“Bali mmebatilisha shauri Langu, Wala hamkutaka maonyo Yangu” (Mithali 1:25).
Wakati wa usiku malaika wa Mungu alimjia Balaamu akiwa na
ujumbe, “Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana
wamebarikiwa.”…
Kwa mara ya
pili Balaamu alijaribiwa tena. Katika kujibu ushawishi wa wale wajumbe
alidai kuwa makini na mwenye uadilifu mkubwa mno, akiwahakikishia kwamba
hakuna kiasi chochote cha dhahabu na fedha ambacho kingeweza
kumshawishi kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Lakini alitafuta
kukubaliana na ombi la mfalme huyo; na licha ya kwamba alikuwa
amedhihirishiwa bayana mapenzi ya Mungu, aliwahimiza wale wajumbe
wangoje, ili aweze kuulizia tena kwa Mungu; kana kwamba Yeye Asiye na
Ukomo alikuwa mwanadamu, awezaye kughilibiwa.
Wakati wa
usiku Bwana alimtokea Balaamu na kusema, «Kwa kuwa watu hawa wamekuja
kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo
utakalolitenda, basi.» Huo ndio umbali ambao Bwana angeliweza kumruhusu
Balaamu ayafuate mapenzi yake mwenyewe, kwa sababu alikuwa amedhamiria
juu ya hilo. Hakutafuta kuyatenda mapenzi ya Mungu, bali alichagua njia
yake mwenyewe, na kisha akajitahidi kujipatia kibali cha Bwana.
Wapo maelfu hivi leo wanaoenenda katika njia ya namna hiyo.
Wasingeliweza kuwa na ugumu wowote wa kuuelewa wajibu wao kama
ungelipatana na mielekeo yao. Umeleezwa bayana mbele yao katika Biblia
au umeoneshwa waziwazi kwa mazingira na mawazoni. Lakini kwa sababu
ushahidi huu hupingana na shauku na mielekeo yao mara kwa mara wanauweka
pembeni na kuthubutu kumwendea Mungu ili kutafuta kujua wajibu wao. Kwa
uangalifu mkubwa unaoonekana dhahiri wanaomba kwa muda mrefu na kwa
bidii ili wapate nuru. Lakini Mungu hatadhihakiwa. Kwa kawaida
huwaruhusu watu wa namna hiyo wafuate shauku zao wenyewe na kukabiliana
na matokeo husika….
Mtu anapouona wajibu wake bayana, hebu asithubutu
kumwendea Mungu akiwa na ombi kwamba asamehewe ili asiufanye. Badala
yake anapaswa, kwa roho na unyenyekevu na kujisalimisha, aombe nguvu na
hekima ya kimbingu ili kutimiza madai yake.
No comments:
Post a Comment