π“Ndipo
huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa
Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo
kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.” Waamuzi 13:8.
πMungu
mwenyewe alimtokea mkewe manoa na kumwambia kuwa atakuwa na mtoto
mwanamume, na kwamba atakuwa mtu mkubwa atakayekomboa Israeli. Kisha
akampatia maelekezo kamili kuhusu namna atakavyomlisha. Hebu tuuchukulie
ujumbe huu kama unaotolewa maalumu kwa kila
mama hapa duniani. Iwapo unataka watoto wako wawe na akili safi na
bora, yakupasa uwe na kiasi katika mambo yote. Hakikisha moyo wako ni
safi na akili yako ni timamu, ili kurithisha uzao wako afya bora ya
kiakili na kimwili.
πKila
mama anapaswa kulijua jukumu lake. Apate kujua kuwa tabia ya watoto
wake itategemea zaidi mno tabia yake kabla na baada ya kuwazaa, kuliko
ilivyo mivuto mingine ya nje iwe mizuri au mibaya. Mama aliye mwalimu
bora kwa watoto wake, sharti kabla ya kuwazaa, adumishe mazoea ya
kujikana nafsi na kujitawala; kwani huwarithisha sifa zake binafsi za
kitabia, ziwe nzuri au dhaifu.
πWashauri
wasiofaa huwahimiza wakina mama umuhimu wa kukidhi kila tamaa na uchu
wa chakula, ila ushauri huo ni potofu. Mama kwa agizo la Mungu ameagizwa
kudhihirisha kiwango cha juu cha kujitawala. Na akina baba na akina
mama wapaswa kujumuika pamoja katika jukumu hili. Wazazi wote wawili,
hurithisha tabia zao kwa watoto wao, kiakili, kimwili, kimwenendo na
kishauku yao ya ulaji.
πWengi
huchukulia kimzaha somo la kiasi. Hujidanganya kuwa BWANA hajihusishi
na mambo madogo madogo kama vile kula na kunywa. Ila endapo Mungu
hajihusishi, mbona akajifunua kwa mkewe Manoa, akitoa maelekezo kamili,
akimsisitiza mara mbili awe mwangalifu kutokuyapuuzia.
πWazazi
wengi huchukulia madhara ya mivuto ya kipindi kabla ya mtoto kuzaliwa
ni jambo dogo la kupuuziwa; ila mbingu hazichukulii hivyo. . . . Kwa
maneno yaliyoongelewa kwa mama huyu wa Kiebrania, Mungu huongea kwa
wakina mama wote wa zama zote.
No comments:
Post a Comment