Sehemu ya 2.
Mungu anampa kila
mtu uwezo wa kutii ama kutotii.! Kutokana na haki na upendo, Mungu amemruhusu
Shetani kueleleza kwa ulimwengu jinsi ambavyo angeuongoza ulimwengu.! Hatuelewi
jinsi yote haya yalivyotokea wakati Mungu alikuwa mwema na mwenye upendo kwa
wote.
Pambano lililoanza
mbinguni halijaisha, limebadilisha tu viwanja!!
Sasa Dunia ni eneo
ambamo pambano kuu kati ya wema na uovu lingepiganwa, ambapo shetani angeeleleza
aina yake ya serikali na jinsi ambavyo angeliiongoza dunia.
Lakini kwa nini
Dunia? Kwa nini sayari yetu ikawa ....
(Fungu: 1 Wakorintho
4:9)! .... tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu.
! 1Wakorintho 4:9.
Dunia ilikuwa ndipo tu imetoka mikononi mwa Muumbaji,
ikiwa inang'aa na ikiwa kamilifu, nzuri kuliko maelezo.! Ni wazi Shetani alifikiri
vivyo pia, kwani aliiona dunia hii kama tunu
ufaayo kuikamata.!
Angejaribu kuikamata sayari hii ikiwa katika
uzuri uwezao kuvunjika - dunia ambayo ndipo imezaliwa.
Ingawa Adamu na Hawa, baba na mama wa
wanadamu, waliumbwa wakamilifu, hawakufanywa wawe juu kuliko uwezekano wa
kutenda makosa.
Walikuwa huru kuchagua kumpenda na kumfuata
Mungu ama kutojali maelekezo Yake.! Lakini utii wao ulipaswa kujaribiwa, na
jaribu hilo
lingewekwa kwenye mti. Mungu alionya, (Fungu: Mwanzo 2:16,17)!
Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula; walakini
matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula
matunda ya mti huo utakufa hakika.! Mwanzo
2:16,17.!
Hilo
laonekana kuwa lilikuwa ombi la busara. Lazima walijihisi salama kabisa. Lakini
mtu yuko katika hatari kubwa akutwapo bila kujilinda kwa sababu hujihisi yu
salama.
Hicho ndicho kilichotokea kwa Hawa.! Shetani
alitumia uwezo wake upitao akili ya mwanadamu ili kumdanganya.! Shetani hutenda
kazi hadharani kwa nadra. Yeye ni mdanganyifu sana.! Anatumia mifumo ya jamii,
watu, au hata nyoka!
Kwa sababu hiyo
Paulo anasema: (Fungu: Waefeso 6:11-12)!
Vaeni silaha anazowapeni
Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
Maana vita vyenu si
kati ! yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho;
tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa
giza.! Waefeso 6:11,12.
Hawa alidanganywa.! Hakudhani
maneno yaliyotoka kwa nyoka yalitoka kwa Shetani.! Mwovu, akinena kupitia kwa
joka, alimwambia,
(Fungu: Mwanzo 3:1)!
....Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?! Mwanzo
3:1. (Fungu: Mwanzo 3:2-4)!
Hawa akajibu,
Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini atunda ya mti ulio katikati
ya bustani Mungu amesema, 'Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Nyoka akamwambia
mwanamke, 'Hakika hamtakufa.' ! Mwanzo 3:2-4
Hawa alipokuwa akimsikiliza joka, lazima
lilipita wazo ghafla kichwani kwamba alikuwa akinena tofauti na na jinsi Mungu
alivyowaambia.! Pengine kwa kuhisi ya kwamba alionekana kuchanganyikiwa, joka
kwa upesi aliongeza, (Fungu: Mwanzo 3:5)! Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku
mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema
na mabaya.! Mwanzo 3:5.
Mwovu alipendekeza ya kwamba Mungu hakufanya
haki, kwamba alikuwa akizuia kitu fulani kizuri.! Kuwa kama Mungu ilikuwa tamaa
kubwa iliyomla Shetani na kuwa chanzo cha maanguko yake. Sasa
Hawa pia aliliona kuwa wazo zuri pia; na kwa
haraka bila kufikiri, aliuzika. (Fungu:
Mwanzo 3:6)!
Mwanamke alipoona kuwa ule mti wafaa kwa
chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa
katika matunda yake akala...! Mwanzo 3:6.
Adamu na Hawa wakashindwa
jaribio la Mungu la upendo na utii, na haikuchukua muda mrefu kwa wao kugundua
ya kwamba kuna jambo limeharibika.
Shetani alikuwa ameteka
nyara dunia iliyozaliwa karibuni! Tangu wakati huo, akadai cheo cha , Mfalme wa
Dunia hii.! Mtawala wa sayari iliyo katika uasi!! Adamu na Hawa walikuwa
wameisikiliza sauti ya mwovu.
Kadiri siku hii ya msiba
mkubwa ilipokuwa inafikia mwisho, Mungu akaja jioni wakati wa jua kupunga kama
kawaida yake, akiwaita Adamu na Hawa.! Hadi sasa, huu ulizoeleka kuwa wakati wa
furaha
mno wa siku - fursa
ya kutembea na kuzungumza na Mungu moja kwa moja Yeye aliyewaumba. Lakini katika
siku hii walikimbia na kujificha vichakani!
Muhtasari (Fungu:
Mwanzo3:10)! ....Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni
uchi, nikajificha.! Mwanzo 3:10.
Muhtasari Adamu
alikuwa hajapata kuogopa kabla ya hapo, lakini hicho ndicho dhambi
inachofanya.! Inamfanya mtu amuogope hata Mungu. (Fungu: Mwanzo 3:11)! Mungu
akajibu, ...Je! Umekula wewe matunda ya mti niliokuagiza usiyale?! Fungu 11.! Adamu
akajibu: (Fungu: Mwanzo 3:12)! ...Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye
aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.! Mwanzo 3:12!
Saa chache kabla ya
hapo, Adamu alikuwa tayari kufa pamoja na Hawa.! Sasa alimlaumu na pia
akamlaumu Mungu kwa kumuumba. Jinsi gani dhambi inavyovunjavunja upendo
uliomkamilifu!
Lakini Hawa naye hakushindwa kushitaki. Mungu
alipomuuliza juu ya kile alichokuwa ametenda, alijibu, Muhtasari (Fungu: Mwanzo
3:13)!
....Nyoka alinidanganya, nikala.! Mwanzo 3:13.! Hawa alimshutumu Mungu pia!
Kwa maneno mengine, alikuwa anasema, Ni nyoka uliyemuumba ndiye aliyeniingiza taabuni.
Siku ile ile Adamu
na Hawa wakawa chini ya kifo! Ili kuwazuia Adamu na Hawa wasile matunda ya mti
wa uzima, Mungu akawaondoa kutoka kwenye nyumba yao ya bustani. ! Mwovu alisema
ya kwamba wasingekufa, bali Biblia yasema, Muhtasari (Fungu: Mwanzo 5:5)!
Siku zote za Adamu alizoishi
ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. Mwanzo 5:5! Wakiwa wamechelewa
kabisa waligundua ya kwamba mwovu alikuwa…... ni mwongo na baba wa huo.
No comments:
Post a Comment