Sunday, February 23, 2014

JE! MBINGUNI WANAABUDU SIKU GANI?

Tumeona kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia siku mbalimbali kwajili ya ibada Ijumaa, Jumamosi, Jumapili, Jumatano na nyingine nyingi. Lakini swali ni hili, je tutakapoenda mbinguni ni siku gani tutakayoabudu kati ya hizi? Je, Biblia inasemaje kuhusu hili? Isaya. 66:22,23 “Kama vile MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO hata SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU ASEMA BWANA.” 

Mungu anasema katika Neno lake kuwa katika mbingu ambayo ameifanya kwajili ya watakatifu wake WOTE, kwamba watakuwa WANAMWABUDU katika kila siku ya SABATO yaani siku ya Jumamosi.
Ni ukweli kuwa Mungu atakuja kuchukua watakatifu wake “hao wazishikao AMRI za Mungu na imani ya Yesu”.
Ufunuo.14:12 Kamwe hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. 

Si ndiyo? Sasa biblia inatoa maana rasmi ya neno dhambi katika 1 Yoh3:4, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwakuwa DHAMBI NI UASI.”
Hivyo dhambi ni uasi wa sheria za Mungu, yaani waasi wote wa sheria hawataingia mbinguni.
Pia amri kumi za Mungu zapaswa kushikwa kwa ukamilifu wake zote kama zinavyoelezwa katika Kutoka. 20:3-17. Na kuvunja amri moja tu, ni sawasawa umevunja amri zote kumi. Yakobo2:10,11 inasema “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
Maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue.
Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekua mvunja sheria.” 

Yaani ukishika amri za Mungu tisa tu, ukaacha kuishika sabato ya Jumamosi UMEKUA MVUNJA SHERIA.
Na kwa wale ambao wanashika sabato tu na kuvunja zingine amekuwa mvunja sheria pia bali usalama upo katika kushika amri zote za Mungu ikiwemo sabato.
Kurani nayo inasema katika suratun Nahl(16) kifungu cha 124 kuwa, “Hakika (adhabu ya kuvunja taadhima ya) Jumamosi iliwekwa juu ya wale waliohitilafiana kwa ajili ya hiyo (Jumaamosi), na kwa yakini Mola wako atahukumu baina yao siku ya kiama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana .” 

Hivyo hata kurani inatoa onyo kwa wavunja sheria ya Mungu hasa wavunja sabato ya BWANA yaani siku ya Jumamosi. 
Je wavunja sabato ya BWANA wote watapotea hata wanaovunja sabato wakati wanatenda miujiza? Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo NITAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ONDOKENI KWANGU NINYI MTENDAO MAOVU.” 
Mungu anasema kwamba kuna watu watamwendea wakimsihi waingie katika ufalme wake lakini atawakataa kwa maana hata wakati wanatenda miujiza hiyo hakuwajua maana hawakutii mapenzi ya Mungu.
Lakini tumaini lipo, Yesu alisema “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sautiyangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, nay eye pamoja name.” 


Ufunuo.3:20 Pia alisema kwakua “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na SAUTI YANGU WATAISIKIA; KISHA KUTAKUWA NA KUNDI 1 NA MCHUNGAJI MMOJA

No comments: