“Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie
asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe.”
Waamuzi 16:6.
Waisraeli walimweka Samsoni kuwa Mwamuzi juu yao,
naye alitawala juu ya Israeli kwa miaka ishirini. Ila kosa moja hufungua
njia kwa kosa jingine. Alivutiwa na mihemko ya kianasa iliyomwongoza
kwenye anguko. “Alimpenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki,” siyo
mbali sana na nyumbani kwao. Jina la mwanamke huyo alikuwa Delila,
“mwangamizi.” Wafilisti walitazama kwa
makini mwenendo wa huyu adui yao, na alipojidhalilisha mwenyewe kwa
kujifungamanisha na mwanamke huyu wa Kifilisti, walinuia, kupitia
Delila, kukamilisha mpango wa kumwangamiza.
Jopo la watu wa heshima lenye kuundwa na mtu mmoja mmoja toka kila
jimbo la Wafilisti walisafiri hadi bonde la Soreki. Hawakuthubutu
kumshambulia akiwa anamiliki hazina ya nguvu zake tele, bali ilikuwa ni
mpango wao kujifunza, ikiwezekana, siri ya nguvu zake. Hivyo walimhonga
Delila atafute siri ya nguvu za Samsoni kisha awafunulie.
Kadiri
msaliti alivyomsonga Samsoni kwa maswali, alimdhihaki kwa kumwambia
nguvu zake zaweza kutoweka, awe sawa na watu wengine dhaifu, iwapo mambo
fulani yatatendeka. Kila aliloambiwa alijaribisha, ila akagundua ni
uongo kwani nguvu zake hazikutoweka. Kisha akamlilia akisema, “Mbona
umenidanganya mara zote hizi, ukisema wanipenda, na roho yako haipo
pamoja nami?” . . . Mara tatu Samsoni ameona ushahidi dhahiri kuwa
Wafilisti wamepanga njama kumwangamiza kupitia huyu mpenzi wake; ila
pale mpango huo ulipoonekana kukwama; mwanamke huyo alilia sana akidai
amemhadaa, hampendi, naye mumewe akapumbazika asitambue hatari iliyoko
mbele yake.
Mwamuzi huyu wa Israeli alitumia saa nyingi mbele ya
mwanamke huyu mlaghai, saa ambazo angalizitumia kwa mafanikio na
maendeleo ya watu wake. Tamaa hizi zenye kupofusha ziwezazo kumfanya
shujaa aonekane dhaifu kabisa, zilikuwa zimeshamtawala akili na dhamiri.
Ukengeufu wa Samsoni ulikuwa taratibu na wa hakika. Mwanzoni
hakudhamiria kufunua siri, ila kwa hiari amejitosa mwenyewe ndani ya
wavu wa msaliti wa roho, na kamba zangu zilikuwa zikimsonga kutoka kila
upande.
No comments:
Post a Comment