“Nikamnyenyekea Bwana wakati huo, nikamwambia,… Nami nakuomba
nivuke, nikaione hiyo nchi nzuri iliyoko ng’ambo ya Yordani, mlima ule
mzuri, na Lebanoni. Lakini Bwana alikuwa amenikasirikia kwa ajili yenu,
asinisikize; Bwana akaniambia, Na ikutoshe, usinene nami zaidi jambo
hili”
(Kumbukumbu 3:23-26).
(Kumbukumbu 3:23-26).
Kamwe haikuwahi kutokea, hadi pale vilipodhihirishwa katika kafara
ya Kristo, ndipo ambapo haki na upendo wa Mungu vilioneshwa kwa kiwango
kikubwa sana kuliko katika kushughulika Kwake na Musa. Mungu alimzuia
Musa asiingie Kanaani, ili afundishe somo ambalo kamwe halipaswi
kusahaulika—kwamba Yeye anahitaji utii kamili, na kwamba wanadamu
wanapaswa kujihadhari ili wasijitwalie utukufu unaomstahili Muumba wao.
Asingeweza kujibu ombi la Musa aliposihi apewe nafasi ya kushiriki
urithi wa Israeli, lakini Mungu hakumsahau wala kumwacha mtumishi Wake.
Mungu wa mbinguni alielewa mateso ambayo Musa alikuwa ameyastahimili;
alikuwa ametazama kila tendo la utumishi wenye uaminifu katika miaka
hiyo yote ya mapambano na majaribu. Juu ya Mlima Pisga, Mungu alimwita
Musa kuingia katika urithi mtukufu sana usio na ukomo ukilinganishwa na
ule wa Kanaani ya duniani..
Katika ule mlima ambako Yesu
alibadilikia sura, Musa alikuwepo pamoja na Eliya, waliokuwa
wamehamishwa kwenda mbinguni. Walitumwa kama wabeba-nuru na utukufu
kutoka kwa Baba hadi kwa Mwanawe. Kwa hiyo, dua ya Musa, iliyotamkwa
karne nyingi hapo kabla, hatimaye ilijibiwa. Alisimama kwenye “mlima ule
mzuri,” ndani ya urithi wa watu wake….
Musa alikuwa mfano
wa Kristo…. Mungu aliona vyema kumfunza Musa katika shule ya mateso na
umaskini kabla hajaandaliwa kuliongoza jeshi la Israeli hadi Kanaani ya
duniani. Israeli wa Mungu, wanaosafiri kuelekea Kanaani ya mbinguni,
wanaye Amri Jeshi asiyehitaji mafundisho ya wanadamu ili kumwandaa kwa
ajili ya utume Wake kama kiongozi wa kimbingu; hata hivyo alikamilishwa
kupitia mateso; na “kwa kuwa [Yesu] Mwenyewe aliteswa alipojaribiwa,
aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa” (Ebr. 2:10, 18). Mkombozi wetu
hakuonesha udhaifu au kasoro yoyote ya kibinadamu; hata hivyo alikufa
ili kutununulia sisi urithi wa kuingia katika ile Nchi ya Ahadi.
“Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama
mtumishi,… bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye
nyumba Yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari
ya taraja letu mpaka mwisho” (Ebr. 3:5, 6).
No comments:
Post a Comment