wa Tanzania
hawakuwa Freemasons lakini
walifahamu taasisi hiyo ni
nini na inafanya nini katika nchi hii. Aidha,
aliwahi
kuweka wazi kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania,
Mwalimu
Julius Nyerere alikuwa akiijua taasisi hiyo na
aliwahi kuikingia kifua
ilipotaka kunyang’anywa jengo
lao ambalo lipo Sokoine Drive, katikati ya
Jiji la Dar es
Salaam linalofahamika kama Freemasons Hall.
Uchunguzi
umeonesha kuwa viongozi wengi wakuu wa
serikali wanafahamu shughuli za
taasisi hiyo, hali
iliyothibitishwa na kiongozi wa Freemasons, Sir
Chande
ambaye amekuwa akipiga nao picha mara kwa mara
wakati wa hafla. Viongozi
wengine wa nchi waliowahi
kualikwa au kumualika kiongozi wa taasisi
hiyo ni Rais
Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani
Karume,
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na
Rais Mstaafu, Sheikh Ally
Hassan Mwinyi.
KITABU CHAKE
Rais mstaafu, Mkapa
katika kitabu cha Sir Andy
Chande kiitwacho ‘Shujaa wa Afrika, Safari
kutoka Bukene’ ameandika utangulizi akisema Chande alikuwa
akijulikana
kama JK na alifahamiana naye baada ya
kumuingiza katika bodi ya Shule ya
Shaaban Robert.
Mkapa amesema Sir Chande ametambuliwa na kupewa
heshima na vyombo vya taifa na vya kimataifa,
heshima ambayo anaistahili
kabisa. “Mimi nafurahi kuhusishwa
na kutambuliwa kwa sifa na heshima
anayopewa,”
alisema Mkapa katika maandishi yake. Mnajimu
maarufu
nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye
amekuwa akiandika makala za
Freemasons katika
gazeti hili, alipohojiwa na mwandishi wetu kama
viongozi hao wanafahamu taasisi hiyo inajishughulisha
na nini, alisema
japokuwa hakuna anayejua
wanachokifanya wanachama wa Freemasons huku
uraiani lakini anaamini kuwa viongozi wakuu wa nchi
wanajua kila kitu.
“Kwa
kawaida huwezi kualikwa katika chama au taasisi
fulani bila kujua
shughuli zao hasa kwa viongozi
wakuu kama hawa, sasa kama waheshimiwa
Mkapa,
Mwinyi, Sumaye, Karume na Kikwete waliwahi kualikwa
au kumualika
Sir Andy Chande ni wazi kuwa
wanafahamu shughuli zake na taasisi yake,”
alisema
Maalim Hassan.
KIMATAIFA
Hivi karibuni, nchini
Kenya, aliyekuwa Waziri wa
Usalama, Profesa George Saitoti aliyefariki
kwa ajali ya
helikopta, kifo chake kimehusishwa na Freemasons
kwa kudaiwa kuwa alipokuwa Makamu wa Rais wa Kenya
wakati wa utawala wa
Daniel Arap Moi, aliwahi kupiga
marufuku makanisa au dini
zinazojihusisha na imani za kishetani.
Imeelezwa kuwa wengi wanadhani
kuwa angeweza
kuwa Rais wa Kenya iwapo angegombea hivyo
kurejesha amri
yake ya kupiga marufuku imani
ambayo yeye haiamini.
Aidha kuna baadhi
ya viongozi duniani wanahusishwa
na Freemasons baada ya kuonekana picha
zao
wakionesha alama za taasisi hiyo, baadhi yao ni Rais
Barack Obama,
George Bush, Sadam Hussein na
Muammar Ghaddafi.
WANAFUNZI WA SHULE YA MPECHI NA SABASABA, WAKIWA KATIKA MAANDAMANO
Wanafunzi wa Shule za Mpechi na Sabasaba, wakiwa katika maandamano baada ya mwanafunzi mwenzao kugongwa na Tax, na kupoteza maisha yake, katika eneo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya. walikuwa wakitoa wito kwa madereva kuwa makini, aidha waliomba serikali ijemge matuta katika eneo hilo.
Picha na Jonas Tave
Moto mkubwa ulioteketeza sako la sido mkoani Mbeya vibanda vingi viliteketea.
Lakini Biblia inasemaje? Mathayo 24.... Hizi ni kengele za kutushitua tujue kua tunaishi nyakati za mwisho,
1 comment:
Watoto, ni wakati wa mwisho; kama vile mlivyosikia kwamba mpinga kristo yuaja, hata sasa wapinga kristo wengi wamekwisha kuwepo. kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho, 1 Yohana 2:18
Adui anajiandaa kwa ajili ya kampeni yake ya mwisho dhidi ya kanisa. Amejificha sana asionekane na watu kiasi kwamba wengi hawafikiri ya kwamba anishi, na vivyo hivyo, wengi hawatambui shughuli na ukubwa wa uwezo wake.
Mwanadamu ni mateka wa Shetani na kwa asili anafuata mapendekezo yake na matashi yake. Ndani yake hakuna nguvu ya kupinga na kuukataa uovu. Ni pale tu Kristo anapokua ndani yake kwa imani iliyo hai. Namna yoyote nyingine yakujilinda haifai kabisa. Ni kupitia kwa Kristo peke yake ndipo uwezo wa Shetani unazuiwa. Huu ni ukweli wa muhimu sana ambao wote wanapaswa kuuelewa. Shetani anashughulika sana kila wakati, akienda huku na kule, akipanda na kushuka duniani, akitafuta mtu ammeze. Lakini ombi la dhati la imani litachanganya jitihada zake hata zile zenye nguvu sana...
Shetani anategemea kuwashinda watu wa Mungu kwa ujumla katika maangamizi yanayokuja katika dunia. Wakati kuja kwa Kristo kunapokaribia, yeye (Shetani) atazidisha azma yake na uthabiti katika jitihada ya kuwaangusha. Wanaume kwa wanawake watainuka wakidai kuwa na nuru mpya au ufunuo mpya ambao kwa kawaida unavuruga imani ambayo imekuwepo katika msingi imara siku zote. Hata ingawa mafundisho yao hayatakuwa na vithibitisho vya neno la Mungu, bado bado roho zitadanganywa. Taarifa za uongo zitasambazwa na baadhi watanaswa katika mtego huu... Hatuwezi kuwa wazembe katika kuangalia aina yoyote ile ya makosa, kwani Shetani anadumu kutafuta namna ya kuwavuta watu toka katikz kweli...
Wapo watu ambao hawako imara kitabia. Wako kama donge la tope la udongo wa mfinyanzi ambalo laweza kuumbwa katika mwonekano wowote... Udhaifu huu. kukosa maamuzi, kutokuwajibika, vyapaswa vishindwe. Katika tabia ya kweli ya Ukristo ipo hali ya ujasiri usuo wa kawaida ambao hauwezi kutengenezwa au kushushwa hata hali iwe mbaya kiasi gani. Watu wanapaswa kuwa na msimsmo katika maadili, unyofu ambao hauwezi kubezwa, kuhongwa au kutishwa.
Mungu ameweka mipaka ambayo shetani hawezi kupita. Imani yetu iliyo takatifu sana ndiyo mipaka; na kama tutajijenga wenyewe zaidi katika imani, basi tutakuwa salama katika utunzaji unaotoka kwa Mwenyezi.
Mungu akubariki sana unapotafakari ujumbe huu.
Post a Comment