Kwa kipindi cha miaka 2500 ya kwanza ya historia ya
mwanadamu,hapakuwepo ufunuo ulioandikwa. watu waliokuwa wamefundishwa na
Mungu walipitisha elimu yao kwa wengine, na ilirithishwa kwa mwana na
baba kutoka kizazi hadi kizazi.
Maandalizi ya neno liloandikwa
yalianza wakati wa Musa. Kisha mafunuo yenye uvuvio yaliunganishwa
kwenye kitabu kilichovuviwa. Kazi hii iliendelea kwa muda miaka 1600 Kuanzia kwa Musa mwana historia ya uumbaji na sheria hadi mpaka Yohana
mwandishi wa kweli kuu za injili.
Biblia inamtaja kuwa Mungu ndiye
mwandishi wake lakini iliandikwa kwa mkono wa wanadamu na katika
mitindo tofauti ya uandishi wa vitabu vyake mbalimbali. Aliwapa ndoto,
njozi, vielelezo na mifano na wale walionyeshwa ukweli huo,
waliyaunganisha mawazo yenyewe katika lugha za kibinadamu.
Amri kumi zilinenwa na Mungu mwenyewe, ziliandikwa na Mungu mwenyewe yeye ndiye mmiliki na hazikutungwa na mwanadamu.
Kanisa la Mungu linaanzia Edeni na kumalizikia Edeni. Neno Kanisa limetokana na neno Ekklesia’ ikimanisha walioitwa.
Kanisa katika Bustani Edeni (Mwanzo 1-2)
• Baada ya Uumbaji liikuwa na waumini wawili Adamu na Hawa
• Mchungaji wa kanisa hili alikuwa Mungu
• Lilikuwa na maagizo ya kufanya na kufuata
• Katika bustani hii Bwana aliweka miti ya kila aina kwa ajili ya
matumizi na uzuri, kulikuwa na miti iliyosheheni matunda tele yaliyojaa
harufu nzuri na yenye ladha ya kupendeza ambayo Mungu alipanga yawe
chakula kwa ajili yawana ndoa hawa watakatifu Adamu na Hawa Katika Edeni.
Wanandoa hawa watakatifu walikuwa na furaha sana wakiwa katika Edeni.
Mungu aliwapa utawala usio na mpaka katika kila kitu chenye uhai. Simba
na Mwana kondoo walicheza pamoja kando yao kwa amani na bila kudhuriana
au walilala miguuni pao. Ndege wa kila rangi na kila aina walirukaruka
miongoni mwa miti na maua na kuwazunguka Adamu na Hawa.
Siku ya kwanza, Iwe nuru, ikawa nuru, Mchana na Usiku – mstri 2-3
Siku ya pili Anga likatengwa na maji, mbingu ikapewa jina – Mstr 6-7
Siku ya tatu, Nchi kavu, bahari, matunda na mimea Mstr 10-12
Siku ya nne, Jua na mwezi viwe dalili ya majira, iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka (14-15)
Siku ya tano Viumbe wa baharini/majini na ndege wa angani
Siku ya sita- Wanyama na Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu
Siku ya Saba, Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe.
Ibada katika kanisa hili.
Ibada ilikuwepo na siku ya ibada ilikuwa ni siku ya SABA YA JUMA.
Wakati huu hata majina ya siku yalikuwa hayajakuwepo. Siku ya saba
ilikuwa ni siku maalumu ambayo Mungu mwenyewe aliitenga. Lakini pia
Mungu aliendelea kutoa mahubiri ndani ya kanisa hili. Mungu aliwakusanya
malaika ili wapate kuchukua hatua ya kuzuia uovu uliokuwa uantishia
kutokea. Iliamuliwa katika baraza la mbinguni kuwa malaika watembelee
Edeni na kumwonya Adamu kuwa alikabiliwa na hatari kutoka kwa adui yule
Malaika waliwapa Adamu na Hawa kisa cha kuhuzunisha cha uasi na anguko
la Shetani.
Sheria pia zilikuwepo ndani ya kanisa hili.
Katikati ya bustani karibu na mti wa uzima ulisimama mti wa ujuzi wa
mema na mabaya Mungu aliuumba mti huu mahususi kwa ajili yao ili kutoa
ushahidi wa utii, imani na upendo wao kwake. Bwana aliwaamuru wazazi
wetu wa kwanza kutokula matunda ya mti huu wasije wakafa. Aliwaambia
kuwa waweza kula matunda ya miti yote ya bustani isipokuwa mmoja tu na
ikiwa watakula matuda ya mti huu watakufa
Vitu vitakatifu katika kanisa hilli
Vitu vitakatifu katika kanisa hili vilikuwa ni Siku ya Saba ya juma
(Siku ya Ibada) na ndoa. Hivi ni vitakatifu kwa sababu mwanzilishi ni
Mungu Mwenye na vilitengwa kwa ajili ya mambo matakatifu.
Dhambi
kipindi hiki ilikuwa haijaingia na walikuwa hawana mavazi yoyote kuuvika
mwili kwani walifunikwa na utukufu wa Mungu. Nyumba yo ilikuwa Bustani
ya edeni.
Katika kanisa hili kazi ilikuwa ni Baraka walifanya kazi siku
sita, kazi ya kutunza bustani na kulima. Walipewa jukumu la kutawala
kila kitu Mungu alichokiumba.
Watu wa kanisa hili waliendelea kwa
kipindi kirefu bila dhambi na waliendelea kuwa wawili kabla ya dhambi
na walikuwa hawajapata watoto. Sheria ya mungu ilitunzwa. Ibada
ilikuwani yashukrani.
Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuupanua ufalme
wake na kuifanya dunia kuwa koloni la mbingu. Hii ilimanisha kuwa
adamu na hawa walipaswa kuakisi tabia za mbinguni, utamaduni wa mbinguni
na lugha ya mbinguni. Hata mfumo wa maisha ulikuwa wa kimbingu. Uwezo
wa akili ulikuwa mkubwa sna maana aliweza kuita majina kila kiumba
ambacho bwana aliipitisha kwake.
Maisha yalikuwa mema na matakatifu yenye furaha kubwa , na walikuwa wakihudumiwa na Mungu mwenyewe pamoja na malaika.
By Yusuph Bigurube.