Saturday, September 22, 2018

BIBLIA BARUA YA MUNGU KWETU

Mungu amejifunua kwetu kwa njia nyingi, mojawapo ni njia kupitia uumbaji au njia ya asili. Tunapoona kila kitu katika dunia hii ni kazi yake. Maana hata sisi tu kazi yake, sio tu kazi yake bali pia tumeumbwa kwa mfano wa sura yake na hata vitu vingine alisema na vikafanyika, mwanadamu akaumbwa kwa Mungu kuushika udongo na kuufinyanga na kutuwekea pumzi ya uhai iliyotoka kwake.

Sehemu ya pili Mungu amejifunua kupitia neno lake yaani Biblia.

Biblia nini? kwa nini tuiamini Biblia? hivi kweli ni sauti ya Mungu, hivi kuna mambo ambayo hatupaswi kuyatii? hivi tunaweza kuyatii yote? Kati ya Neno la Mungu na kile viongozi wangu wanachoniambia nitii kipi? Dini yangu na biblia kipi kiko juu?
Biblia inaonyesha nia ya Mungu, inafunua hali ya binadamu jinsi ilivyo, njia ya wokovu, kuangamia kwa mwenye dhambi na furaha ya waaminio. kanuni zake ni takatifu, amri zake haziepukiki, historia zilizomo ni za kweli, na uamuzi wake kamwe haubadilshwi.

Uisome ili kuwa na hekima, uisome ili usalimike na tenda isemavyo ili uwe mtakatifu.
Biblia ni ramani na mkongojo wa msafiri, ni fira ya nahodha, upanga wa askari na mkataba wa mkristo. Mbingu inafunguliwa na inabainisha milango ya jehahanamu waziwazi.
Kristo ndio kiini kikuu cha biblia. ndiye daraja la kutuunganisha na baraka za Mungu.

Biblia inapaswa ijae akilini, iutawale moyo na iongoze miguu.Uisome mara kwa mara tena kwa maombi. Ni mgodi wenye utajiri bustani iliyojaa utukufu wa Mungu. Mungu amejifunua kupitia hapa ili kila mmoja aweze kumfahamu Mungu. Itawatia hatiani wale wote wanaodharau na kutoyatii maandiko matakatifu.
2Tmetheo 3: 15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki

Tunapaswa kutii kila neno lililopo ndani yake na wala sio tu baadhi ya sehemu fulani fulani kama ambavyo wengi tunafanya. 

Mfalme Daudi naye anasema yakuwa katika zaburi 119:115 neno lako ni taa ya miguu yangu na Mwanga wa njia zangu... yatupasa kuwa kuwa ndio iwe kiongozi wetu kila wakati.
2Petro 1:19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


Mungu aliamua kuwasiliana na wanadamu kwa kutumia akili za mwanadamu, kalamu ya mwandamu na lugha ya mwanadamu lakini hapa Petro anasema waliongozwa na Roho mtakatifu kuweza kuuandika ujumbe huu. Ujumbe wa biblia haukuletwa na mwanadamu bali ni Mungu kupitia mwanadamu. Lakini pia haupaswi kutafsiria ujumbe huu kama sisi tupendavyo na wengi wetu tumefanya hivi na hivyo wengi wamepotoshwa. Lazima tuombe kabla ya kusoma ili tuweze kupewa tafsiri sahihi kama Mungu alivyokusudia.
Bwana akubari tunapooanza katika mfuulizo wa masomo ya Biblia. 

Endelea kutembelea blog hii tujifunze pamoja juu ya biblia.

By Yusuph Bigurube

No comments: