Sehemu ya mwisho.
Wewe nami tumekutwa
katikati ya pambano linalochanganya la ulimwengu, ugomvi kati ya mamlaka na
uasi, kati ya Muumbaji na Shetani, muasi wa kwanza.! Sisi si watazamaji.
Tunahusika, tupende tusipende.
Dhana kwamba Shetani
ni hadithi tu ama mvuto fulani tu, hutuacha tukiwa hatukujiandaa kabisa kukabiliana
na kiumbe mwenye akili kama alivyo.
Kitabu cha Ufunuo
kinasema: Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na
bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya
kuwa ana wakati mchache tu.! Ufunuo 12:12.
Kwa sababu hiyo,
furahini enyi mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, ole wenu nchi na bahari,
maana Ibilisi amewajieni akiwa na ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba siku
zake zilizobakia ni chache.
Petro aliandika onyo
hili: Muwe na kiasi na kukesha kwa adui, Ibilisi, mshitaki wenu kama simba
angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ammeze. akitafuta mtu ammeze. 1 Petro
5:8.
Lakini hata ingawa
Shetani hutenda ubaya zaidi, Mungu wa uumbaji anao mpango wa kuumba upya ambao
umjumuisha Mwana wake Yesu- Mwana wake wa thamani aliyekuwa hiari kufa ili
kulipa deni letu ili tuwe na uzima wa milele.
Shetani alitenda
kazi kupitia kwa Mfalme Herode ili kumuangamiza mtoto Kristo (Akashindwa).
Shetani alikuja kwa
Yesu jangwani, akijifanya kuwa malaika kutoka mbinguni akiwa na majaribu makuu
matatu (Akashindwa).
Shetani alichochea
halaiki ya watu ili wamwangamize Yesu pale Kalvari (Alikuwa adui aliyeshindwa
milele).
Ingawa kulikuwa na Kalvari,
kulikuwa pia na ufufuo! Mungu Asifiwe!!
Hivyo ndivyo
ilivyokuwa ya kwamba Mungu alimtoa Mwanae; na Mwana akajitoa mwenyewe, ili kubatilisha
hatima yako na yangu.! Ilikuwa ni saa ya ushindi, siku ya kutamka uhuru kwa
ajili ya wafungwa wote wa mwovu katika Sayari Dunia.
Siku hiyo Shetani
akawa adui aliyeshindwa! Kristo kwa mauti yake akapata haki ya kuangamiza uovu wote
na mateso.! Paulo aliandika katika Waebrania 2:14: Basi, kwa kuwa watoto
wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo ili kwa
njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi.
Shetani
alidhihihirisha mbele ya wenye ufahamu wote wa ulimwengu kuwa yeye ni kiumbe wa
jinsi gani. Na bado anaendelea kudhihirisha jinsi ambavyo angeuendesha
ulimwengu.! Vimbunga, matetemeko, mafuriko, uhalifu, maradhi, huzuni, na
maumivu!! Haya tunayaona Lakini nguvu isimamayo nyuma ya yote haya bila kuonekana
kwa macho ni ile kazi ya Shetani ipitayo akili ya mwanadamu.
Waweza kuwa
unashangaa juu ya masikitiko, huzuni, na matatizo katika maisha yako binafsi. Waweza
kuwa unashangaa juu ya kifo cha mtoto ama mpendwa na kuuliza Yu wapi Mungu?
Biblia inafundisha
ya kuwa Mungu yupo. Yupo katikati ya huzuni zako masikitiko, na matatizo.! Na
atakuja muda si kitambo kushughulikia tatizo la dhambi na mateso.
Habari njema ni kwamba
sayari hii nzuri, iliyotekwa na Shetani, i karibu kuokolewa.! Ufahamu huu
wapaswa kunyamazisha hofu za abiria wenye shauku, juu ya sayari inayokwenda
kombo!! Mungu anao mpango wa kumwangamiza Shetani-- mwovu mdanganyifu.
Hebu tuone kile
ambacho Biblia inasema juu ya Shetani: .....Nami nimekuangamiza, Ewe kerubi
ufunikaye....... Basi nimetokeza moto kutoka ndani yako; nao umekuteketeza,
nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi... Ezekieli 28:16,18! Dhambi na taabu
vitapotea milele.
Ndiyo, rafiki, Yesu
anakuja upesi! Siyo kama mtu wa chini wa Galilaya, siyo kama aliyetukanwa,
aliyetemewa mate, na aliyekataliwa. Siyo kama mtu anayening'inia msalabani, bali
kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana akiwa na haki ya kutawala! Lazima
tuwe tayari kukutana naye maana kama tukikosa hilo, tumekosa kila kitu
Utii wako uko wapi? Swala
leo ni, Ni nani tutakayemwamini? Ni nani tutakayemfuata? Mungu mwenye upendo
-au malaika aliyeanguka?
Mistari inachorwa; Ulimwengu nzima unagawanywa katika sehemu
mbili. Wewe uko
upande wa nani?
Kwa kila moyo usiotulia,
moyo mpweke, kwa kila roho inayoumia, yenye hatia, kwa watoto wake wote katika
sayari dunia iliyo katika uasi, Yesu anatoa mwaliko wa upendo:
Njoni kwangu ninyi
nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Wote anipao
Baba watakuja kwangu; ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe! Yohana
6:37 Je, hii si habari ya
ajabu? Mathayo 11:28.
Katikati ya misiba ya maisha, simanzi,
huzuni na kukata tamaa, Yesu yuko hapo.! Anaelewa simanzi uliyo nayo sasa hivi.
Yesu anaelewa unachokipitia mwili wako unaporaruliwa na ugonjwa. Anajua
maumivu. Aliyapitia wakati watu wakatili walipopigilia misumari yenye kukwaruza
katika mikono Yake. Anajua upweke Aliupitia wakati aliponing'inia peke yake
katika giza
msalabani. Anajua umaskini.
Aliupitia alipotembea
katika barabara zenye vumbi za Palestina akiwa na chakula kidogo tu huku akiwa hana
mahali pa kupaita nyumbani.
Njoo kwake leo.
Atakupatia tumaini
jipya na moyo mkuu. Hapa kuna habari nzuri kuliko zote. Siku moja hivi karibuni
Yesu huyu atakuja tena na kukomesha taabu zote za maisha. Atakuja tena
kuanzisha ulimwengu mpya. Dhambi na wadhambi
wataangamizwa. Hatimaye Shetani, atashindwa kwa ujumla kabisa. Yesu anatamani
kukurejesha wewe kwa familia ya Mungu, kukupatia wewe uzima wa milele kwenye
sayari iliyofanywa mpya.
Lakini uamuzi lazima
ufanyike--Ni nani atakayekuwa Mkuu na Bwana wako ?
Rafiki, uamuzi huu
ni swala la kufa na kupona Je, hutachagua sasa hivi kumruhusu Kristo awe Mfalme
wako? Anasubiri. Mikono yake imefunguliwa wazi. Anasema, Njoo! Njoo! Njoo!!
Je, waweza
kuinamisha kichwa chako tunaposali na kusema, Naam, Yesu, ninakuja.
AHSANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI KATIKA MFULULIZO WA MASOMO HAYA.
***MWISHO***
No comments:
Post a Comment