Tuesday, February 25, 2014

AMRI YA JUMAPILI KWA ULIMWENGU MZIMA

 Biblia inasemaje juu ya kuinuka tena ulimwenguni kote kwa uongozi ule wa Roma ya Kikatoliki kabla ya mwisho wa wakati? Ufunuo 13:3,8.
  1. Ni Taifa gani lililopata upendeleo litakaloongoza katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili?

a. "Kundi lilo hilo lilitoa madai yake ya kwamba kuenea haraka kwa ufisadi kwa sehemu kubwa kulichangiwa na kuinajisi ile wanayoiita 'Sabato ya Kikristo,' na ya kwamba kule kulazimisha utunzaji wa Jumapili kungeyaboresha sana maadili ya jamii. Madai hayo yanasisitizwa hasa katika Amerika, ambako fundisho la Sabato ya Kweli limehubiriwa karibu kwa mapana yake yote." GC 587.

b. "Mataifa ya kigeni yatafuata mfano wa Marekani. Japokuwa Taifa hili linaongoza, hata hivyo hatari iyo hiyo itawajia watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu." 6T 395.

2. Ni mataifa mangapi yatakayofuata mfano huo wa Marekani?

a. "Amerika, nchi yenye uhuru wa dini, itakapoungana na upapa katika kuzitenda jeuri dhamiri za watu na kuwalazimisha watu kuiheshimu sabato hiyo ya uongo [Jumapili], hapo ndipo watu wa kila nchi ulimwenguni watakapoongozwa kufuata mfano wake." 6T 18 (Angalia GCB 1-28- 1893).

b. " '[A]liwanywesha Mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake [mafundisho yake potofu]' Ufunuo 14:6-8. Hii inakuwaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato bandia [Jumapili]." 8T 94.
c. "Suala hili la Sabato ndilo litakuwa hoja kuu katika Pambano Kuu la mwisho ambalo kwalo ulimwengu wote utakuwa na sehemu yake ya kufanya." 6T 352.

4. Ni dini gani hasa ya ulimwengu mzima inayohusika na kulazimisha utunzaji huu wa Jumapili?

a. "Kwa vile Sabato imekuwa jambo la pekee la mabishano katika Mataifa ya jamii za Kikristo, na wenye mamlaka ya dini [ya Muungano] na serikali wameungana katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili, basi, wale walio wachache sana watakaoendelea kukataa kukubaliana na madai hayo yanayopendwa na wengi watakuwa watu wa kuchukiwa mno ulimwenguni kote." GC 615.

b. "Jamii yote ya Kikristo itagawanyika katika makundi makuu mawili, wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake." GC 450; 9T 16; 2SM 55.

5. Ni jambo gani litakalowapata Waadventista Wasabato ambao hawawezi kukubaliana na Amri hiyo ya Jumapili?

a. "Amri ile itakayoitia nguvu ibada ya siku hii [ya Jumapili] itatangazwa ulimwenguni kote.... Maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao, kwa kulitii Neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo [Jumapili]." 7BC 976.
b. "Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista Wasabato, kwa sababu hawatakubali kumsujudu papa kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, siku iliyowekwa na mamlaka hiyo ya Mpinga Kristo. Ni kusudi lake Shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili ukuu wake humu duniani usipate kupingwa." TM 37; RH 8-22-1893.

c. "Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo." GC 604.

6. Ni athari gani zitakazoletwa na uamsho huo wa bandia juu ya karibu wote wanaojiita Wakristo kwa jina tu?

"Wakatangaza ya kwamba wao walikuwa na ile kweli; ya kwamba miujiza ilitendeka kati yao; ya kwamba uwezo mkuu na ishara na maajabu yalitendeka miongoni mwao; na ya kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ile Milenia [miaka elfu moja] waliyokuwa wanaingojea kwa muda mrefu sana. Ulimwengu wote uliongolewa na kuafikiana na Amri ile ya Jumapili." Letter 6, 1884. 7.

Ni alama gani mbili zinazopingana zitapokewa na makundi hayo mawili ya watu katika ulimwengu huu hapo Jumapili itakapotiwa nguvu kwa kuitungia sheria?

a. "Wakati utunzaji wa sabato hiyo ya uongo [Jumapili] kwa kuitii amri ya serikali, kinyume na amri ile ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya Kweli, kwa kuitii Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ni ushahidi wa utii kwa Muumbaji. Wakati kundi moja, kwa uikubali alama ya utii kwa mamlaka za duniani, linapokea Alama (chapa) ya Mnyama, lile jingine, kwa kuichagua ishara ya utii kwa Mamlaka ile ya Mbinguni, litapokea Muhuri wa Mungu." GC 605.

c. "Matokeo ni ya kuogofya ambayo kwayo ulimwengu huu utakabiliwa nayo. Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo.

Kwa upande mwingine, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inayoamuru Siku ya Mapumziko iliyowekwa na Muumbaji inataka watu wote waitii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zake [kumi]. "Jambo hilo likiwa limewekwa wazi hivyo mbele yake [kila mtu], hapo ndipo ye yote atakayeikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguu yake ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea Alama ya Mnyama...." GC 604.

No comments: