Sehemu ya 3
Shetani ndiye
aliyeleta taabu kwa sayari hii na ndiye ambaye amekuwa akisababisha dhambi na
mateso tangu hapo. Yesu alimfichua mwovu na jinsi anvyotesa watu.
Siku zote yeye
amekuwa akiwafunga watu kwa magonjwa ya ajabu na ajali vita majanga ya kila
namna Shetani ndiye kiongozi.
Katika Biblia
tunaona kisa cha mwanamke aliyefungwa na Shetani miaka 18, Yesu alibainisha
kuwa amefungwa na shetani, yampasa kufunguliwa. Yesu akamponya yule mwanamke.
Luka 13:16
Pengine hakuna
mahali katika Biblia tuwezapo kuona mkakati wa Shetani kwa wazi zaidi kuliko ulivyo
fichuliwa katika sura ya kwanza ya kitabu cha Ayubu, katika mazungumzo kati ya
mwovu na Mungu.
Ilikuwa wakati
fulani baada ya kuanguka kwa Shetani kwamba wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha
mbele za Bwana. Shetani naye
akaenda kati yao.! Fikiria
hili! Mkutano wa wana wa Mungu, na Shetani akaja bila kualikwa! (Fungu:
Ayubu 1:7)
BWANA akamwuliza Shetani, 'Umetoka wapi
wewe?' ! Ayubu 1:7
Kwa maneno mengine,ni nani aliyekualika? Una
haki
gani ya kuwa hapa? Ndipo Shetani akamjibu
Bwana, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
Ayubu 1:7 Shetani alidai
miliki juu ya Sayari Dunia.
Alikuwaamenyakua
nafasi ya Adamu! Adamu anaitwa mwana wa Mungu (Angalia Luka 3:38), kama tu wale
wengine waliokuja siku ile kwa ajili ya mkutano na Mungu.
Je, yawezekana ya
kwamba walikuwa ni viongozi wa dunia zingine, kama jinsi ambavyo Adamu alikuwa awali
kiongozi wa ulimwengu wetu?! Kwa vyovyote vile, dai la Shetani la kuwakilisha
Dunia halikupita bila kupingwa. Bwana akamwuliza Shetani; (Fungu: Ayubu
1:8,9,11) ..... 'Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? kwa kuwa hapana
mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uwelekevu, mwenye kumcha Mungu
na kuepukana na uovu?
Ndipo Shetani
akamjibu BWANA, na kusema, Je, huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
Lakini nyosha mkono
wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako'
Ni changamoto kubwa
kiasi gani! Siku hiyo Shetani alidai ya kwamba sababu pekee ambayo kwayo Ayubu
alimtii Mungu ilikuwa ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu alimtendea, na si kwa
sababu alimpenda na kumtumaini Mungu. (Fungu: Ayubu 1:12)
BWANA akamwambia
Shetani,' Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono
wako juu yake mwenyewe.'Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA. Ayubu 1:12.
Shetani aliondoka, akiwa na shauku ya kutia mikono yake katika mali ya Ayubu.
Mara mapigo yakaanza
kuanguka: Kwanza: Waseba wakaiba ng'ombe wa Ayubu na kuwaua wafanyakazi wake.
Pili: Radi ikapiga,
na kua kondoo wake na wachungaji wake.
Tatu: Wakaldayo walikuja
na kuteka nyara ngamia wa Ayubu.
Nne (habari ya
kuvunja moyo mno): kimbunga kiliipiga nyumba ya kijana mkubwa wa Ayubu. Karamu
ilikuwa ikiendelea, na watoto wote kumi wa
Ayubu waliokuwemo wakauawa
Maskini Ayubu
alidhani kwamba Bwana alikuwa amechukua mali yake na kusababisha msiba wote huo.
Hakuelewa ya kwamba mwovu ndiye alikuwa ametenda hiyo Hata ingawa alizidiwa na
huzuni, uaminifu wa Ayubu kwa Mungu haukubadilika.
Akasema, ....BWANA
alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Ayubu 1:21
Ingawa hakuelewa
misiba iliyoangamiza mali zake na watoto, Ayubu alidumu tu kutumaini wema wa Mungu.
Lakini Shetani alikuwa hajamaliza. Akampa Mungu changamoto tena akisema, Ayubu
2:4-6
...Naam, yote aliyo
nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
BWANA akamwambia
Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Ayubu
2:4-6.
Lakini sasa nyosha
mkono wako,uuguse mfupa wake na nyama yake,naye atakufuru mbele za uso wako.
Jaribu lilikuwa
tayari limeanza Je, Ayubu angesalia kuwa mwaminifu kwa Mungu wakati makali yatakapozidi
kuwa makali, ama atamwacha Mungu?
Basi Shetani akatoka
mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata
utosi wa kichwa. Ayubu 2:7.
Kama umewahi kupata
na jipu, unajua jinsi ambavyo jipu moja tu linavyoweza kuuma.Fikiria sasa
kitendo cha kufunikwa na majipu toka utosini hadi wayo wa mguuni.
Hata ingawaje
Shetani alikuwa amempokonya Ayubu mali yake, watoto wake, na afya yake, Ayubu alisalia
mwaminifu kwa Mungu. Mtu wa namna gani huyu! Biblia inasema, Katika mambo hayo
yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu. Ayubu 1:22.
Ni nani aliyemuumiza Ayubu? Ni nani aliyemletea mapigo Ayubu?
NI SHETANI.
Ni nani aliyeiba mifugo yake na kuua
watumishi wake? Ni SHETANI!
Ni nani aliyeleta kimbunga kilichoteketeza
wana na binti zake! Ni SHETANI.
Bwana anaweza kuruhusu matatizo yaje ili
kujaribu utii na upendo wetu, bali SHETANI ndiye mwenye hatia kwa ajili ya uovu
wote uliopo kwenye Sayari Dunia!
No comments:
Post a Comment