HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI!
Fungu la tafakari: “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea
Utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliye viumba vitu vyote,
na kwa sababu ya mapenzi yako
vilikuwako, navyo vikaumbwa.” Ufunuo 4:11.
Makusudi
ya somo hili: Kujifunza ni nani
aliumba ulimwengu na uliumbwa kwa nanna
gani.
UTANGULIZI…
Ingawa
wana sayansi wengine hujaribu kueleza kwamba Mungu hakuumba binadamu na dunia,
Biblia hutufundisha kwamba “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbigu na nchi” (Mwanzo
1:1) na kwamba binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Katika somo
la leo tutajifunza ukweli huo na kuona kuwa dunia na vyote vilivyomo
havikutokea kwa njia ya mabadiliko ya polepole ya vitu asilia, Bali “ kwa Neno la Bwana” Zaburi 33:6.
Utatu
Mtakatifu ulihusika kikamilifu katika Uumbaji wa ulimwengu huu. Mwanzo
1:1,2,26; Yohana 1:1-3; Waebrania 1:2.
Biblia
hufundisha kuwa Umoja wa nafsi tatu za milele ulishirikiana kuanzisha historia
ya mwanzo wa binadamu na ulimwengu. Mungu Mwana (Kristo) alikuwa ndiye wakala
nkuu wa uumbaji, sababu hakuna kiumbe chochote kilichoumbwa pasipo yeye. Mungu
Roho Mtakatifu alikuwa na sehemu ya kufanya.
Kwa neno la
Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake
lote kwa pumzi ya kinywa
chake. Zaburi 33:6-9;
Kwa imani
twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu
vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Ebrania 11:3.
Neno la Mungu
halikuwa tu na nguvu ya kuumba ulimwengu, bali lina nguvu pia ya kuutegemeza
(Waebrania 1:3)
Maana Bwana,
aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na
kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na
watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. Isaya 45:18; Zaburi 19:1-4.
Siku
sita za Uumbaji:
Siku ya 1: Mungu aliamurisha
mwanga kuwepo kwa kutenganisha nuru na giza. Hii ndiyo asili ya kuwepo mchana
na usiku. Mwanzo 1:2-5.
Siku ya 2: Mungu aliamuru
anga kuwepo kwa kuyatenganisha maji. Mwanzo 6:6-8.
Siku ya 3: Mungu aliamuru
nchi kavu, bahari, miti, mimea na majani kuwepo. Mwanzo 1:9-13.
Siku ya 4: Mianga mitatu
(Jua, Mwezi na Nyota) viliamrishwa kuwepo. Mwanzo 1:14-19.
Siku ya 5: Ndege , Samaki
na wanyama wa baharini na ziwani pamoja na viumbe wengine wanaoishi majini
waliamrishwa kuwepo. Mwanzo 1:20-23.
Siku ya 6: Wanyama wa
kufugwa, wanyama wa porini na vyote vitambaavyo juu ya nchi viliwekwa. Binadamu
aliumbwa siku hiyo pia. Mwanzo 1:24-27.
Siku sita za uumbaji zilikuwa siku halisi kabisa, kila
siku ikiwa na saa 24.
Siku hizi hazikuwa mifano ya kuwakilisha maelfu au
mamilion ya miaka, kama wengine wanavyofikiri.
Baada ya siku sita za uumbaji kumalizika tunaona siku
nyingine ya muhimu sana na ndiyo chimbuko la ibada zote duniani. Maana tumeubwa
tukiwa na asili ya kuabudu ndani yetu. Haijarishi unaabuni nini, ama unamwabudu
nani. Lakini makusudi ya Mungu anataka tumwabudu yeye peke yake.
Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote
aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote
aliyoifanya.
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu
katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na
kuifanya.
Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.
Mwanzo 2:1-4.
HIVI NDIVYO MIMI NA WEWE TULIVYOUMBWA NA MUUMBAJI WETU
NA VYOTE VINAVYO ONEKANA. NA SI VINGINEVYO. NDO UKWELI WA MAANDIKO MATAKATIFU
(BIBLIA).
AHASANTE KUWA PAMOJA NAMI KATIKA SOMO HILI.
No comments:
Post a Comment