Wednesday, February 29, 2012

MIUJIZA YA SHETANI

Je, imani ya mizimu ilikuwa ni tatizo katika siku za Biblia?
  Kutoka 22:18; Mambo ya Walawi 20:6,27; Kumbukumbu 18:9-12;
Marko 5:1-18; 9:14-29; Matendo 16:16-18.

Je, Shetani alijigeuza nyakati fulani na kuwa kitu fulani au mtu fulani anayevutia macho kuliko yeye mwenyewe?
  Mwanzo 3:1-5; 1 Samweli 28:6-14.

Je, bado anao uwezo huo wa kujigeuza mwenyewe ili apate kufanana na kile kitu anachokitaka?
  2 Wakorintho 11:13-15.

Ni kwa kusudi gani Shetani atafanya miujiza yake katika siku za mwisho kabisa za historia ya ulimwengu huu?
  Ufunuo 16:13,14; 13: 13,14;  2 Watesalonike 2:9,10; Mathayo 24:4,24.

Je, ni wapi umizimu wa kisasa ulikoanzia?
  "Naliona kwamba zile sauti za makelele ya ajabu katika mji wa New York [Hydesville, N.Y. mwaka 1848] na mahali pengine zilikuwa ni nguvu za Shetani, na kwamba mambo kama hayo yangezidi kuongezeka na kuwa ya kawaida, yakiwa yamevikwa vazi  la dini ili kuwatuliza wale waliodanganyika wajisikie kuwa na usalama zaidi, na kama ikiwezekana, kuyavuta mawazo ya watu wa Mungu wapate kuyaangalia mambo hayo na kuwafanya waone mashaka juu ya mafundisho na uweza wa Roho Mtakatifu" (EW 43).
  "Zile sauti za makelele ya ajabu ambapo umizimu wa kisasa ulianza nako hakukuwa ni matokeo ya hila au ujanja wa kibinadamu, bali kulikuwa ni kazi ya moja kwa moja ya malaika wabaya" (GC 553).

Ni kwa njia ipi umizimu sasa unabadilisha mfumo wake?
  "Umizimu sasa unabadilisha mfumo wake, ukiwa umeficha baadhi ya sehemu zake muhimu zinazochukiza, sasa umejivika vazi la Kikristo. ... Wakati zamani ulimkana Kristo na Biblia, sasa unakiri kukubali vyote viwili" (GC 557,558).

Je, Shetani sasa anafanya maandalizi maalum kwa ajili ya jambo gani?
  "Kwa muda mrefu Shetani amekuwa akijitayarisha kwa juhudi zake za mwisho ili kuudanganya ulimwengu. ... kidogo kidogo ametayarisha njia kwa madanganyo yake makuu kwa kusitawisha umizimu" (GC 561).
  "Raho wa Mungu anaondoka hatua kwa hatua ulimwengguni. Shetani naye pia anakusanya majeshi yake ya uovu, akiwaendea 'wafalme wa dunia na wa ulimwengu wote; kuwakusanya chini ya bendera yake, ili kuwapa mafunzo kwa ajili ya 'vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi'" (7BC 983).


Ni baada ya tukio gani tunaweza kutazamia udhihirisho maalum wa utendaji wake wa ajabu?
  "Kwa kupitisha amri inayolazimisha desturi ya upapa huku likivunja sheria ya Mungu, taifa letu litakuwa limejitenga kabisa lenyewe mbalia na haki. Wakati Uprotestanti utakaponyosha mkono wake ng'ambo ya shimo kubwa ili kuushikilia mkono wa mamlaka ya Rumi, wakati utakaponyosha mkono mikono juu ya shimo kubwa ili kushikana  mikono na Umizimu, wakati nchi yetu, chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya katiba yake kama serikali  ya Kiprotestanti na ya Jamuhuri, na kuandaa njia kwa ajili ya utangazaji wa uongo na madanganyo ya upapa, hapo ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia kwa utendaji miujiza wa ajabu wa Shetani na kwamba mwisho u karibu" 
(5T 451).

 Itaendelea...

