Saturday, November 22, 2014

THE JESUITS

Shirika la Jesuits lilianzishwa na Ignatius Loyola aliyezaliwa mwaka 1491 na kufariki Julai 31, 1556. Sherehe ya Ignatius.
Loyola hufanyika kila ifikapo Julai 31 ya kila mwaka, siku aliyokufa. Mkuu wa shirika la Jesuit anaitwa “Black Pope” yaani “Papa Mweusi.” 
Hapa haimaanishi kuwa mkuu huyo anatakiwa awe wa rangi nyeusi yaani mwafrika bali neno ‘black’ linamaanisha ‘asiyeonekana,’ na kwa maana hiyo Jesuit Society wanafanya kazi za siri, zisizoonekana, tena za giza ambazo ni kinyume na nuru ya neno la Mungu.
Shirika hili lilianzishwa ikiwa ni matokeo ya kanisa Katoliki kupiga vita uprotestant.
Kujitoa kwa Loyola katika kulitumika kanisa kunaweza kuonekana kwenye kanuni 13 za shirika la Jesuits zinazolihusu kanisa; “Rules for thinking with the church” anaposema “I will believe that the white that I see is black if the hierarchical Church so defines it”.
Kwamba “nitaamini rangi nyeupe ninayoiona kuwa
ni nyeusi kama mfumo wa uongozi wa kanisa utatafsri hivyo.” Na ndivyo ilivyo katika shirika hili ya kwamba mtu anapaswa kuamini na kufanyia kazi kile anachofundishwa na kanisa hata kama dhamira yake inamwambia kuwa hicho si sahihi. Hebu soma
nukuu hizi ili tuone chanzo cha chama cha Jesuits:
“Kuinuka kwa dhama za giza kulitokana na kuruhusu Biblia ipatikane kwa urahisi hata kwa watu wa kawaida na mafundisho ya waprotestant wanamatengenzo. Mafundisho haya yalikuwa na msingi wa kutafsiri unabii kutokana na historia; yaani kuwakilisha siku 1260 za Danieli na Ufunuo kuwa miaka 1260.
Viongozi wa matengenezo kama Luther, Calvin, Huss, Wycliff, Knox, Latimer, Cranmer, Ridley, Hooker, Sir isaack Newton na wengine waliamini hivyo na kufundisha.” Ibid p 7.
“Kwa kutumia mbinu hii ya kutafsiri unabii, kanisa
la Roma lilionekana wazi kuhusika na unabii huu wa pembe ndogo katika Daniel 7, na mnyama wa Ufunuo 13:1, mwanamke wa Ufunuo 17, ikiwa ni pamoja na kichwa cha kanisa kuwakilisha Mtu wa Kuasi wa 2 Wathesalonike 2. Kadri mafundisho haya yalivyozidi, kanisa la Roma lililazimika kujilinda dhidi ya kuongezeka kwa ushahidi wa unabii wa Biblia kulihusisha kanisa hilo.
Hivyo upapa ukaanza kuweka mipango ya kuwapinga waprotestant kwa kuanzisha ‘Jesuit society’ ili kisaidie kufundisha mafundisho ya kanisa na kuharibu mafundisho na vitabu vyote vilivyokuwa kinyume na kanisa na kuanzisha “Holy Office of the Inquisition” maalumu kwa ajili ya kuwatesa hata kuwaua wapinzani wa kanisa.” Ibid. pp 126, 127.
Kati ya mwaka 1524 na mwaka 1537 Loyola alisomea Theology huko Hispania na Ufaransa. Mwaka 1534 alifika Ufaransa wakati wa kipindi cha mapambano dhidi ya uprotestant, mapambano ambayo yalimfanya John Calvin akimbie kutoka Ufaransa.
Mwaka 1539, Loyola akiwa na wenzake walifanikiwa kuanzisha muungano na kuuita ‘Society of Jesus’. Mwaka uliofuata yaani 1540 chama hicho kikapewa baraka na Papa Yohana III na ilipofika mwaka 1548 Papa huyo akatoa kibali kwa Society of Jesus ili kiweze kushughulika na maswala ya kiroho.
Loyola alikufa mnamo Julai 31, 1556 na akabarikiwa na Papa Paul V mwaka Julai 27, 1609, akapewa hadhi ya utakatifu Machi 12, 1622 na Papa Gregory XV na akatangazwa kuwa kiongozi wa maswala la kiroho mwaka 1922 na Papa Pius XI.
Jina kamili la Loyola lilikuwa ni Íñigo akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 13.
Baada ya kifo cha mama yake mwaka 1506 Íñigo alichukua jina la mwisho “de Loyola” kutokana na jina la mji ulioitwa Loyola ambako alizaliwa. 
Akaamua kutumia jina la “Ignatius of Loyola” yaani Ignatius anayetokea mji wa Loyola.
Mwaka 1534 aliwakusanya marafiki zake sita ambao alikutana nao chuo kikuu wakiwa ni wanafunzi wenzake ambao ni Francis Xavier, Alfonso Salmeron, Diego Laynez na Nicholas Bobadilla wote wakiwa ni Wahispania; Peter Faber akiwa ni Mfaransa; na Simao Rodrigues aliyekuwa Mreno. Asubuhi ya tarehe 15 Agust 1534, katika kanisa la Our Lady of the Martyrs huko Montmartre, Loyola akiwa na wenzake sita ambapo mmoja wa marafiki hao alikuwa ni padre, waliapa kutumika maisha yao yote. Ignatius akawa ndiye kiongozi mkuu (Superior General) wa chama cha Yesu – Society of Jesus.
Yeye ndiye aliyetunga katiba ya chama hicho mwaka 1540. Nukuu muhimu tunayoweza kuichukua kutoka kwa Ignatius wa Loyola ni hii: “That we may be altogether of the same mind and in conformity with the Church herself, if she shall have defined anything to be black which appears to our eyes to be white, we ought in like manner to pronounce it to be black.
For we must undoubtingly believe, that the Spirit of our Lord Jesus Christ, and the Spirit of the Orthodox Church His Spouse, by which Spirit we are governed and directed to Salvation, is the same.” [Ignatius Loyola, Spiritual Exercises, Rule 13 Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church, 2nd ed. (London: Oxford University Press, 1963), p. 260.]
“Kwamba wote tuwe na nia moja na kukubaliana na kanisa, kama limetafsiri kitu chochote kuwa ni cheusi wakati kinaonekana machoni mwetu kuwa ni cheupe, tunapaswa kukitangaza kuwa ni cheusi. Maana bila shaka
tunapaswa kuamini, kwamba roho wa bwana wetu Yesu kristo, na roho wa kanisa la Orthodox ndugu yake, roho ambaye anatuongoza katika wokovu, ni yule yule.” [Ignatius Loyola, Spiritual Exercises, Rule 13 Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church, 2nd ed. 
(London: Oxford University Press, 1963), p. 260.]
Kwa mujibu wa Ignatius Loyola, kanisa Katoliki na
kanisa la Orthodox ni ndugu mmoja na wote wanaongozwa na roho mmoja.
Lakini pia tunaweza kujiuliza kwa nini Loyola atumie rangi nyeusi hata kama ni nyeupe? Jibu ni kwamba alikuwa anaongelea kiongozi mkuu wa chama hicho cha Jesuits ambaye anaitwa ‘black Pope’ yaani Papa mweusi. 
Lakini pia Loyola aliweka kanuni 13 za kuongoza chama cha Jesuits.

No comments: