MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU.
KWA NINI MUNGU MWANA
YAANI YESU KRISTO ALIKUFA MSALABANI NA SIYO MUNGU BABA AU MUNGU ROHO
MTAKATIFU?
1. Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni baraza uumbaji
ambalo liliamua Mungu Mwana yaani Yesu Kristo awe msemaji na Mtendaji
mkuu. Yohana 1:1-3, 14 "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako
kwa Mungu.
Vyote vilifanyika kwa huyo: wala pasipo yeye hakukufanyika
cho chote kilichofanyika... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu:
nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa
Baba: amejaa neema na kweli. "
Wakolosai 1:14-20 "... ambaye katika
yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi: naye ni mfano wa Mungu
asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye
vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana: ikiwa ni viti vya enzi, au usultani,
au enzi, au mamlaka: vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili
yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana
katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa: naye ni
mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi
katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae: na kwa
yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake, akisha kufanya amani kwa
damu ya msalaba wake:kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au
vilivyo mbinguni.".
Yesu ndiye aliyemwambia Adamu, "walakini matunda
ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula
matunda ya mti huo utakufa hakika". Ndiyo sababu Yesu anaitwa Neno.
Msemaji mkuu wa serikali ya mbinguni.
Yesu alikufa msalabani kwa niaba ya mwanadamu. Kwa kuwa ndiye aliyesema 'utakufa hakika'. Kama asingekufa na wanadamu wasamehewe basi shetani angedai kuwa Mungu ni mwongo. Ndiyo maana neema na haki zilibusiana msalabani. Yaani neema mwanadamu asamehewe dhambi alipotenda. Haki mwanadamu atii amri na maagizo ya Mungu baada ya kusamehewa dhambi. Yesu alikufa msalabani ili kumtetea mwanadamu asife na pia kutetea maagizo au amri zake zisipuuzwe. Ndiyo maana mtu anapoasi anamrudisha Yesu msalabani.

Waebrania 6:4-6 "Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja
kipawa cha mbinguni, na kufanywa wahirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja
neno zuri la Mungu, na nguvu... Kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu
mara ya pili...".
No comments:
Post a Comment