Je, imani ya mizimu ilikuwa ni tatizo katika siku za Biblia?
Kutoka 22:18; Mambo ya Walawi 20:6,27; Kumbukumbu 18:9-12;
Marko 5:1-18; 9:14-29; Matendo 16:16-18.
Je, Shetani alijigeuza nyakati fulani na kuwa kitu fulani au mtu fulani anayevutia macho kuliko yeye mwenyewe?
Mwanzo 3:1-5; 1 Samweli 28:6-14.
Je, bado anao uwezo huo wa kujigeuza mwenyewe ili apate kufanana na kile kitu anachokitaka?
2 Wakorintho 11:13-15.
Ni kwa kusudi gani Shetani atafanya miujiza yake katika siku za mwisho kabisa za historia ya ulimwengu huu?
Ufunuo 16:13,14; 13: 13,14; 2 Watesalonike 2:9,10; Mathayo 24:4,24.
Je, ni wapi umizimu wa kisasa ulikoanzia?
"Naliona kwamba zile sauti za makelele ya ajabu katika mji wa New York [Hydesville, N.Y. mwaka 1848] na mahali pengine zilikuwa ni nguvu za Shetani, na kwamba mambo kama hayo yangezidi kuongezeka na kuwa ya kawaida, yakiwa yamevikwa vazi la dini ili kuwatuliza wale waliodanganyika wajisikie kuwa na usalama zaidi, na kama ikiwezekana, kuyavuta mawazo ya watu wa Mungu wapate kuyaangalia mambo hayo na kuwafanya waone mashaka juu ya mafundisho na uweza wa Roho Mtakatifu" (EW 43).
Ni kwa njia ipi umizimu sasa unabadilisha mfumo wake?
"Umizimu sasa unabadilisha mfumo wake, ukiwa umeficha baadhi ya sehemu zake muhimu zinazochukiza, sasa umejivika vazi la Kikristo. ... Wakati zamani ulimkana Kristo na Biblia, sasa unakiri kukubali vyote viwili" (GC 557,558).
Je, Shetani sasa anafanya maandalizi maalum kwa ajili ya jambo gani?
"Kwa muda mrefu Shetani amekuwa akijitayarisha kwa juhudi zake za mwisho ili kuudanganya ulimwengu. ... kidogo kidogo ametayarisha njia kwa madanganyo yake makuu kwa kusitawisha umizimu" (GC 561).
"Raho wa Mungu anaondoka hatua kwa hatua ulimwengguni. Shetani naye pia anakusanya majeshi yake ya uovu, akiwaendea 'wafalme wa dunia na wa ulimwengu wote; kuwakusanya chini ya bendera yake, ili kuwapa mafunzo kwa ajili ya 'vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi'" (7BC 983).
Ni baada ya tukio gani tunaweza kutazamia udhihirisho maalum wa utendaji wake wa ajabu?
"Kwa kupitisha amri inayolazimisha desturi ya upapa huku likivunja sheria ya Mungu, taifa letu litakuwa limejitenga kabisa lenyewe mbalia na haki. Wakati Uprotestanti utakaponyosha mkono wake ng'ambo ya shimo kubwa ili kuushikilia mkono wa mamlaka ya Rumi, wakati utakaponyosha mkono mikono juu ya shimo kubwa ili kushikana mikono na Umizimu, wakati nchi yetu, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya katiba yake kama serikali ya Kiprotestanti na ya Jamuhuri, na kuandaa njia kwa ajili ya utangazaji wa uongo na madanganyo ya upapa, hapo ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia kwa utendaji miujiza wa ajabu wa Shetani na kwamba mwisho u karibu"
Itaendelea...

"Zile sauti za makelele ya ajabu ambapo umizimu wa kisasa ulianza nako hakukuwa ni matokeo ya hila au ujanja wa kibinadamu, bali kulikuwa ni kazi ya moja kwa moja ya malaika wabaya" (GC 553).
Ni kwa njia ipi umizimu sasa unabadilisha mfumo wake?
"Umizimu sasa unabadilisha mfumo wake, ukiwa umeficha baadhi ya sehemu zake muhimu zinazochukiza, sasa umejivika vazi la Kikristo. ... Wakati zamani ulimkana Kristo na Biblia, sasa unakiri kukubali vyote viwili" (GC 557,558).
Je, Shetani sasa anafanya maandalizi maalum kwa ajili ya jambo gani?
"Kwa muda mrefu Shetani amekuwa akijitayarisha kwa juhudi zake za mwisho ili kuudanganya ulimwengu. ... kidogo kidogo ametayarisha njia kwa madanganyo yake makuu kwa kusitawisha umizimu" (GC 561).
"Raho wa Mungu anaondoka hatua kwa hatua ulimwengguni. Shetani naye pia anakusanya majeshi yake ya uovu, akiwaendea 'wafalme wa dunia na wa ulimwengu wote; kuwakusanya chini ya bendera yake, ili kuwapa mafunzo kwa ajili ya 'vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi'" (7BC 983).
Ni baada ya tukio gani tunaweza kutazamia udhihirisho maalum wa utendaji wake wa ajabu?
"Kwa kupitisha amri inayolazimisha desturi ya upapa huku likivunja sheria ya Mungu, taifa letu litakuwa limejitenga kabisa lenyewe mbalia na haki. Wakati Uprotestanti utakaponyosha mkono wake ng'ambo ya shimo kubwa ili kuushikilia mkono wa mamlaka ya Rumi, wakati utakaponyosha mkono mikono juu ya shimo kubwa ili kushikana mikono na Umizimu, wakati nchi yetu, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya katiba yake kama serikali ya Kiprotestanti na ya Jamuhuri, na kuandaa njia kwa ajili ya utangazaji wa uongo na madanganyo ya upapa, hapo ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia kwa utendaji miujiza wa ajabu wa Shetani na kwamba mwisho u karibu"
(5T 451).
Itaendelea...
No comments:
Post a Comment