Je kila dhehubu la Kiprotestanti katika nchi ya Marekani litaingia katika muungano wa makanisa unaokuja?
Wakati makanisa makuu ya Marekani, yatakapoungana katika yale mafundisho wanayoyashikilia kwa pamoja, yataishawishi seirikali kuyatia nguvu kisheria maagizo yao na kuzitegemeza desturi zao, ndipo Marekani ya Kiprotestanti itakua imeunda sanamu ya utawala wa kidini wa Rumi, na ndipo utoaji adhabu ya kiserikali kwa wale wanaopinga utakuwa jambo lisiloepukika.
Ni katika msingi gani hatimaye makanisa ya Kiprotestanti yataweza kuungana?
"Tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya Kiprotestanti inaangaliwa na wengi kama ushahidi wa kukata maneno kwamba hakuna juhudi yoyote inayoweza kufanywa ili kupata umoja kwa kulazimishwa. Lakini kwa m,iaka mingi, katika makanisa yenye imani ya Kiprotestanti, pamekua na maoni yenye nguvu, yanayozidi kuongezeka ambayo yanapendelea muungano uliojengwa juu ya mafundisho wanayoyaamini kwa pamoja. Ili kupata muungano kama huo, mjadala wa mafundisho yote ambayo hawaafikiani wote kwa pamoja - haidhuru yawe ya muhimu jinsi gani kutakana na msimamo wa Biblia- ni lazima uachwe.
Ni mafundisho gani makuu mawili yenye makosa ambayo makanisa hayo yameyashika kwa pamoja?
"Kwa njia ya makosa makuu mawili... imani kwamba roho haifi, na utakatifu wa Jumapili.... Shetani atawaleta watu chini ya madanganyo yake. Wakati lile la kwanza linaweka msingi wa imani ya umizimu, lile la pili linaleta mapatano ya kukubaliana na Rumi"
Je, Uprotestanti hatimaye utaungana na Ukatoliki?
"Neno la Mungu linafundisha kwamba matukio ya [kuikandamiza Sabato] yatarudiwa tena wakati Wakatoliki wa Rumi na Waprotestanti watakapoungana kwa lengo la kuitukuza Jumapili"
"Hatuwezi kuona ni kwa jinsi gani Kanisa Katoliki la Rumi linaweza kujinasua dhidi ya shitaka la kuabudu sanamu. ... Na hiyo ndiyo dini ambayo Waprotestanti wanaanza kuiangalia kwa upendeleo mkubwa sana, na ambayo hatimaye itaungana na Uprotestanti.
"Maadam muda wa majaribio bado ungalipo, kutakuwepo na nafasi kwa mwinjilisti wa vitabu kufanya kazi. Wakati madhehebu za dini zitakapoungana na upapa ili kuwatesa watu wa Mungu, mahali palipo na uhuru wa dini patafunguliwa kwa uinjilisti wa vitabu"
Je, kutakuwa na muungano wa mfumo au muungano katika utendaji?
"Ulimwengu unaojidai kuwa ni wa Kiprotestanti utaungana kwa mapatano na yule mtu wa kuasi, ndi0po kanisa na ulimwengu vitakua katika mwafaka potofu"
"Uroma katika Ulimwengu wa Zamani wa Ulaya, na Uprotestanti Ulioasi katika Ulimwengu Mpya wa Marekani, watafuata njia ileile katika katika kuwashughulikia wale wanoziheshimu amri zote za Mungu.
Je, ni Rumi itabadilika au ni Uprotestanti ndio utakaobadilika ili kufanya muunganiko tena uwezekane?
