Wednesday, March 7, 2012

MPINGA KRISTO

Biblia haijakaa kimya juu ya watu waliokinyume chake japo wengi wamevaa vazi la Ukristo, lakini kiulweli ndani ni Mbwa mwitu, tena wabaya.

Kitabu cha 2Watesalonike 2:1-4. (1) Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
(2) kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
 (3) Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
 (4) yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu


Biblia inasema siku ya Bwana haiji usipokuja kwanza ule ukengeufu akafunuliwa yule mtu wa kuasi mwana wa uharibifu; ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.


Wapendwa Yesu hawezi kuja hadi mpinga Kristo amekuwa dhahiri, na watu wameamua kwa mioyo yao nani watamwabudu, je, ni Mungu Muumbaji ama watamwabudu mwanadamu. Hapo ndipo watajulikana wakristo wa kweli na wauongo.


Sasa mpinga Kristo ni nani? kiukweli mamlaka inayojulikana kwamjibu wa unabii ni mamlaka ya Rumi. inamaana gani, mamlaka hii wakokinyume na Yesu, pia wamechukua nafasi ya Yesu kwakudai wao wanaouwezo wa kusamehe dhambi, nakwamba Papa ni mwakilishi wa Mungu duniani.


Angalia picha hapo chini, ikimwonyesha Papa akitoa ishara za Freemasons.

Huyu ndiye mtu wa kuasi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa

No comments: