Katika kitabu cha Mathayo 24:1 - 45, Wanafunzi walimwendea YESU ili wamwonyesheshe majengo ya hekalu, Akawambia hamyaoni haya yote? amini nawambieni halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
Majengo ya hekalu la Yelusalemu yalijengwa kwa ustadi wa hali ya juu na ilikua ni fahari kwa wayahudi kuliona jengo lao likiwa limenakishiwa kwa vito vya thamani. hata wanafunzi nao walilipenda. Mtazamo wa Yesu ukawa tofauti, wanafunzi walidhani huenda angewasifia, lakini ikawa tofauti, mtazamo wa Yesu ukawa tofauti yeye aliona mbele zaidi.
Hata alipokua katika Mlima mzeituni ilibidi wanafunzi wamwendee wakamwuliza mambo hayo yatakua lini?
nayo ni nini dalili ya kuja kwako? na ya mwisho wa dunia?
Yesu akajibu akawambia angalieni mtu asiwadangaye. Kwanini Yesu alianza na neno hili "mtu asiwadanganye" unajua ndugu zangu shetani hajalala Yesu alilijua hilo ndo maana alisema neno hilo. wengi tumesikia sehemu mbalimabali watu wakisema na kutabilri habari za kuja kwa Yesu wengine wakaweka na tarehe, lakini hawakua sahihi walikua waongo. ndo maana Yesu aliwatahadharisha "mtu asiwadanganye"
Pia Yesu akasema wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; na watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. angalieni msitishwe hayo hayanabudi kutukia lakini ule mwisho bado.
Kwamaana Taifa litaondoka kupigana na taifa, na Ufalme kupigana na Ufalme, kutakua na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. "Sikia" Yesu ana sema Hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
Yesu anaongezea kitu kingine, "Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtachukiwa na mataifa kwaajili ya jina langu. Wote wanao shikilia imani ya Yesu lazima wasalitiwe dunia itawachukia na watauawa. Shetani atakua na chuki na waote wanao mcha Mungu na kushika amri zake. Kumbuka hata mitume waliteseka sana na wengine waliuawa. Makristo wengi wa uongo watakuja na kudanganya wengi, hawa makristo wauongo waliotajwa hapo ni wakristo wanao taja jina la Yesu lakini wanapotoa maandiko. mfano, kitabu cha Kutoka 20:8 linasema "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase" wao wanasema shika kitakatifu siku ya Bwana Mungu wako. Yeyote anaye fundisha Biblia vibaya huyo ni mkristo wa uongo.
Ndugu yangu mpendwa utakaye soma ujumbe huu, fahamu kua tunaishi nyakati za mwisho na mbaya za kutisha. yale yote aliyo sema yesu yamesha timia. Vita, njaa, matetemeko, maradhi, n.k yamesha tokea.
Lakini habari njema itahubiriwa katika ulimwengu wote, ili kua ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapo kuja. sasa tunaona kila mahali neno la mungu likihubiriwa, ingekua heri kama tungejitoa maisha yetu kwa Mungu.
Pia fungu la 15, limetajwa chukizo la uharibifu lililo nenwa na nabii Daniel.. sikia (Chukizo la uhalibifu ni sheria ya kuabudu Jumapili kwa lazima) hilo ndilo chukizo la uhalibifu. kuifanya siku iliyowekwa na wanadamu kua badala ya siku aliyoiweka Mungu muumbaji.
Lakini Yesu anasema mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka.
Hebu kila mmoja wetu angechunguza maandiko kwaajili ya wokovu wake binafsi, Yesu alikufa kwaajili yako na yangu ili tupate uzima wa milele. Uzima hauji tuu kwa kuka tu lazima kujibidisha kumtafuta Mungu na kufanya mapenzi yake. Yeyote anayeongozwa na Mungu atakua mshindi.
Mungu akubariki.
Imeandaliwa na J .Tave
1 comment:
huo ni unabii unaotimia hivyo tujiweke tayari.
Post a Comment