"Hata hivyo, muungano huo, hautafanyika kutokana na badiliko katika Ukatoliki, kwani Rumi kamwe haibadiliki. Inadai kwamba haiwezi kukosea. Ni Uprotestanti, utakaobadilika. Kukubali mawazo yaliyo huru kwa upande wake kutauleta mahali utashikana mkono na Ukatoliki. 'Biblia, ndiyo msingi wa imani yetu;ilikua ndiyo kauli ya Waprotestanti katika siku za Luther, wakati Wakatoliki walipaza sauti zao, wakisema, Mababa, desturi, mapokeo; siku hizi Waprotestanti wengi wanaona ni vigumu kuthibitisha mafundisho yao kutoka katika Biblia, lakini hata hivyo, hawana ujasiri wa kimaadili kukubali ukweli unaohusisha msalaba; kwahiyo wanaelekea kwenye msimamo wa Ukatoliki. Naam, Waprotestanti wa karne ya kumi na tisa wanawakaribia kwa kasi Wakatoliki katika kukosa kwao uaminifu kuhusu Maandiko"
"Waprotestanti wa Marekani watakuwa msitari wa mbele katika kunyosha mikono yao juu ya shimo kubwa na kuushika mkono Umizimu; watanyosha mikona juu ya shimo kubwa na kushikana mikono na mamlaka ya Rumi; na chini ya uongozi wa muunganohuo wa utatu [Uprotestanti, Umizimu, na Ukatoliki], nchi hii itafuata katika nyayo za Rumi kwa kukandamiza uhuru wa dhamiri"
"Wakati Uprotestanti utakapo nyosha mkono kuvuka shimo kubwa na kuushika mkono wa Mamlaka ya Rumi, wakati utakaponyosha mkono juu ya shimo kubwa na kushikana mikono na Umizimu, wakati chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, nchi yetu [Marekani] itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya Katiba yake kama Serikali ya Kiprotestanti na ya Jamuhuri, na kuandaa njia kwaajili ya kueneza uongo na udanganyifu wa upapa, ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia wa utendaji wa miujiza wa ajabu wa Shetani na kwamba mwisho u karibu"
"Uprotestanti utaipatia mamlaka ya Rumi mkono wa ushirika. Ndipo itapitishwa sheria dhidi ya Sabato ya uumbaji wa Mungu, na ndipo Mungu atakapofanya 'kazi yake ya ajabu' katika dunia"
"Wakati taifa letu [Marekani] litakapozikataa kanuni za serikali yake hata kuweza kutunga sheria ya Jumapili, kwa kitendo hicho Uprotestanti utakuwa umeshikana mikono na Upapa"
Je, Upapa hatimaye utakuwa na nguvu kiasi gani hapa Marekani?
"Waprotestanti wanafungua mlango kwa Upapa kupata tena mamlaka katika Marekani ya Kiprotestanti mamlaka ambayo ulipoteza katika Ulimwengu wa zamani"
Ni nani atakayewaongoza watu watakapokuwa wameungana ili kuwapinga wafuasi wa Mungu.
"Tunapokaribia dhiki kuu ya mwisho, ni jambo la maana sana kwamba upatano na umoja viwepo miongoni mwa vyombo vya Bwana. Ulimwengu umejawa na dhoruba na vita na kutofautiana. Hata hivyo, chini ya kiongozi mmoja --- Mamlaka ya Papa -- watu wataungana kumpinga Mungu kwa njia ya mashahidi wake. Muungano huo unaimarishwa kabisa na yule mwasi mkuu"
Kusema kweli, ni nani hasa anayesimama nyuma ya Papa?
"Yuko mmoja anayesondwa kidole katika unabii kuwa ni mtu wa kuasi. Yeye ni mwakilishi wa Shetani,,.... Hapa yuko mtu aliye msaidizi mkuu wa Shetani, aliye tayari kutekeleza kazi ambayo Shetani aliianzisha kule mbinguni, kazi ya kujaribu kuirekebisha sheria ya Mungu. Na ulimwengu wa kikristo umezikubali juhudi zake kwa kumpokea mtoto huyu wa Upapa, yaani, sheria ya Jumapili"
Je, ni nini tunachopaswa kuwa tunafanya sasa, ili kuweza kukabiliana kwa ufanisi na upinzani wa jamii ya Kikristo iliyojiunga pamoja?
"Ulimwengu wote u kinyume chetu, makanisa yanayopendelewa na watu wengi yako kinyume chetu, sheria za nchi hivi karibuni zitakuwa kinyume chetu. Kama kuna wakati ambapo watu wa Mungu walipaswa kushikamana pamoja nisasa"
Imenukuliwa kitabu cha Dhiki kuu, Sura ya 2.
Mungu akubariki unaposoma na kufanya uamuzi pamoja na matayarisho ya kwenda Mbinguni, maana mwisho wa hayo ni makao ya milele.
No comments:
Post a Comment