Friday, May 18, 2012

UTAWALA WA FREEMASON KATIKA BIBLIA TAKATIFU - SEHEMU YA TATU.


Somo la 3.

FREEMASONS NA IBADA YA SANAMU INAYOKUJA

NIREJEE historia ya Socrates, Yule mwanafalsafa wa Ugiriki. Ndiye mwalimu wa Plato; Plato ndiye mwalimu wa Aristotle.
Encyclopedia Britannica, hutuambia kwamba, Aristotle (384-322 BC)ndiye mwanasayansi wa ukweli katika historia ya ulimwengu.Hawa wanafalsafa wengine,wamufuatisha kile alichofikiri yeye kwanza.
Socrates, aliuliwa na mamlaka ya Athens,kwa kuwa aliwafundisha wanafunzi wake,akina Plato, kwamba hakukuwa na miungu 391 juu ya kilele cha Mlima Olympus. Alifundisha kwamba, kulikuwa na Mungu mmoja tu,naye aliishi mbinguni.
Kwamba, magalaksi(galaxies) yoote aliyaumba yeye pamoja na nyota na sayari zote ulimwenguni, na kwamba dunia haikutokea kwa bahati kwa njia uibukaji(evolution) kama alivyofundisha Charles Robert Darwin katika karne ya 19.
Sokrati huyu, alipewa alipewa rehema ya juma moja, ili ayakane mafundisho yake ya kuidharau miungu ya taifa lake la Ugiriki; alikataa na mwisho wa siku alihukumiwa hukumu ya kifo.
Alipewa sumu ainywe mbele ya hao wanafunzi wake akina Plato, akianywa sumu hiyo,mwili ulipopatwa ganzi akalala na kufunikwa shuka akiwa tayari amekufa-waliahidi kumlipa posho ya chakula kila siku kama angeyakana mafundisho yake hayo.
Nataka kusema kwamba, Sokrati alishikilia msimamo,mwisho akauawa mbele ya wanafunzi wake. Naam, ukweli huandamana na hukumu ya mauti.
Msomaji,utambue kuwa ibada ya miungu katika ulimwengu ule lilikuwa suala la maisha au la mauti duniani,tangu Ulaya hiyo ya akuna Sokrati,Plato na Aristotle na ndivyo itakavyokuwa tuendako.
Hao wazungu wa Magharibi,hawakuwahi kuijua dini. Walikuwa washenzi na watambikia mizimu na waabudu sanamu.
Unajua watu wa kwanza kumwabudu Mungu mmoja ni Waisraeli wa kale? Unajua dini ya Ukristo imekuja wakati wa Yesu na mitume?
Mitume kama Petro, Paulo n.k ndiyo waliopeleka Ukristo Ulaya,hususan jijini Rome, na wakaishia kukataliwa na kuuliwa kinyama?
Hata Afrika ilitangulia kumjua Mungu kuliko hawa; tazama historia ya nchi kama Ethiopia, Sudan, Misri n.k
Edward A. McDowell, Profesa wa Agano Jipya katika Seminari ya Baptisti,Nort Carilina,Marekani, ameandika katika kitabu kiitwacho The Meaning and Message of Revalation,kwamba watawala wa Romi ya kale(emperors) walilazimisha raia wawaabudu, ambao walijiona ndiyo miungu!
Rumi ya kale kulikuwa na dini ya kuwaabudu wafalme waha wa Rumi. Julius Caesar, alitengeneza SANAMU lake lililowekwa miongoni mwa masanamu mengine hekaluni mwake-hekalu la Kaisari!
Kaisari Augusto(27 BC-14 AD) alikubali cheo kiitwacho, “Augustus” kutoka katika Baraza la seneti. Hiki ni cheo cha miungu.
Caius Caligula( AD 37-41) aliwalazimisha raia wa milki hiyo ya Rumi dunia nzima waiabudu sanamu yake. Jitihada zake za kuisimika sanamu hiyo katika hekalu la mjini Jerusalemu zikapingwa vikali sana na Wayahudi; kwa kuwa wao walijua ibada ni kwa Mungu tu ambaye huishi mbinguni,na hawakilishwi na masanamu!
Domitian, alikuja kupunguza mgogoro mkubwa kati ya Wakristo na makaisari wa Kirumi waliotaka kuabudiwa na watu wote,na wale waliopingwa, waliuawa kwa kuraruliwa na wanyama katika viwanja ambavyo siyo tofauti sana na stadium za sasa hivi.
Kaisari Nero alitaka raia wa makaloni yote chini ya dola hii wawaone wao kama miungu. Hatimaye masanamu yaliingizwa kanisani,wakati Wakristo wakitaka kujikomba kwa hawa makaisari walioanza kujifanya wameongoka na kuwa wakristo.
Aina hii ya madhehebu ya ibada ya wafalme ni maarufu hata Asia; na ilidhaniwa kumwabudu Mfalme ndiyo ‘Patriotism’ yaani uzalendo kwa taifa lako.
Dola ya Waislam wa Ottoman(Uturuki) ambayo sasa imejisalimisha NATO, walijaribu kuzuia uhalifu huu, lakini kama tulivyoona katika makala zilizotangulia, dola hii ya Ottoman ilianguka katika karne ya 16 AD.
Kwa hiyo, zama za Ukristo,watu waliokataa kuwasujudia ma-emperor wa Rumi walionekana waasi, watukutu na wasio wazalendo-waliuliwa,kufungwa jela na wengine walifukuzwa wakawa wakimbizi huko uhamishoni,wengine ndiyo waliokimbilia Marekani wakiogopa mateso Ulaya.
Wakristo, walilazimishwa kuwaabudu makaisari,kuwatolea sadaka katika sanamu zao huku wakitamka maneno haya, “Kyrios Kaisar” maana yake, “Bwana Mungu wangu Kaisari”!!
Lilikuwa zoezi dogo tu; lakini lenye kukudai uaminifu wako wewe mkristo,Muislam,Budha,Hindu n.k kwa Kaisari badala ya Yule Mungu wako unayemwabudu wewe kwa kicho na kutetemeka.
Wakazi wa Afrika Mashariki wanajua mambo haya ya “Kasinge Mwombeki” kumbe yalianzia Ulaya. Kiongozi wa kidunia alikuwa nawinda heshima ya kimungu,ili mwanadamu apate kumwabudu yeye.
Nimeleta kisa hiki ili tujue maana hasa ya kukufuru. Mwanadamu anapojiita Mungu,ndiyo kukufuru,anapowalazimisha wanadamu wenzake kumwabudu yeye badala ya Mungu wa mbinguni-ndiyo kukufuru.
Msomaji mmoja anataka kujua,namna mamlaka(Mnyama) ya Danieli 7:23-25 na Ufunuo 13:1,4-8 na pia Ufunuo 17:3-11 itakavyojigeuza kutoka mamlaka ya siasa na kuwalazimisha watu wa dunia nzima kuiabudu,kama alivyoabudiwa Kaisari wa Rumi na SANAMU yake,sawa sawa na Wakristo ama Waislam wanavyomwabudu Mungu.
Mamlaka itakayofuata duniani baada ya Marekani na washirika wake kuitiisha dunia nzima,itatengeneza sanamu(Ufunuo 13:14-15).
Sanamu hii itadai kila raia wa dunia nzima(sensa ya dunia nzima ipo,na kila raia wa dunia anajulikana) kutoa heshima yake kwa Mtawala huyu mpya wa dunia, ambaye atarithi enzi zote za tawala za Kaisari. Watu watadaiwa kuonesha kifo kwa huyu mtawala ili kuonesha uzalendo wao kwa kutamka maneno, “Kyrios Kaisar” yaani Bwana Mungu Kaisari badala ya kutamka,”Kurios lesous” yaani Bwana Yesu ama kwa Waislam, ‘Allah Akbar”!!
Ugomvi wa sasa wa Marekani,Ulaya, Israeli na washirika wao wengine, ni kitu gani kama siyo kutaka dunia iwe na mtawala mmoja, na taifa la Kiislam kama Iran linagoma?
Hivi leo,kuna vitu vya kijesi(Military Base) nyingi za Marekani huko Ghuba ya Uajemi. Na vita vikianza, tayari Iran iko kati kati-mataifa mengi ya Kiarabu kama Kuwait,Qatar, UAE wameruhusu vituo hivi vya kijeshi vya Marekani,ili Waislam wenzao wakileta jeuri,wananyeshewa mvua kali ya mabomu na risasi za rashasha(automatic rifles).
Huu ndiyo ulikuwa ugomvi wa Wakristo na Makaisari wa Rumi zama zile.Wakristo wengi waliteswa Ulaya kwa kugoma kumsujudia Kaisari na sanamu zake,na ndivyo itakavyokuwa,kwamba tunakwenda kulazimishwa kuiabudu sanamu ya Kaisari mamboleo, ambaye ndiye Marekani na washirika wake wanamwandalia barabara kuelekea ‘Zulia Jekundu’.
Kati ya Mungu na Kaisari wa Rumi,kulikuwa na ugomvi,mmoja akidai kuabudiwa na mwanadamu. Kuna nguvu mbili duniani zinashindana kutaka kuabudiwa,na kutolewa sadaka, lazima mmoja apewe heshima na kicho. Ukikataa kuiabudu mamlaka,unauawa.
Juma lililopita,nikamwona Waziri Mkuu wa Israeli, Benyamin Netanyahu,akimwambia Rais Obama wa Marekani huko White House:
“Iran wanatuita sisi Shetani mdogo; na ninyi Marekani wanawaita Shetani mkubwa! Kwa nini wasishambuliwe na vinu vyao vya Nyuklia kuharibiwa,kabla hawajaanza kutushambulia sisi?” Alisema Netanyahu.
Iran wanaiita Israeli na Marekani kuwa Shetani. Tabia ya Shetani ni kujiinua mahali alipo Mungu na kudai kuabudiwa-na tabia hii imeonekana wazi katika siasa za dunia. Marekani ni Baba wa dunia, Israeli wanafanya wapendavyo, hawaguswi.
Ujinga ni watu kudhani Israeli ni taifa teule la watu wa Mungu-tuwasaidie, Israeli walikoma kuwa taifa teule la watu wa Mungu walipomuua Yesu,Mitume na Manabii na mashahidi kama Stephano,wakasema damu zao ziwe juu ya vichwa vyao na vichwa vya watoto wao.
Unajua Yerusalem ulibomolewa na majeshi ya Kirumi mwaka 70 AD? Unajua W     aisraeli wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, Waarabu wakaikalia hadi huo mwaka 1948 waliporejeshwa kwa msaada wa Umoja wa Mataifa? Marcus Mpangala ameandika jambo hili kwa kina.
Taifa la Israeli lilisha mwasi Mungu; leo wamekaribia kumalizwa na Adolf Hitler, damu ya manabii iko juu ya vichwa vyao, isipokuwa Muisraeli mmoja mmoja akitubu kwa kiburi chao hiki na ukatili dhidi ya mitume na manabii wa Mungu.
Ni kwa sababu hii, Israeli,Ulaya,Marekani na Vatican wamekubaliana kutengeneza mfumo mmoja wa dini,ili “Kaisari” mmoja miongoni mwao aabudiwe na dunia nzima.
Huku sasa ni kuondoa UHURU WA DINI,Demokrasia na haki za binadamu. Siku hizi haki za binadamu ni ushoga, usagaji na wanawake kutaka kuoa wanaume zaidi ya mmoja! Waliosikia siku ya wanawake duniani wanajua tuendako.
Haki za Binadamu!! Haki hizi zinaletwa na miungu ya Ulaya na Freemasons na Illuminati.
Mwandishi mashuhuri hapa nchini, William Shao, amepata kuandika katika jarida la Rai juu ya sanamu ya mwanamke aliyeketi juu ya mnyama huko Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya(EU) mjini Brussels.
Shao, aliandika kwamba sanamu hiyo inayofanana sana na kile kinachosemwa katika Ufunuo 17:3-11 iko mbele ya Ofisi za European Union huko Brussels, Ubelgiji. Nimewahi kuongea na Shao siku za karibuni juu ya kitabu chake kuhusu Freemasons.
Sasa,kama tunabahatisha,kama wengine wanavyodhani, ni suala la kila mmoja kutafiti na kuamua. Tunawaandikia wenye hekima; hatuna shida na wapumbavu!
Mwanamke aliye sawa na huyu wa mjini Brussels, ni Yule aliyemwona Mtume Yohana katika Ufunuo 17:3-11. Anaitwa jina la siri, “Yezebeli”.
Naam, nataka tumjadili Yezebeli. Yezebeli anabebwa na Umoja wa Ulaya(EU) na washirika waao,Israeli na Marekani.
Yezebeli huyu alikuwa muumini wa kanisani Thiatira(Ufunuo 2:20-24) na alijiita Nabii,alifundisha waumini watu wa Mungu ili kuwapoteza,ili wazini(kuabudu miungu) na kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na masanamu ya makaisari wa Rumi.
Naam, Yezebeli hataki kutubu,ni mzinzi,nusu yuko kwa Mungu,nusu ibada ya sanamu.Uzinzi wa kiroho ni watu wa Mungu kutambikia mizimu na miungu na kusujudia sanamu(Hesabu 25:1-3).Yezebeli anatufundisha sasa kutambikia miungu ya Misri, Babeli,Uyunani na Rumi,na somo hili tumejifunza katika makala tulizotangulia kuona.
Yezebeli, anavaa nguo za rangi ya zambarau na nyekundu(Ufunuo 17:4).Mwandishi Gidion M. juzi aliandika kwamba nguo hizi za rangi ya zambarau na nyekundu walivaa wafalme wa Babeli na makuhani wa miungu.
Labda, ndiyo maana mama huyu ana jina linguine la siri-‘BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA’!!
Huyu Yezebeli anayebebwa na wafalme hukoo Umoja wa Ulaya(EU) anao watoto ambao pia ni makahaba.Watoto wa changudoa nao huwa changudoa kwa sababu ya mivuto mibaya. Sasa mama huyu ni nani? Amewazaa akina nani? Tafakarini.
Yezebeli, alikuwa Malkia aliyejifanya mlinzi na Mfadhili wa manabii wa Baali na Ashtorethi zama za Nabii Eliya(1Wafalme18:19).Ashtorethi alikuwa mungu mkuu mke wa Wafoeniki na Baali alikuwa mungu mkuu mume.
Nani mungu mkuu mke-Ashtoreth? Gidion M. AREJEE SOMO HILI, ili wasomaji waelewe. Tunajifunza,Yezebeli alikuwa adui mkuu wa Eliya,Nabii wa Mungu, na alitaka kumuua Eliya. Hapa Yezebeli anafananishwa na mtu ama kikundi cha watu wanaotaka kuwaua watu kwa sababu wamekataa kuabudu Baal na Ashtoreth. Kwani kuabudu dini ni lazima?Hata Mungu halazimishi.
Yezebeli wa kanisani(Thiatira) anawaongoza waumini ‘kuzini’ yaani kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa masanamu(Ufunuo 2:20).
Yezebeli alikuwa mke wa Mfalme Ahabu,aliyehamasisha Waisraeli wa kale kumwacha Mungu(hata sasa wamemwacha Mungu) na kuabudu Baali na Ashtoreth,kitu hiki huitwa uzinzi. Waisraeli wa sasa wanamwabudu Baali,mungu mume wa Ufoeniki na mungu mke ndiye Ashtoreth, na mataifa mengi watalazimishwa kumwabudu huyu,na wanamwabudu Ashtoreth hata katika siku kuu zijazo za Pasaka, Krismasi,MWAKA Mpya n.k