Tuesday, February 21, 2012

MUUNGANO WA MAKANISA

Je kila dhehubu la Kiprotestanti katika nchi ya Marekani litaingia katika muungano wa makanisa unaokuja?

Wakati makanisa makuu ya Marekani, yatakapoungana  katika yale mafundisho wanayoyashikilia kwa pamoja, yataishawishi seirikali kuyatia nguvu kisheria maagizo yao na kuzitegemeza desturi zao, ndipo Marekani ya Kiprotestanti itakua imeunda sanamu ya utawala wa kidini wa Rumi, na ndipo utoaji adhabu ya kiserikali kwa wale wanaopinga utakuwa jambo lisiloepukika.

Ni katika msingi gani hatimaye makanisa ya Kiprotestanti yataweza kuungana?
  "Tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya Kiprotestanti inaangaliwa  na wengi kama ushahidi wa kukata maneno kwamba hakuna juhudi yoyote inayoweza kufanywa ili kupata umoja kwa kulazimishwa. Lakini kwa m,iaka mingi, katika makanisa yenye imani ya Kiprotestanti, pamekua na maoni yenye nguvu, yanayozidi kuongezeka ambayo yanapendelea muungano uliojengwa juu ya mafundisho wanayoyaamini kwa pamoja. Ili kupata muungano kama huo, mjadala wa mafundisho yote ambayo hawaafikiani wote kwa pamoja - haidhuru yawe ya muhimu jinsi gani kutakana na msimamo wa Biblia- ni lazima uachwe.

Ni mafundisho gani makuu mawili yenye makosa ambayo makanisa hayo yameyashika kwa pamoja?
   "Kwa njia ya makosa makuu mawili... imani kwamba roho haifi, na utakatifu wa Jumapili.... Shetani atawaleta watu chini ya madanganyo yake. Wakati lile la kwanza linaweka msingi wa imani ya umizimu, lile la pili linaleta mapatano ya kukubaliana na Rumi"

Je, Uprotestanti hatimaye utaungana na Ukatoliki?  
 "Neno la Mungu linafundisha kwamba matukio ya [kuikandamiza Sabato] yatarudiwa tena wakati Wakatoliki wa Rumi na Waprotestanti watakapoungana kwa lengo la kuitukuza Jumapili"
  "Hatuwezi kuona ni kwa jinsi gani Kanisa Katoliki la Rumi linaweza kujinasua dhidi ya shitaka la kuabudu sanamu. ... Na hiyo ndiyo dini ambayo Waprotestanti wanaanza kuiangalia kwa upendeleo mkubwa sana, na ambayo hatimaye itaungana na Uprotestanti.
   "Maadam muda wa majaribio bado ungalipo, kutakuwepo na nafasi kwa mwinjilisti wa vitabu kufanya kazi. Wakati madhehebu za dini zitakapoungana na upapa ili kuwatesa watu wa Mungu, mahali palipo na uhuru wa dini patafunguliwa kwa uinjilisti wa vitabu"

Je, kutakuwa na muungano wa mfumo au muungano katika utendaji?
  "Ulimwengu  unaojidai kuwa ni wa Kiprotestanti utaungana kwa mapatano na yule mtu wa kuasi, ndi0po kanisa na ulimwengu vitakua katika mwafaka potofu
   "Uroma katika Ulimwengu wa Zamani wa Ulaya, na Uprotestanti Ulioasi katika Ulimwengu Mpya wa Marekani, watafuata njia ileile katika katika kuwashughulikia wale wanoziheshimu amri zote za Mungu.

Je, ni Rumi itabadilika au ni Uprotestanti ndio utakaobadilika ili kufanya muunganiko tena uwezekane? 
   "Hata hivyo, muungano huo, hautafanyika kutokana na badiliko katika Ukatoliki, kwani Rumi kamwe haibadiliki. Inadai kwamba haiwezi kukosea. Ni Uprotestanti, utakaobadilika. Kukubali mawazo yaliyo huru kwa upande wake kutauleta mahali utashikana mkono na Ukatoliki. 'Biblia, ndiyo msingi wa imani yetu;ilikua ndiyo kauli ya Waprotestanti katika siku za Luther, wakati Wakatoliki  walipaza sauti zao, wakisema, Mababa, desturi, mapokeo; siku hizi Waprotestanti wengi wanaona ni vigumu kuthibitisha mafundisho yao kutoka katika Biblia, lakini hata hivyo, hawana ujasiri wa kimaadili kukubali ukweli unaohusisha msalaba; kwahiyo wanaelekea kwenye msimamo wa Ukatoliki.  Naam, Waprotestanti wa karne ya kumi na tisa wanawakaribia kwa kasi Wakatoliki katika kukosa kwao uaminifu kuhusu Maandiko"
  "Waprotestanti wa Marekani watakuwa msitari wa mbele katika kunyosha mikono yao juu ya shimo kubwa na kuushika mkono Umizimu; watanyosha mikona juu ya shimo kubwa na kushikana mikono na mamlaka ya Rumi; na chini ya uongozi wa muunganohuo wa utatu [Uprotestanti, Umizimu, na Ukatoliki], nchi hii itafuata katika nyayo za Rumi kwa kukandamiza uhuru wa dhamiri"
 "Wakati Uprotestanti utakapo nyosha mkono kuvuka shimo kubwa na kuushika mkono wa Mamlaka ya Rumi, wakati utakaponyosha mkono juu ya shimo kubwa na kushikana mikono na Umizimu, wakati chini ya uongozi wa muungano huo wa utatu, nchi yetu [Marekani] itakapokuwa imeikataa kila kanuni ya Katiba yake kama Serikali ya Kiprotestanti na ya Jamuhuri, na kuandaa njia kwaajili ya kueneza uongo na udanganyifu wa upapa, ndipo tunaweza kujua kwamba wakati umewadia wa utendaji wa miujiza wa ajabu wa Shetani na kwamba mwisho u karibu"
  "Uprotestanti utaipatia mamlaka ya Rumi mkono wa ushirika. Ndipo itapitishwa sheria dhidi ya Sabato ya uumbaji wa Mungu, na ndipo Mungu atakapofanya 'kazi yake ya ajabu' katika dunia"
  "Wakati taifa letu [Marekani] litakapozikataa kanuni za serikali yake hata kuweza kutunga sheria ya Jumapili, kwa kitendo hicho Uprotestanti utakuwa umeshikana mikono na Upapa"

Je, Upapa hatimaye utakuwa na nguvu kiasi gani hapa Marekani? 
  "Waprotestanti wanafungua mlango kwa Upapa kupata tena mamlaka katika Marekani ya Kiprotestanti mamlaka ambayo ulipoteza katika Ulimwengu wa zamani"

Ni nani atakayewaongoza watu watakapokuwa wameungana ili kuwapinga wafuasi wa Mungu.
   "Tunapokaribia dhiki kuu ya mwisho, ni jambo la maana sana kwamba upatano na umoja viwepo miongoni mwa vyombo vya Bwana. Ulimwengu umejawa na dhoruba na vita na kutofautiana. Hata hivyo, chini ya kiongozi mmoja  --- Mamlaka ya Papa -- watu wataungana kumpinga Mungu kwa njia ya mashahidi wake. Muungano huo unaimarishwa kabisa na yule mwasi mkuu"

Kusema kweli, ni nani hasa anayesimama nyuma ya Papa? 
  "Yuko mmoja anayesondwa kidole katika unabii kuwa ni mtu wa kuasi. Yeye ni mwakilishi wa Shetani,,.... Hapa yuko mtu aliye msaidizi mkuu wa Shetani, aliye tayari kutekeleza kazi ambayo Shetani aliianzisha kule mbinguni, kazi ya kujaribu kuirekebisha sheria ya Mungu. Na ulimwengu wa kikristo umezikubali juhudi zake kwa kumpokea mtoto huyu wa Upapa, yaani, sheria ya Jumapili"

   Je, ni nini tunachopaswa kuwa tunafanya sasa, ili kuweza kukabiliana kwa ufanisi na upinzani wa jamii ya Kikristo iliyojiunga pamoja?
  "Ulimwengu wote u kinyume chetu, makanisa yanayopendelewa na watu wengi yako kinyume chetu, sheria za nchi hivi karibuni zitakuwa kinyume chetu. Kama kuna wakati ambapo watu wa Mungu walipaswa kushikamana pamoja nisasa"


Imenukuliwa kitabu cha Dhiki kuu, Sura ya 2.



Mungu akubariki unaposoma na kufanya uamuzi pamoja na matayarisho ya kwenda Mbinguni, maana mwisho wa hayo ni makao ya milele.
 
 

Sunday, February 19, 2012

PAPA AAGIZA KUUNDWA SERIKALI MOJA DUNIANI.
  • Asema itaanza na UN kisha kukabidhiwa dini
  • Lengo ni kulinda mataifa masikini duniani
  • Yahofiwa kuwa mwanzo wa Mpinga kristo
Wakati dunia nzima ikikabiliwa na migogoro ya kisiasa na mitikisiko ya kiuchumi, kiongizi wa Katoloki duniani, Papa Benedict wa XVI, amesema suluhiso la hayo yote ni kuundwa upesi kwa serikali moja ya kidunia, itakayoongozwa kwa muda na Umoja wa Mataifa (UN), lakini baadaye itaachiwa huru ijiendeshe yenyewe.
  Waraka rasmi wa kanisa Katoliki, ulitolewa na mamlaka ya Vaticani (makao makuu ya kanisa hilo) hivi karibuni, umemkariri Papa   akieleza kua kwa hali iliyofikia sasa dunia inahitaji kua na mfumo mpya wa serikali moja "a supranational authority" utakaotoa mwongozo katika masuala ya uchumi na siasa.
  Ili kuharakisaha uundwaji wake serikali hiyo, ataanzishwa na kusimamiwa na umoja wa mataifa kwa muda, lakini baadaye utajitegemea na kua serikali huru, na itakua na nguvu za kuhakikisha kua mataifa yaliyo endelea hayabani mataifa yaliyo masikini kwakutumia mabavu kupita kiasi.
  Waraka wa Vatican unasema ; Katika roho moja na nia moja, tukiwa wamoja Papa Benedict wa XVI anaona kuwa nilazima sasa kuharakisha kuundwa  kwa mfumo, (serikali) moja ya kisiasa duniani kote. Hili ni suala endelevu liloshughulikia  na kutatua matatizo ya ulimwengu wote kwa pamoja.
  Fikiri, kwa  mfano; hitaji kubwa la dunia kwa sasa ni amani na usalama, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kudhibiti silaha kali, kutetea na kulinda haki za msingi za binadamu, utawala wa uchumi na uratibu wa sera, wimbi la uhamiaji na usalama wa chakula na mazingira. Mambo haya yanapaswa yasimamiwe kwa pamoja na serikali moja ya dunia. Kimsingi hatuwezi kupata suluhisho la mambo yote haya, bila dunia kua kitu kimoja, yaani kuunganisha serikali zote na dini zote kua na mamlaka moja yenye nguvu na mamlaka ya kushughulikia kikamilifu na kwa nguvu kubwa.
  Kiukweli mamlaka ya Vatican inakerwa na tabia iliyoanzishwa na serikali za mataifa ya Magharibi ya kuzuiya wahamiaji kutoka mataifa maskini (dunia ya tatu) katika kambi ya watakatifu (Jean Rapsail), tulioamua kua kinyume na Magharibi katika suala la kuwatenga wahamiaji wanaotoka katika eneo la dunia ya tatu. Tunaunga mkono uingiaji wa wahamiaji hao wanao vamia mataifa tajiri.
  Kwa baraka zote, imeidhiniswa kuwa makasisi wa kanisa katoliki waunge mkono misafara ya wahamiaji wanaoingia nchi za Magharibi kwa kuwa Papa yuko kinyume na msimamo na mataifa ya ulaya na Afrika wa kupiga marufuku wahamiaji.
   Kimsingi  mamlaka ya Vatican inapendekeza serikali hiyo moja iwe na fedha yake, itakayotumiwa na watu wote, benki kuu moja, na mamlaka kamili ya dunia ambayo itatoa ruhusa kwa wanadamu, kuingia taifa lolote atakalo kuishi.
   Tayari vikao vimekaa mjini Vatcan na kushirikisha madhehebu kadhaa, ambayo yamekubali mpango huo wa kufaa, serikali moja ya dunia itakayokua mwalubaini wa matatizo na migogoro iliyopo sasa duniani. 
   Kwa mujibu wa Papa, kuundwa kwa serikali moja ya dunia itakayokuwa na mamlaka itakua ni hatua ya kwanza ya kuufikia umoja wa kiimani, aliagiza Bwana Yesu wa kukusanya pia makanisa yote  ya kikristo na kua na umoja wa dunia kidini.
  Mpango huu wa Vatican, ulitangiliwa na ule wa kuiunganisha dunia katika Teknolojia ya juu sana ya upachikaji wa chip maalumu kwenye mkono wa kulia au paja la uso, ambazo zinaweza kutoa taarifa zote za mwanadamu na kumtambulisha anachofanya na mahali alipo.
  Tayari majaribio kadhaa yamefanyika, ikiwa ni pamoja na kutumika katika mataifa ya Austrelia ambapo mwanasheria mkuu wa serikali amepachikwa kifaa hicho, na juhudi za kuwapachika wengine ziko mbioni.
  Kwakupitia mfumo wa chip, mwanadamu mmoja anaweza kutawala dunia yote kwa urahisi kuliko mfumo mwingine wowote. Inaelezwa kuwa, mfumo huo huu ukishashika kasi utaelekeza taifa kwenye mfumo mwingine unaitwa 'cashlesss' ambapo wanadamu wataondokana na matumizi ya fedha tasilimu na badala yake watatumia kadi iliyopachikwa mwilini.
  Mchakato wa masuala hayo yote  yameibua hisia tofauti, kwa baadhi ya waumini wa Protestant kuwa huenda hii ikawa ni mwanzo wa kuingia kwa Mpinga kristo duniani.

Imenukuliwa toka Gazeti la JIBU LA MAISHA la Jumapili, Februari 12 - 18, 2012.

Majibu ya mambo hayo hapo juu kwa msaada zaidi tafuta kanisa la Wa Sabato ndilo pekee lililojaliwa kujua unabii na vipindindi vyote hadi mwisho wa dunia.
Taarifa hizi kwao ni matayarisho ya kwenda mbinguni, maana Yesu karibu kuja, sio muda mrefu tutamwona mawinguni. Wito mpokeeni Yesu awe mwkozi wa maisha yenu, shikeni amri zake zote ikiwemo na sabato, ambayo wengi wameikataa, na kwasababu hiyo hawatafikia kipeo cha kweli yote maana wameikataa tabia ya Mungu.

Mungu akubariki unapofanya uamuzi.  
 

Saturday, February 18, 2012

NI AKINA NANI PEKEE WATAKAO SIMAMA IMARA KATIKA PAMBANO KUU LA MWISHO?

"Ni wale tu walioimarisha akili zao kwa kweli za Biblia ndio watakaoweza kusimama imara katika pambano kuu la mwisho"

"Jifunze Biblia yako kwa namna ambayo hujawahi kamwe kujifunza siku za nyuma. Isipokua unainuka na kufikia kiwango cha juu cha utakatifu katika maisha yako ya dini, utakua tayari kwaajiri ya kufunuliwa kwa Bwana wetu"

 "Ni wale tu ambao wamekua wanafunzi wenye bidii wa Maandiko, na ambao wameipenda hiyo kweli, watakaolindwa dhidi ya madanganyo yenye nguvu yatakayouteka ulimwengu wote"

 "Tunazikaribia nyakati za dhoruba ... Kila msimamo wa imani yetu utachunguzwa; na ikiwa sisi si wanafunzi kamili wa Biblia, tuliothibitika, tulioimarishwa, na kutulia katika ukweli, basi, hekima ya watu mashuhuri wa ulimwengu huu itatufanya tupotee"         Dhiki kuu inakuja lakini kunatumaini, uk 15



Friday, February 17, 2012

DUNIA HII IMEFIKIA UKINGONI HEBU KILA MTU ANGESOMA MAANDIKO

Katika kitabu cha Mathayo 24:1 - 45, Wanafunzi walimwendea YESU ili wamwonyesheshe majengo ya hekalu, Akawambia hamyaoni haya yote? amini  nawambieni halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
 Majengo ya hekalu la Yelusalemu yalijengwa kwa ustadi wa hali ya juu na ilikua ni fahari kwa wayahudi kuliona jengo lao likiwa limenakishiwa kwa vito vya thamani. hata wanafunzi nao walilipenda. Mtazamo wa Yesu ukawa tofauti, wanafunzi walidhani huenda angewasifia, lakini ikawa tofauti, mtazamo wa Yesu ukawa tofauti yeye aliona mbele zaidi.
 Hata alipokua katika Mlima mzeituni ilibidi wanafunzi wamwendee  wakamwuliza mambo hayo yatakua lini?
nayo ni nini dalili ya kuja kwako? na ya mwisho wa dunia?
 Yesu akajibu akawambia angalieni mtu asiwadangaye.  Kwanini Yesu alianza na neno hili "mtu asiwadanganye" unajua ndugu zangu shetani hajalala Yesu alilijua hilo ndo maana alisema neno hilo. wengi tumesikia sehemu mbalimabali watu wakisema na kutabilri habari za kuja kwa Yesu wengine wakaweka na tarehe, lakini hawakua sahihi walikua waongo. ndo maana Yesu aliwatahadharisha "mtu asiwadanganye"
 Pia Yesu akasema wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; na watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. angalieni msitishwe hayo hayanabudi kutukia lakini ule mwisho bado.
 Kwamaana Taifa litaondoka kupigana na taifa, na Ufalme kupigana na Ufalme, kutakua na njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. "Sikia" Yesu ana sema  Hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
 Yesu anaongezea kitu kingine, "Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtachukiwa na mataifa kwaajili ya jina langu. Wote wanao shikilia imani ya Yesu lazima wasalitiwe dunia itawachukia na watauawa. Shetani atakua na chuki na waote wanao mcha Mungu na kushika amri zake. Kumbuka hata mitume waliteseka sana na wengine waliuawa. Makristo wengi wa uongo watakuja na kudanganya wengi, hawa makristo wauongo waliotajwa hapo ni wakristo wanao taja jina la Yesu lakini wanapotoa maandiko. mfano, kitabu cha Kutoka 20:8 linasema "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase"  wao wanasema shika kitakatifu siku ya Bwana Mungu wako. Yeyote anaye fundisha Biblia vibaya huyo ni mkristo wa uongo.
 Ndugu yangu mpendwa utakaye soma ujumbe huu, fahamu kua tunaishi nyakati za mwisho na mbaya za kutisha. yale yote aliyo sema yesu yamesha timia. Vita, njaa, matetemeko, maradhi, n.k yamesha tokea.
 Lakini habari njema itahubiriwa katika ulimwengu wote, ili kua ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapo kuja. sasa tunaona kila mahali neno la mungu likihubiriwa, ingekua heri kama tungejitoa maisha yetu kwa Mungu.
 Pia fungu la 15, limetajwa chukizo la uharibifu lililo nenwa na nabii Daniel.. sikia (Chukizo la uhalibifu ni sheria ya kuabudu Jumapili kwa lazima) hilo ndilo chukizo la uhalibifu. kuifanya siku iliyowekwa na wanadamu kua badala ya siku aliyoiweka Mungu muumbaji.
 Lakini Yesu anasema mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka.
Hebu kila mmoja wetu angechunguza maandiko kwaajili ya wokovu wake binafsi, Yesu alikufa kwaajili yako na yangu ili tupate uzima wa milele. Uzima hauji tuu kwa kuka tu lazima kujibidisha kumtafuta Mungu na kufanya mapenzi yake. Yeyote anayeongozwa na Mungu atakua mshindi.

 Mungu akubariki.

Imeandaliwa na J .Tave