MATUNDA YA MTI WA UJUZI' USILE , SIKU UTAKAPO KULA UTAKUFA HAKIKA.
Fungu la tafakari: “Kwa
hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti;
na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamafanya dhambi.” Warumi
5:12.
Makusudi ya somo hili:
Kuonyesha kuwa mwanadamu aliumbwa vyema ili aishi millele, na kwamba kifo ni
matokeo ya kutokutii amri za Mungu.
UTANGULIZI..
Kazi ya uumbaji kwa siku sita, ilimalizika kwa kuumbwa kwa mwanadamu.
Ulikuwa mpango wa Mungu, mwanadamu aweze
kuufurahia ulimwengu milele. Lakini ilitegemea utii wake na kuwa na dini ya
uongozi wa Mungu.
Mungu aliwaumba wanyama wengine wote – Samaki, ndege, mijusi, wadudu,
n.k “kwa jinsi yake” Kila jamii ya viumbe ilikuwa na mwonekano wa namna yake.
Lakini mwanadamu aliumbwa kwa namna ya Mungu, na si ya wanyama. Kwa
viumbe wengine Mungu alitamka na
vikatokea, lakini kwa mwanadamu, Mungu alienda chini, akafinyanga udongo, na
“kumfanya” mtu kwa sura yake. Mwanadamu alikuwa ni kilele cha ubora wa kazi ya
uumbaji ya Mungu.
“Pumzi ya Mungu” iliyoleta uhai kwa umbo lililofinyangwa la “mtu” ni
zaidi ya pumzi tunazozijua. Hii ni kanuni ya uhai inayoweza kufananishwa na
umeme unaoleta tofauti unapounganishwa kwenye gropu. Ni nguvu inayoanzisha uhai
na kuendeleza (Matendo 17:28). Nguvu hii inapoondolewa, uhai wamtu hukoma.
Kuanguka kwa mwanadamu katika dhambi:
Mwanadamu alipoumbwa aliwekwa katika bustani ya Edeni. Mwanzo 2:8.
“Mungu alimweka mwanadamu chini ya sheria, kama sharti lisilokwepeka la
kuishi kwake”
Bwana Mungu akachipisha katika
ardhi kila mti wa matunda unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti
wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mwanzo 2:9.
Bwana Mungu akawapa agizo kuwa matunda ya mti wa ujuzi
wa mema na mabaya usile; kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa
hakika.
Mwanzo 2:17.
“Wazazi wetu wa kwanza, ijapokuwa waliumbwa bila
dhambi, hawakuwa kwenye mazingira yasiyofikiwa na dhambi. Mungu aliwaumba wawe
na uhuru wa kimaadili, wanye uwezo kuchagua kutii au kutotii. ... Mti wa ujuzi,
ambao ulikuwa jirani na mti wa uzima katikati ya bustani uliwekwa kuwa mtihani
wa utii, imani na upendo wa wazazi wetu wa kwanza.
Dhambi iliingiaje?
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa
mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema
Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanzo 3:1
Majibu ya mwanamke;
Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya
bustanini twaweza kula;
lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu
amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Mwanzo 3:2,3;
Nyoka akasema nini baadaye?
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana
Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho,
nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanzo 3:4,5.
Shetani aliwaonyesha “Adamu na Hawa” kwamba
wangenufaika kwa kuvunja sheria ya Mungu. Je, siku hizi hatusikii hoja
zinazofanana na hizo? Watu wengine wanashutumu wale wanaozitii amri za Mungu,
wanasema wanamawazo mafinyu, huku wakidai wenyewe kuwa wanamawazo mapana na
wanafurahia uhuru mkubwa zaidi. Hiki ni nini, kama si mwangwi wa sauti ya
Shetani toka Edeni inayosema , ‘siku mtakayokula matunda ya mti huo’ (vunjeni
matakwa ya Mungu) ‘Mtakuwa kama Mungu’’’’?
Ona madhara ya dhambi:
Baada ya Shetani kufanikiwa kuwadanganya wazazi wetu
wa kwanza, madhara yakaanza kujitokeza. Wakafumbuliwa macho yao wakajiona wako
uchi, (yaani wakavuliwa mavazi ya utukufu aliyo wavika Bwana) wakatengeneza
mavazi ya mtini wakajivika (yaani wakajivika mavazi bandia) Wakajificha yaani
wakakimbia mbali na uso wa Bwana. Mwanzo 3:6,7,16,17-19.
Laana ikawa juu yao. Kuzaa kwa uchungu, kula kwa
jasho, na kifo kikawakabili, sasa ukweli wa Shetani ni upi? Alisema “hamtakufa
bali mtafanana na yeye” je, leo hatufi? Hata wazazi wetu wa kwanza nao
walikufa.
“Kwa mtu mmoja dhambi ikaingia ulimwenguni” na sote
tumeshuhudi vifo, ajali, majanga ya kila namna. ...”Mauti ikwafikia wote kwa
sababu wote wamefanya dhambi. Warumi 5:12. haya yote ni ushuhuda kuonyesha kuwa
dunia inasumbuka na iko katika maumivu.
Kauli ya Mungu imebaki palepale “Hakika mtakufa” na ni
kweli ndivyo ilivyo, hakuna anaye bisha sote tunajua kuwa siku moja tutakufa.
WITO: Niheri kufa
katika Bwana, maana Mungu hafurahishwi na kifo cha mwenye dhambi, bali
ghairini, mrejee kwake naye atawamehe.
AHSANTENI WOTE MLIOSHIRIKI PAMOJA NAMI KATIKA
SOMO HILI.
No comments:
Post a Comment