"Imeandikwa hivii; "Uzinzi na Divai na Divai mpya huondoa fahamu za mwanadamu" Hosea 4:11.
Dhambi ya uzinzi licha ya kwamba sio uzinzi peke yake
utakaowakosesha wengi wasiingie mbinguni; lakini neno la Mungu
limeizungumza kwa uchungu madhara yake kama mwanadamu angeliielewa.
Paulo katika Wakorintho pia alisema mtu akizini msichangamane naye na
kwa baadhi ya makanisa mtu anayefumwa katika uzinzi huondolewa katika
ushirika wa kanisa. Dhambi hii ni kweli ni sawa tu na dhambi zingine;
lakini imetajwa katika dhambi kuu mbili zinazoondoa fahamu za mwanadamu.
Biblia inaelewa kwa uwazi kupitia nabii Hosea kwamba Uzinzi na
Divai huundoa fahamu za mwanadamu. Mtumishi wa Mungu Sulemani ingawa
aliandika yeye mwenyewe katika Kitabu cha Mithali kwamba; "Mtu aziniye
na mwanamke hana akili, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake" Bado
kama mwanadamu anayo historia ya kutenda kosa hilo kwa kuoa akina mama
700+300 masuria jumla akawa na 1,000 wake wa kulala nao kimapenzi.
Uzinzi na ulevi ni dhambi kuu zinazovuma na zimeshika nafasi ya
kwanza katika ulimwengu wa sasa. Wachungaji, mapadre, maaskofu,
watumishi wengi wa Mungu, wainjilisti, wahubiri, na waumini wa madhehebu
mbalimbali hatuko nyuma katika kujishughulisha na dhambi ya uzinzi na
ulevi( Divai) ingawa dhambi ni dhambi bila kujali ni uongo, majungu,
masengenyo, wizi wa zaka, ulawiti, ubakaji, uchonganishi, dharau,
kiburi, majivuno na kiola aina ya ubaya unaomwandama mwanadamu; ila
katika kuondoa ufahamu wa mwanadamu (yaani anakuwa punguwani
asiyejielewa kiroho na kuwa mtumwa wa uovu huo) ni Uzinzi na ulevi kama
asemavyo Mungu kupitia nabii Hosea, na mtume Paulo.
Angalia mtu
akilewa anavyokosa adabu, asivyojiheshimu, anavyopiga kelele,
anavyosumbua mke au mme wake, anavyotishia watu, anavyopiga mke,
anavyopiga mume, anavyopiga watoto! Je, ulevi na kunywa japo kidogo
mbele za Mungu ni halali? imeandikwa nini katika Isaya 28:7? ni kosa
kumpa mtu kileo. Katika Biblia yaani maandiko matakatifu hakuna fungu
linalosema kunywa kidogo ila usilewe, halipo ila ni fundisho miongoni
mwa mafundisho ya shetani kwamba watu wanywe kidogo ila wasilewe!
Niliwahi kuona mtu mmoja aliyejiita mtumishi wa Mungu akiwa amevalia
kanzu akienda katika tukio la ujenzi wa makaburi akawa akizibariki
pombe! wakati huo nikiwa gizani kama yeye niliona ni jambo jema; baada
ya kupata mafunuo ya Mungu kupitia neno lake nikagundua yule alikuwa
mtumishi wa shetani aliyevaa kanzu ya kondoo.
Ulevi umekatazwa kabisa; wapendwa wakristo wenzangu; Uzinzi na ulevi tumwombe Mungu atusaidie dhambi hizi zinaondoa fahamu za mwanadamu; na ujue ya kwamba Fahamu za mtu zikiondoka mtu huyo huitwa mwendawazimu. Soma tena Hosea 4:11 ujue mambo yanayoondoa fahamu za mwanadamu. Mungu halazimishi, ila anaonya ili isiwe siku ya kutupwa katika ziwa la moto ukamlaumu kwamba hukumu zake si za haki. Ni lazima siku zote Mungu aonye ukatae ili siku ya hukumu maneno yaleyale uliyoyakataa yawe sheria mbele zake ya kukugeuka. Amua leo kumtii Mungu katika kila jambo ili uwe salama. Haleluya!

No comments:
Post a Comment