Wednesday, May 10, 2017

KABLA MTOTO HAJAZALIWA

πŸ“–“Ndipo huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa.” Waamuzi 13:8.

πŸ’Mungu mwenyewe alimtokea mkewe manoa na kumwambia kuwa atakuwa na mtoto mwanamume, na kwamba atakuwa mtu mkubwa atakayekomboa Israeli. Kisha akampatia maelekezo kamili kuhusu namna atakavyomlisha. Hebu tuuchukulie ujumbe huu kama unaotolewa maalumu kwa kila mama hapa duniani. Iwapo unataka watoto wako wawe na akili safi na bora, yakupasa uwe na kiasi katika mambo yote. Hakikisha moyo wako ni safi na akili yako ni timamu, ili kurithisha uzao wako afya bora ya kiakili na kimwili.

πŸ’Kila mama anapaswa kulijua jukumu lake. Apate kujua kuwa tabia ya watoto wake itategemea zaidi mno tabia yake kabla na baada ya kuwazaa, kuliko ilivyo mivuto mingine ya nje iwe mizuri au mibaya. Mama aliye mwalimu bora kwa watoto wake, sharti kabla ya kuwazaa, adumishe mazoea ya kujikana nafsi na kujitawala; kwani huwarithisha sifa zake binafsi za kitabia, ziwe nzuri au dhaifu.
πŸ’Washauri wasiofaa huwahimiza wakina mama umuhimu wa kukidhi kila tamaa na uchu wa chakula, ila ushauri huo ni potofu. Mama kwa agizo la Mungu ameagizwa kudhihirisha kiwango cha juu cha kujitawala. Na akina baba na akina mama wapaswa kujumuika pamoja katika jukumu hili. Wazazi wote wawili, hurithisha tabia zao kwa watoto wao, kiakili, kimwili, kimwenendo na kishauku yao ya ulaji.

πŸ’Wengi huchukulia kimzaha somo la kiasi. Hujidanganya kuwa BWANA hajihusishi na mambo madogo madogo kama vile kula na kunywa. Ila endapo Mungu hajihusishi, mbona akajifunua kwa mkewe Manoa, akitoa maelekezo kamili, akimsisitiza mara mbili awe mwangalifu kutokuyapuuzia.

πŸ’Wazazi wengi huchukulia madhara ya mivuto ya kipindi kabla ya mtoto kuzaliwa ni jambo dogo la kupuuziwa; ila mbingu hazichukulii hivyo. . . . Kwa maneno yaliyoongelewa kwa mama huyu wa Kiebrania, Mungu huongea kwa wakina mama wote wa zama zote.

No comments: