📖“Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usiku-bali.” Mithali 1:10
👉🏼Samsoni
wakati wa matatizo makuu yaliyomsibu alikuwa na chimbuko lile lile la
nguvu kama ilivyokuwa kwa Yusufu. Angaliweza kuchagua jema au baya kama
apendavyo. Badala ya kushikilia nguvu za Mungu, aliruhusu tamaa yake
mbaya imtawale. Uwezo wa kufikiri ulipotoshwa, uwezo wa kimaadili
ulichafuliwa. Mungu alikuwa amemwita Samsoni kwa wadhifa wa jukumu
kubwa, heshima, na manufaa; ila kwanza angalipaswa kujua uongozi kwa kujifunza utii kwa sheria za Mungu.
👉🏼Yusufu
alikuwa mtu huru mwenye maamuzi huru. Mema na mabaya yalikuwa mbele
yake. Angaliweza kuchagua njia ya usafi, utakatifu, heshima, au njia ya
uasherati na vitendo vya aibu. Alichagua njia sahihi, naye Mungu
alitukuzwa. Samsoni, chini ya majaribu ya jinsi iyo hiyo, ambayo
alijisababishia yeye mwenyewe, alijiachia akatekwa na tamaa mbaya. Njia
aliyoichagua ilimfanya aishie kwenye aibu, majanga, na hatimaye kifo.
Kuna utofauti gani ukilinganisha na maisha ya Yusufu.
👉🏼BWANA
katika Neno lake alikuwa ameweka wazi kuwa watu wake hawapaswi
kujifungamanisha na wale wasiompenda au kumcha. Watu wa jinsi hiyo
hawataridhika kupewa heshima na upendo ule waustahilio pekee. Bali
watadumu kutafuta kupata kutoka kwa mke au mume mcha Mungu upendeleo
maalumu utakaohusika kupotoka na kuyaacha mapenzi ya Mungu.
👉🏼Kwa
mwanamume mcha Mungu, na kwa kanisa alilojifungamanisha nalo, mke au
rafiki wa kidunia ni mpelelezi kwenye kambi hiyo, ambaye atakuwa
akitafuta daima kila fursa kusaliti mtumishi wa Kristo, na kumfichua kwa
mashambulizi ya adui.
👉🏼Historia
ya Samsoni hutoa fundisho kwa wale ambao tabia zao hazijaundwa, ambao
hawajaingia kwenye jukwaa la maisha ya shughuli. Vijana wanaoingia
kwenye shule zetu na vyuo watapata kila darasa la kuulisha ubongo. Iwapo
wanatamani michezo na mizaha; iwapo wanachagua kuacha mema na
kukumbatia uovu, wanayo fursa hiyo. Dhambi na utakatifu vipo mbele yao,
na uchaguzi ni wao. Ila hebu wakumbuke kuwa “Kile mtu apandacho, ndicho
atakachovuna.”
No comments:
Post a Comment