Wapendwa wakristo,someni 1Wakorintho sura 8 MTAONA jambo hilo lililoanza kutokea AD 95. Uzinzi ni kumwabudu Kaisari,ni ibada ya sanamu, ibada ya sanamu ni kinyume na AMRI 10 ZA MUNGU,ni kinyume cha amri ya Pili(Kutoka 20:4-6).
Tuijadili kidogo miungu hii.
Zeus,
mwaka 29 BC hekalu lilijengwa na Kaisari Augusto,LIKAWEKWA WAKFU kwa ajili ya Kaisari huko Pergamo,na mjini Rome sanamu hilo liliwekwa makau makuu ya Sinodi ya Kanisa.
Tumeona maofisa wa serikali ya Rumi wakilazimisha watu kumwabudu Kaisari has huko Pergamo. Huyu Zeus(Jupiter) sanamu lake lipo Olympia na ni moja ya MAAJABU SABA YA DUNIA.
Huyu Zeus ni mfalme wa miungu na anaketi katika kiti cha enzi.Sanamu hili limejengwa mwaka 457 BC na linaabudiwa dunia nzima kwa njia anuwai.
Utaona sasa Yezebeli wa leo akiwa amebebwa na Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels,Ubelgiji, tunalazimishwa kumwabudu na kumtolea dhabihu. Yohana anasema Wafalme wa dunia wamezini naye na wafanyabiashara wamepata mali kwa nguvu ya kiburi chake(Ufunuo 18:1-3).
Unataka utajiri? Yezebeli ni jibu lako,utauza maua wakati wa siku kuu zake, utauza pombe kuliko wakati wowote, utauza miti ya Krisimasi n.k
Nimegusa jiji la Rome lililojengwa miaka 2765 iliyopita, watawala wake maarufu sana ni Julius Caesar, Augusto, Tiberio, Gaius,Claudio,Nero,Galba, Vespasianus,Titus orodha ni ndefu.Hawa walitengeneza masanamu yao ili yaabudiwe. Hata masanamu ya Nyerere yapo mengi-hatujaambiwa kuyasujudia.
Freemasons ni hatari. Ugiriki imeathiri dunia nzima kwa maarifa yake,tamaduni zake, miungu yake na ustaarabu wake. Demokrasia imeanzia Ugiriki,lakini leo ni nchi masikini, wanapewa msaada na Eurozone!
Mataifa ya kiarabu yanazimwa yasiwe Super power. Afrika utajiri wake ullikwenda wapi? Niliwahi kuhoji,kwanini Ashanti isiendelee kuwa dola ya Ghana ya Mwafrika, eti siku hizi ni kampuni ya Mzungu ya kuchimba dhahabu hata hapa Tanzania?
Unaweza kusema sisi ni mafala! Lakini, Babeli ama Iraki,Misri, Wamedi na Waperizi na Wagiriki wako wapi?
Nani alianza kuandika? Nani alianzisha hesabu? Viwanda vya kufua chuma havikuwa Afrika?
Zbigniew Brzezinski,mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani enzi za Jimmy Carter alisimamia Mradi wa kutengeneza Virsi vya Ukimwi huko kilomita 75 kutoka Washington miaka ya 70.Lengo lilikuwa kupunguza watu duniani kwa sababu rasimali zinazidi kuwa chache.
Ukimwi ni silaha ya kupunguza idadi ya watu,chakula ni kidogo, watu wengi,makazi yanazidi Wazungu wamekwenda hata mwezini,Mars ili kutafuta nishati.
Sasa,lazima kuwepo na mkakati wa siri kuwapunguza,wanaobaki ni wale watakaosujudu miungu yao-hawa ni mawakala wa shetani. Tutafanyeje? Mtafuteni Mungu wa kweli.
MWISHO.


2 comments:

Anonymous said...

Inatisha kama si Yesu kutuokoa itakuwaje?

Erisha - Musoma.

Anonymous said...

Sasa kama hali ni hivyo tutaokolewa kweli? ama wote tutapotea!!!

Ashery Nipo Arusha.