KUMFAHAMU MUNGU WETU NI JMBO LA MSINGI SANA: KARIBU KATIKA SOMO HILI.
Fungu
la tafakari: “Bali BWANA ndiye Mungu wa Kweli; Ndiye Mungu aliye
hai, Mfalme wa milele.” Yeremia 10:10.
Makusudi
ya somo hili: Ni kufahamu kuwa tunaye Mungu mmoja na kuwa si kama
mifano inayofanywa na mwanadamu.
UTANGULIZI..
Mungu ni nini? Na ni nani? Hili ni swali la msingi kabisa unaloweza
kuuliza. Majibu kwa maswali muhimu maishani mwako hupatikana kwa kutegemea
unamwelewaje Mungu. Fikira zako juu ya Mungu zinaathiri mtazamo wako wa kila
jambo; muhimu zaidi, ni namna unavyojitazama. Maisha yanathamani yoyote? Kuna
sababu ya kuhangaika leo? Je, lipo tumaini la kesho? Bila shaka, utambuzi wako
wa Mungu utapelekea kupata majibu kwa maswali haya, na kupata mengine zaidi.
Ikiwa ni muhimu kiasi hicho kuwa na maarifa sahihi ya Mungu, unawezaje
kumfahamu Mungu.
Je, inawezekana kwa mwanadamu kumjua Mungu?
Ndiyo, inawezekana
kabisa. Yohana 17:3, Na uzima wa milele ndio huu,
Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Tutapata uzima wa milele ikiwa tayari tunao ufahamu kamili wa huyu
tunaye mtumikia (Mungu) na Kristo Mwokozi wetu.
Yesu alikuja.....”naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa
kweli,.... huyu ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele. 1Yohana 5:20.
Tukimwamini Yesu tutamjua na Baba, maana atatufunulia Mathayo 11:27.
1Wakorintho 1:21.
Kumjua Mungu hakupatikani kwa kutegemea ubongo wa mwanadamu bali moyo
wa mwanadamu. Ujuzi wa mambo ya kidunia hutegemea uwezo wa wa kiakili wa mtu,
lakini kumfahamu Mungu hakutafutiki kwa njia za kibinadamu. Kutumia akili za
kibinadamu kujaribu kumjua Mungu
kunafananishwa na kujaribu kutumia tochi kulichunguza jua, jambo
lisilowezekana kabisa.
Wasioamini hawawezi kabisa kumjua Mungu. Ujuzi wa Mungu unapatikana pale
mtu anapoamini na kufanyia kazi kila ujuzi anaoupata. (Yohana 7:17).
Hakuna mawazo ya mwanadamu
yanayoweza kumtambua Mungu. Hebu mwanadamu dhaifu na mwenye ukomo asijaribu
kumtafsiri au kubashiri habari za Mungu. ... Mwenye maarifa yote hajadiliwi.
Kadri tunavyojifunza zaidi na zaidi jinsi Mungu alivyo, na jinsi
sisi wenyewe tulivyo mbele zake,
tutaweza kuogopa na kutetemeka mbele
zake. 8T. Uk, 283
Kama kila kilichoko duniani kina msanii basi hata ulimwengu huu na vyote
vilivyomo kunamsanii aliye sanifu. Zaburi 19:1, Na vyote vinatangaza utukufu
wake, na nikazi ya mikono yake.
Warumi 1:20; Zaburi 14:1; Warumi 1:18-22,28.
Viumbe vya asili na Maandiko matakatifu ni vyanzo vikubwa viwili vya
ushahidi wa uwepo wa Mungu.
Unaweza ukawa unajiuliza maswali mengi kuhusu Mungu, maana kuna Yesu, na
Roho Mtakatifu, je, kuna Mungu watatu
mbinguni? Swali la msingi sana hili.
Maelezo: Maandiko Matakatifu yanasisitiza juu ya kuwepo kwa Mungu
Mmoja; Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele. Katika
mashirika ya kibinadamu madaraka ya mwisho huwa juu ya mtu mmoja – Raisi,
Mfalme, au Waziri mkuu.
Katika Utatu Mtakatifu, madaraka ya mwisho yapo kwa wote Watatu. Pamoja
na kwamba Utatu Mtakatifu si nafsi moja, Mungu ni mmoja. Umoja huu hauondoi
nafsi tatu huru zinazojitegemea za Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Na pia
utofauti wa nafsi Uungu haziharibu mkazo wa maandiko matakatifu kwamba Baba,
Mwana, na Roho Mtakatifu ni Mungu Mmoja.
Torati 6:4; Waefeso 4:4-6; Mwanzo 1:26;3:22;11:7; Isaya 48:16; Yohana
14:16.
Majina
ya Mungu:
(a) El na Elohim, yaani ‘Mungu’ Jina hili
huonyesha nguvu ya kiungu ya Mungu. Humuonyesha Mungu kuwa mwenye nguvu na
Muumbaji (Mwanzo1:1; Kutoka 20:2; Daniel 9:4)
(b) Elyon, yaani ‘Aliye juu sana’ na El Elyon, yaani ‘Mungu
Aliye juu sana’ Jina hili huelezea jinsi alivyotukukuka. (Mwanzo 14:18-20; na
Isaya 14:14)
(c) Adonai, yaani ‘Bwana’ Jina hili humwelezea Mungu kama Mtawala
Mwenye Enzi (Isaya 6:1; Zaburi 35:23)
Yako majini mengine ambayo huonyesha utayari wa Mungu wa kufanya urafiki
na watu wake. Majina hayo ni pamoja na Shaddai, yaani ‘Mwnyezi’ na El
Shaddai. Yaani ‘Mungu Mwenyezi’ Jina hili humwelezea Mungu Mwenyezi
kuwa ni chanzo cha baraka na faraja (Isaya 6:3; Zaburi 91:1). Jina jingine ni Yahweh,
ambalo hufasiliwa kama Yehovah au BWANA, ambalo husisitiza
uaminifu na neema za agano la Mungu. (Kutoka 15:2; Hosea 12:5,6)
Kuna mabo mengi kumhusu Muumbaji wetu hata vitabu havitoshi kuelezea,
kulingana na akili zetu finyu zilizoathiriwa kwa kiwango kikubwa na dhambi,
kwaleo tuishie hapa. Natumai somo hili limekutoa sehemu moja na kukusogeza
sehemu nyingine karibu na Mungu wetu.
WITO: KWA MUNGU YOTE
YANAWEZEKANA (MATHAYO19:26).
No comments:
Post a Comment