Yawezekanaje
Mungu wa upendo akayaruhusu?
SEHEMU YA 1.
Clara Anderson
alikuwa mjakazi jijini San Francisco, na Clara alikuwa mwanamke muungwana sana
- na pia mwaminifu sana.! Siku moja baada ya kuwa mtendakazi kwa muajiri mmoja
kwa miaka 15, alitoweka.! Muajiri wake hakujua alipokwenda. Alikuwa tu kama aliyetokomea
toka machoni pa watu.! Kisha kwa namna ya ajabu, baada ya siku za kutafuta,
idara ya jiji ya ustawi wa jamii ikampata.! Clara alikuwa katika mpango wa
'mgomo wa kula hadi kufa' katika kificho cha mlima nje ya San Fransisco.
Akasema, Nataka kufa. Niacheni. Wakati mwandishi wa habari aliyemkuta
alipomhoji, Clara
alisema,! Tazama ,
hakuna anayenijali. Mimi ni kijakazi tu - mmoja tu kati ya maelfu katika jamii
watendao kazi za kinyonge. Maisha yangu hayana thamani. Sina ndugu wa karibu,
sina jamaa, sina marafiki. Mimi ni mpweke kiasi kwamba sihitaji kuishi. Hakuna
ninaye mdhani kuwa wa karibu nami - sina niwezaye kuzungumza naye, hayupo
niwezaye kufungua moyo wangu kwake. Hivyo niacheni tu nife, kwa sababu hakuna
kwa kweli anayejali.
Hakuna anayejali!
ndicho kilio cha wanaume na wanawake katika sayari iliyo pweke.!
Hivi karibuni katika
utafiti kuhusu Mungu, watu waliulizwa, Kama ungemuuliza Mungu swali moja, hilo
swali lingelikuwa lipi?!
Vipi wewe? Kama ungemuuliza Mungu swali moja, lingelikuwa lipi? Tazama
jinsi ambavyo mamilioni wangeuliza:! Mungu , je, kweli unanijali? Kama wewe ni
mwema hivyo, kwa nini kuna maradhi mengi kiasi hiki? Mbona mahangaiko na mauti
duniani?! Mbona kuna kuvunjika moyo hivi na huzuni?! Mbona kuna njaa, mafuriko,
maafa yatokanayo na nguvu za asili, na vita?
Kila mahali kuna
maafa ya kutisha yanayotokea kila siku.
Ni nani anayewajibika
kwa sababu ya maafa, shida, na taabu katika dunia?! Watu wengi humlaumu Mungu
kwa matatizo wanayopitia.! Mara kwa mara utawasikia wakiuliza swali, Kwa nini Mungu
alitenda hivi kwangu?
Hebu tutizame kile
ambacho Biblia inasema juu ya pambano kuu linaloendelea kati ya nguvu za wema na
zile za uovu.! Waweza kuuliza, Kama Mungu haleti shida zote hizi na huzuni
duniani, ni nani anayewajibika kwa maafa yote haya tunayoyashuhudia?
Biblia inasonda
kundi lenye makosa!! Yesu alieleza
kisa juu ya mkulima alliyepanda mbegu ndani
ya shamba, lakini mimea ilipokua, kulikuwa na magugu ndani ya shamba. (Fungu:
Mathayo 13:27) !
Watumishi wa yule
mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, "Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu
nzuri katika shamba lako.
Sasa magugu yametoka
wapi?" ! Walitaka kujua, magugu yalitokea wapi.
(Fungu: Mathayo
13:37) ! Yesu akawaambia, Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
Lile shamba ni ulimwengu.
Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao ufalme wa mbinguni ni wao,lakini yale magugu
ni wale watu wa yule mwovu. Adui aliyepanda yale magugu ni ibilisi.
Mathayo 13:37-39! Mavuno
ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.
Unaona, wakati Mungu
anapojaribu kuonyesha wema kwa kila mmoja, kuna nguvu nyingine itendayo kazi duniani
iletayo maafa, misiba, mauti, na maradhi kwa maisha ya wana wa Mungu.
Kitabu cha mwisho cha
Biblia, Ufunuo, kinatuambia jinsi mambo yalivyoanza ili tuwe na ukweli hakika juu
y kile kilichotokea mbinguni na kusababisha taabu kubwa namna hii katika Sayari
Dunia.! Tutagundua chanzo cha uovu. Waweza kushangaa,lakini kulipata kuwa na
vita mbinguni!
Kisha kukazuka vita
mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia
pamoja na malaika wake. na joka hilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa
na nafasi tena juu mbinguni kwa ajili yake na malaika wake.
Basi joka hilo kuu
likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia ibilisi au
shetani. Ndiye anayeudanganya ulimwengu wote;
Naam, alitupwa
duniani, na malaika wake pamoja naye.! Ufunuo 12:7-9.
Sasa, tazama jinsi
huyu joka, au mwovuanavyotambulia katika Ufunuo 12:3,4:
Ishara nyingine
ikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na
kila kichwa kilikuwa na taji.
Joka hilo liliburuta
kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani...
Ni wazi kwamba
theluthi moja ya malaika wa mbinguni walimfuata mdanganyifu katika uasi wake dhidi
ya Mungu.!
Lakini hebu
tuchunguze zaidi juu ya huyu malaika aliyeanguka aitwaye Lusifa.! Katika Agano
la Kale anatajwa kama Mfalme wa Tiro, na yasema hivi juu yake: Ni wazi kwamba
theluthi moja ya malaika wa mbinguni walimfuata mdanganyifu katika uasi wake dhidi
ya Mungu.! Lakini hebu tuchunguze zaidi juu ya huyu malaika aliyeanguka aitwaye
Lusifa.! Katika Agano la Kale anatajwa kama Mfalme wa Tiro, na yasema hivi juu
yake: (Fungu: Ezekieli 28:12 -14)!
Bwana MUNGU asema
hivi: Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.! Ezekieli
28:12.
Ulikuwa ndani ya Adeni,
bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako....! Ezekieli
28:13.
Wewe ulikuwa kerubi
mwenye kutiwa mafuta afunikaye...ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu; umetembea
huko na huko kati ya mawe ya moto.! Ezekieli 28:14
Lusifa alikuwa malaika
mkamilifu, aliyeumbwa kwa ukamilifu kwa namna zote.! Alikuwa malaika
aliyesimama mbele za Mungu kama kerubi afunikaye.
Lusifa alishikilia
nafasi iliyotukuka huko mbinguni. Katika pande zote mbili za kiti cha rehema au
cha enzi cha Mungu kulikuwa na malaika wawili-mmoja kulia na mmoja kushoto.
Mmoja wa hawa alikuwa Lusifa.
Hakuridhika kwa kuwa karibu hivyo na Mungu.!
ALITAKA KUWA MUNGU!! Kitu kilitokea kwa Lusifa katika uhusiano wake wa karibu
na Mungu. Mungu alimwambia
Lusifa, (Fungu: Ezekieli
28:15)!
Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu
siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.! Ezekieli 28:15. (Fungu:
Ezekieli 28:17).
'Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri
wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako...;! Ezekieli 28:17.
Huyu malaika mzuri, aliyetukuka akajipenda
nafsi. Alitamani utukufu na
heshima iliyomstahili Mungu pekee. Akawa na uchu wa madaraka. Akawa na ujasiri
wa kumpa changamoto Muumbaji hata katika swala la utawala wa ulimwengu!
Sikiliza kwa makini: Fungu: Isaya 14:12-14)!
Jinsi ulivyoanguka
kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa..........
Nawe ulisema moyoni
mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za
Mungu... .....Nitafanana na Yeye Aliye juu.! Isaya
14:12-14.
Maneno haya ya kiburi yalipoendelea
kumiminika toka midomoni mwa Lusifa, upendo ulio kamili na amani ya mbinguni
vikavunjwa vunjwa katika mamilioni ya vipande vidogo vidogo vya uchoyo.
Haikuchukua muda hadi Lusifa alipoanza
kusambaza roho ya kutoridhika kati ya malaika wengine.! Pole pole bali kwa uhakika, aliharibu
upendo wa Mungu na haki yake.
Kama tunda lililooza
kwenye tenga, uasi wake ulienea kwa malaika wengine mbinguni.!
Pengine unashangaa
kwa nini Mungu hakumuangamiza Shetani wakati ule.! Mungu angeweza kuwaangamiza
Lusifa na malaika
waliojiunga naye katika
uasi kwa muwako mmoja tu wa kupofusha, lakini kama angefanya hivyo, viumbe wote
wangemtumikia kwa hofu.
Mungu ni Mungu wa
upendo. Aweza tu kuwa na furaha katika mahusiano ya upendo na viumbe Vyake
ambapo wanamwabudu kwa sababu wanampenda na kumuamini.
Shetani alikuwa ametoa
changamoto kwa sheria za Mungu na haki yake, lakini Mungu hakuwa ameweka sheria
hizi kwa mabavu ili aonyeshe ni nani aliye mkubwa! Aliziweka kulinda viumbe
Wake,
kuhakikisha amani
yao na furaha.
Sheria zake ni kama
taa na alama zionyeshazo mwendo kasi ulio salama vyote vikiwa vimepangwa kwa
ajili ya usalama wetu na kwa ubora wetu.! Bali huyu aliyeheshimika kati ya
malaika wote alidhani ya kwamba angeweza kuendesha ulimwengu kwa ubora kuliko Mungu
Muumbaji wake!
Shetani, adui wa
Mungu , alijifanyia 'mwovu' ndani yake!
ITAENDELEA KATIKA SOMO LIJALO...............
No comments:
Post a Comment