Monday, February 24, 2014

KANISA LA MWISHO LA KRISTO

Ukweli uo huo umeelezwa wazi katika Agano Jipya pamoja nalile la Kale. 
Katika maono yake matakatifu Mtume Yohana, akiwa kisiwani Patmo, aliruhusiwa kuangalia mpaka mwisho wa karne za Kipindi cha Kikristo. Analiona Kanisa la Mwisho la Kikristo, yaani, Kanisa ambalo litamlaki Bwana atakapokuja mara ya pili.
Naye Yohana analieleza hivi kanisa hilo.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke [kanisa],
akaenda afanye vita juu ya wazao wake WALIOSALIA, WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, na KUWA NA USHUHUDA WA YESU" (Ufunuo l2:17). "JOKA" hapa anamwakilisha Shetani. "MWANAMKE" analiwakilisha Kanisa la Kristo.
"WAZAO WAKE WALIOSALIA" huhusu Kanisa mpaka mwisho kabisa wa dunia, Kanisa litakalokuwako wakati wa kuja mara ya pili kwa
Kristo.
 Hapa Kanisa linaonyeshwa kuwa lina tabia za pekee mbili: 
Kwanza, LINASHIKA AMRI ZA MUNGU; pili, LINA KARAMA YA UNABII [ROHO YA UNABII]  ambayo ndiyo USHUHUDA WA YESU
(Ufunuo 19:10).
 
Kanisa hili la mwisho litakuwa ni KANISA LINALOSHIKA SABATO, kwa maana kwa kweli isingeweza kusemwa kamwe juu ya kanisa lo lote ambalo halishiki Sabato kuwa lilizishika amri za Mungu. 
Kanisa linalozishika amri za Mungu tisa tu ni kanisa
linalovunja amri za Mungu.
Kanisa hilo la mwisho ni Kanisa lishikalo amri zote 10, ikiwemo na Sabato.
Tena Yohana, akiangalia mbele kupita karne zote, anauona ujumbe ule wa mwisho wa injili ukihubiriwa kwa '"Kila taifa na kila kabila na lugha na jamaa."
Anaueleza ujumbe huo katika sura ile ya kumi na nne ya Ufunuo. 
Ujumbe huo ni wa aina tatu, na hapo utakapotimizwa, ndipo Kristo ATAKAPOONEKANA akija na mawingu ya mbinguni kuvuna mavuno ya nchi (Ufunuo 14:14,15). 
Kwa hiyo huo lazima uwe ni ujumbe wa mwisho kutolewa kwa wanadamu.
Yohana pia anawaona watu wale watakaoutoa ujumbe huo, naye anaeleza hivi habari zao: "Hapa ndipo penye subira ya WATAKATIFU, hao WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU na
IMANI YA YESU" (Ufunuo 14:l2).
Kwa hiyo katika Agano la Kale na Jipya Mungu anaonyesha wazi kwa mwanafunzi wa Biblia ya kwamba KILA MKRISTO ANAWAJIBIKA KUSHIKA KILA SEHEMU YA SHERIA YAKE TAKATIFU.
Katika siku hizi za mwisho Sheria hii itakuwa KIPIMO CHA IMANI ya watu wa Mungu. 
Na wale ambao kwa uaminifu WATASHINDA katika jaribio [Kipimo] hilo wanapewa ahadi hii: "Heri wale wazishikao amri Zake, wawe na haki kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake" (Ufunuo 22:14, Tafsiri ya King James Version)

No comments: