KITABU CHA MAAJABU
KUNAVITABU VINGI HUMU DUNIANI LAKINI HIKI NI YOTE KATIKA VYOTE.
Fungu la
tafakari:- Majani yakauka au lanyauka, bali neno la Mungu wetu litasimama
milele.” Isaya 40:8
Kusudi la somo hili:- Kuonesha kuwa Neno la Mungu
lililoandikwa – Biblia, ni ufunuo wa Mungu kwa wanadamu.
UTANGULIZI:
Tunaye Mungu mmoja wa kweli aishie milele. Amejtambulisha
kwa wanadamu kwa kuangalia kazi zake alizozifanya.
Tena tunazo
njia za maana ambazo kwazo tunaweza kumfahamu kama fundisho hili
linavyofundisha.
Je, Biblia
inatambuliwaje na waandishi wake? Warumi 1:2; 2Timotheo 3:15
Inatambuliwa
kama mafundisho au maandiko. Maana ya “Maandiko” ni Neno la Mungu.
Mungu ndiye
aliyeongoza kazi yote ya uandishi, maana watu walinena yaliyotoka kwa Mungu
wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 2Petro 1:21
Maandiko
haya yalitolewa na Mungu ili kutuonya sisi na kutuadibisha katika haki.
2Timotheo
3:16.
Watakatifu
wa Mungu, waliohusika katika uandishi wa Biblia walitoka katika taifa la
Kiebrania, taifa lililo chaguliwa na Mungu, kumwakilisha katika ulimwengu huu.
Mungu
hakuwaacha waandike kwa kutegemea utashi wao pekee isipokuwa aliwaongoza
kuandika kama alivyopenda.
Mungu ndiye
aliyesema na manabii.. Ebrania 1:1; Ufunuo 1:1.
Wao
walikuwa ni vyombo vya kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu.
Roho wa
Mungu alinena na Manabii, nao wakayandika. Matendo 1:16; 2Samweli 23:2.
Kwa nini ni
ktabu cha maajabu.
Watu
arobaini waliandika Biblia. Na waliishi miaka 4000 iliyopita... Kunamaneno
yaliyoandikwa na wafalme, wana wa kifalme, watunga mashahiri, wenye hekima,
wenye elimu ya rugha, wavuvi, wenye maarifa ya utawala. Watu waliojifunza elimu
ya Misri,
Walioelimishwa
katika skuli ya Babeli, waliofundishwa mjini Yerusalemi. Liliandikwa na watu waliohamishiwa mbali kutoka kwao, katika
mjangwa, katika mahema ya wachungaji, katika malisho ya kijani. Mbali na haya
miongoni mwa wandishi tunaona wakusanyaji wa kodi, Wachungaji, wakusanyaji wa
matunda, watu maskini, watu matajiri, watawala, wahubiri, majaji, watu wakila
dalaja na wakila darasa wanakuwa mawakili wake katika ullimwengu huu. Biblia
inayo kila namna ya maandiko, ni michanganyiko inayotengeneza idadi ya vitabu
66 vilivyoandikwa kwa watu wa kawaida.
Ajabu kubwa
zaidi; wandishi wa Biblia hawakukaa nchi moja ama sehemu moja, lakini maandishi
yao yalipounganishwa yakaoana, yakalingana kana kwamba yameandikwa na mtu
mmoja. Huo ni utendaji mkuu wa Mungu mwenyewe.
Maandiko,
yanatuhekimisha hata tunapata wokovu, 2Timotheo 3:15
Neno la
Mungu linabadili na kugeuza mioyo yetu linaukali kuliko upanga ukatao kuwili.
Hakuna
aliyekuja kwa Yesu akabaki kama mwanzo, lazima neno limbadilishe. Ebrania 4:12.
Kunauwezo
unaoelimisha, Biblia haina mpinzani, katika Neno la Mungu akili hukutana na
somo lenye hoja za kina, kirefu, matamanio ya juu. Biblia ni historia yenye
mafundisho ambayo wanadamu wakiyafuata wanapata uzima. Ilikuwa safi kutoka
kwenye chemichemi ya kweli yenye uzima, na mkono wa Mungu umeuhifadhi usafi
wake katika katika zama zote.
Katika neno
la Mungu tunauona uwezo ule ulioiweka misingi ya dunia na kuzitandaza mbingu.
Hapa matatizo makubwa ya uwajibikaji, na hatima ya badaye yanafunuliwa.
Katika kutafakari kwa kicho ukweli kama ulivyoelezwa
katika neno lake, mawazo ya mwanafunzi yanakutana na akili asiyo na kikomo
katika ushirika wa karibu. Kujifunza kwa namna hiyo hakukuzi tu na kuboresha
tabia, bali pia kutapanua na kuhamasisha nguvu za kiakili.
Tunasafisha
njia zetu kwa kutii na kufuata neno lake, Zaburi 119:9,15.
NENO LA
MUNGU LADUMU MILELE ISAYA 40:8
WITO TUSOME
NENO LA MUNGU NA KUTII.
No comments:
Post a Comment