Sunday, September 16, 2018

UPENDO WA KWELI

Kigezo cha kwamba unakubalika ama unapendwa na watu, siyo ile idadi kubwa ya watu waliofika au watakaofika siku ya harusi yako. Kuacha hawa wanafiki wanaotumia gharama kubwa kukununulia jeneza na kugharamia mazishi siku ukifa.

Kigezo cha kwamba unapendwa ni ile idadi ya watu watakaofika ama kuja kukuona siku ukipata matatizo, siku ya kuugua kwako.

Ni rahisi sana watu kukusaidia, kukuchangia, kukupa zawadi mbali mbali siku ya harusi yako lakini ni vigumu sana watu hao hao waliokusapoti na kukusaidia siku ya harusi, wakaja kukusaidia siku ukipata matatizo..!

Amini usiamini siku ya matatizo yako wengi wao wengine ni marafiki zako kabisa na ndugu wa damu kama siyo wote, watakukimbia na kujitenga na wewe kabisa.

Hivyo basi mtu mmoja anayekusaidia wakati wa shida, wakati upo hoi kitandani ni bora zaidi kuliko watu elfu waliokusaidia siku ya harusi, siku ya furaha ama siku ya mahafali yako.

Mpende na kumheshimu sana mtu aliyekusaidia siku ukiwa na changamoto, siku ya matatizo.

 

No comments: