Tuesday, February 25, 2014

AMRI YA JUMAPILI KWA ULIMWENGU MZIMA

 Biblia inasemaje juu ya kuinuka tena ulimwenguni kote kwa uongozi ule wa Roma ya Kikatoliki kabla ya mwisho wa wakati? Ufunuo 13:3,8.
  1. Ni Taifa gani lililopata upendeleo litakaloongoza katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili?

a. "Kundi lilo hilo lilitoa madai yake ya kwamba kuenea haraka kwa ufisadi kwa sehemu kubwa kulichangiwa na kuinajisi ile wanayoiita 'Sabato ya Kikristo,' na ya kwamba kule kulazimisha utunzaji wa Jumapili kungeyaboresha sana maadili ya jamii. Madai hayo yanasisitizwa hasa katika Amerika, ambako fundisho la Sabato ya Kweli limehubiriwa karibu kwa mapana yake yote." GC 587.

b. "Mataifa ya kigeni yatafuata mfano wa Marekani. Japokuwa Taifa hili linaongoza, hata hivyo hatari iyo hiyo itawajia watu wetu katika sehemu zote za ulimwengu." 6T 395.

2. Ni mataifa mangapi yatakayofuata mfano huo wa Marekani?

a. "Amerika, nchi yenye uhuru wa dini, itakapoungana na upapa katika kuzitenda jeuri dhamiri za watu na kuwalazimisha watu kuiheshimu sabato hiyo ya uongo [Jumapili], hapo ndipo watu wa kila nchi ulimwenguni watakapoongozwa kufuata mfano wake." 6T 18 (Angalia GCB 1-28- 1893).

b. " '[A]liwanywesha Mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake [mafundisho yake potofu]' Ufunuo 14:6-8. Hii inakuwaje? Kwa kuwalazimisha watu kuikubali sabato bandia [Jumapili]." 8T 94.
c. "Suala hili la Sabato ndilo litakuwa hoja kuu katika Pambano Kuu la mwisho ambalo kwalo ulimwengu wote utakuwa na sehemu yake ya kufanya." 6T 352.

4. Ni dini gani hasa ya ulimwengu mzima inayohusika na kulazimisha utunzaji huu wa Jumapili?

a. "Kwa vile Sabato imekuwa jambo la pekee la mabishano katika Mataifa ya jamii za Kikristo, na wenye mamlaka ya dini [ya Muungano] na serikali wameungana katika kulazimisha utunzaji wa Jumapili, basi, wale walio wachache sana watakaoendelea kukataa kukubaliana na madai hayo yanayopendwa na wengi watakuwa watu wa kuchukiwa mno ulimwenguni kote." GC 615.

b. "Jamii yote ya Kikristo itagawanyika katika makundi makuu mawili, wale wanaozishika amri [kumi] za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa yake." GC 450; 9T 16; 2SM 55.

5. Ni jambo gani litakalowapata Waadventista Wasabato ambao hawawezi kukubaliana na Amri hiyo ya Jumapili?

a. "Amri ile itakayoitia nguvu ibada ya siku hii [ya Jumapili] itatangazwa ulimwenguni kote.... Maonjo na mateso yatawajia wale wote ambao, kwa kulitii Neno la Mungu, watakataa kuisujudu sabato hiyo ya uongo [Jumapili]." 7BC 976.
b. "Ulimwengu wote utachochewa kuwa na uadui dhidi ya Waadventista Wasabato, kwa sababu hawatakubali kumsujudu papa kwa njia ya kuiheshimu Jumapili, siku iliyowekwa na mamlaka hiyo ya Mpinga Kristo. Ni kusudi lake Shetani kusababisha wafutiliwe mbali duniani, ili ukuu wake humu duniani usipate kupingwa." TM 37; RH 8-22-1893.

c. "Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo." GC 604.

6. Ni athari gani zitakazoletwa na uamsho huo wa bandia juu ya karibu wote wanaojiita Wakristo kwa jina tu?

"Wakatangaza ya kwamba wao walikuwa na ile kweli; ya kwamba miujiza ilitendeka kati yao; ya kwamba uwezo mkuu na ishara na maajabu yalitendeka miongoni mwao; na ya kwamba hiyo ilikuwa ndiyo ile Milenia [miaka elfu moja] waliyokuwa wanaingojea kwa muda mrefu sana. Ulimwengu wote uliongolewa na kuafikiana na Amri ile ya Jumapili." Letter 6, 1884. 7.

Ni alama gani mbili zinazopingana zitapokewa na makundi hayo mawili ya watu katika ulimwengu huu hapo Jumapili itakapotiwa nguvu kwa kuitungia sheria?

a. "Wakati utunzaji wa sabato hiyo ya uongo [Jumapili] kwa kuitii amri ya serikali, kinyume na amri ile ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu, utunzaji wa Sabato ya Kweli, kwa kuitii Sheria ya Mungu [Amri Kumi], ni ushahidi wa utii kwa Muumbaji. Wakati kundi moja, kwa uikubali alama ya utii kwa mamlaka za duniani, linapokea Alama (chapa) ya Mnyama, lile jingine, kwa kuichagua ishara ya utii kwa Mamlaka ile ya Mbinguni, litapokea Muhuri wa Mungu." GC 605.

c. "Matokeo ni ya kuogofya ambayo kwayo ulimwengu huu utakabiliwa nayo. Mamlaka za ulimwengu huu, zikiwa zimeungana pamoja kuzipiga vita Amri [Kumi] za Mungu, zitatangaza amri kwamba 'wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,' (Ufunuo 13:16), watafuata kwa lazima desturi za kanisa kwa kuitunza sabato hiyo ya uongo [Jumapili]. Wale wote watakaokataa kutii watakabiliwa na adhabu kutokana na sheria za serikali zao, na hatimaye itatangazwa kwamba wanastahili kifo.

Kwa upande mwingine, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] inayoamuru Siku ya Mapumziko iliyowekwa na Muumbaji inataka watu wote waitii na kutishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zake [kumi]. "Jambo hilo likiwa limewekwa wazi hivyo mbele yake [kila mtu], hapo ndipo ye yote atakayeikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguu yake ili kuitii amri ile iliyotungwa na binadamu atapokea Alama ya Mnyama...." GC 604.
http://api.ning.com/files/RuWbev-xAt8JOWYH*2QzHqULqrczY2cTkdyS0lJKMUhqFz9Rg-cE2jJFBpnzpe*o6DssmOLFnoQgOcJGwwDFZncTvV721K8a/Supermarket2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQzRe_8yyusGYhl4BbiDAvXDY03cKFoX0RhNoj8OTYXE03ri0ELrai_zW-ZoC6V9RYBRqprQqDkuTQ7nuYvl2Lvk6jO_a5NvpZ8bsjVXm4bXvbIkSKoVlxiSahbk-OKJHPw1j27_PJE8Y/s1600/otmmktcra.jpg

WATU WANNE WAPO KATIKA HALI MBAYA NA WENGINE 7 WAMEJERUHIWA BAADA YA LORI SCANIA KUGONGANA USO KWA USO NA BASI DOGO LA ABIRIA


Picha juu ni baadhi ya abiria wakiwa kwenye hali  baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga jana

WATU wanne wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga.

Kwa mujibu wa shuhuda ya ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota, ameiambia blogu hii usiku huu kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki isiyotumia akili ya lori hilo . Majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda mfupi baadaye walianza kukimbizwa kuleta dare s salaam kw amatibabu zaidi.

Abiria wawili waloikuwa mbele  ya daladala walikatika miguu.

Majeruhi wengine walioweza kuzungumza ni: Mustafa mfungapoa wa mkuranga Abdul Ally wa mwandege Ramadhani rajab Theofrida Mwinuka (alikuwa mbele amevunjika miguu)Jamal  mbaraka (aliyekwanguka ngozi ya kichwa) Abraham Mohamed

Swalehe salum

KITUNGUU SWAHUMU KINGA YA KUDUMU YA MARADHI

http://api.ning.com/files/DQZ40zyDI503SCBB5Kds6P0bF98gDD0SAqjStbxo8M1xcM6cbTGJ1fow-E2nKzgU6e30R91hE1HyF2RaX6ZN4jStXu5FQPZ7/jinsiulivyo.jpg
 Tafiti nyingi zimeshafanyika duniani kuhusu faida za kitunguu swaumu ambazo zimethibitisha kuwa mtu akitafuna na kumeza hata punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku asubuhi, basi mtu huyo atakuwa amejitengenezea kinga ya mwili ya kudumu itakayomlinda na maradhi mbalimbali, yakiwemo maradhi sugu yaliyoshindikana hospitalini.   
 Kitunguu swaumu kimegundulika kuwa rafiki wa damu mwilini, kwani kinapoliwa, huenda moja kwa moja kutoa sumu zote kwenye damu na kuipa damu vitamin na huongeza uwezo wa damu kusafiri vyema katika mishipa hivyo kumfanya mtu ajisikie mwenye afya njema kila siku.
Aidha, kitunguu swaumu kimegundulika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa ya moyo kwa kupenya katika mishipa ya damu na kuvunja-vunja Cholestrerol zote ili kupisha njia ya damu iwe safi na wazi kutokana na ‘antibiotic’ iitwayo ‘Allicin’ iliyomo kwa wingi katika chakula hiki.
China na India zinaaminika kuwa ni nchi ambazo wakazi wake ni watumiaji wakubwa wa kitunguu swaumu katika milo yao ya kila siku. Tabia hii imewasaidia sana kujikinga na maradhi mengi yanayoweza kuzuilika. Bila shaka hata Watanzania tukiamua kutumia kwa wingi kitunguu hiki katika milo yetu ya kila siku, tutajikinga na maradhi mengi na hata  uwezo wa kufikiri (Extra clear thinking capacity) utaongezeka, kwani kitunguu huongeza akili pia.
Ili nawe kujiepusha na maradhi na pengine kuyatibu yale ambayo umeshayapata kwa kutumia njia asilia, tafadhali anza sasa utaratibu wa kutafuna na kumeza angalau punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku asubuhi kabla ya kula chochote, fanya kuwa utaratibu wako wa kila siku. Ili kuondoa harufu mdomoni, tafuna kwanza kisha kapige mswaki na kuendelea na mlo wako wa kawaida.
Kuna jambo ambalo linaweza kuwakatisha tamaa ya kupona baadhi ya watu watakaotumia kitunguu swaumu kama dawa. Tafiti zimeonyesha kuwa upo uwezekano wa baadhi ya vitunguu swaumu kutokuwa na virutubisho vinavyotakiwa. Hii inatokea, na inahusisha sana aina ya udongo uliyopo mahali kilipooteshwa kitunguu hicho na kwa akili ya kawaida, utakubali kuwa kile kilichoota kwenye udongo wa mfinyanzi hakitakuwa na ladha sawa ya kile kilichoota kwenye mchanga.
Kwa kutambua hilo, watafiti waliamua kutengeneza vidonge vya vitunguu swaumu ambavyo tayari vimepitishwa katika maabara kuhakiki ubora kabla ya kusindikwa na kutengezwa vidonge vyenye uhakika wa tiba. Vidonge hivyo vipo madukani na ukivihitaji utapewa maelekezo ya kuvipata kwa kuwasiliana na mwandishi wa makala haya.
                   Global Publishers

Monday, February 24, 2014

KANISA LA MWISHO LA KRISTO

Ukweli uo huo umeelezwa wazi katika Agano Jipya pamoja nalile la Kale. 
Katika maono yake matakatifu Mtume Yohana, akiwa kisiwani Patmo, aliruhusiwa kuangalia mpaka mwisho wa karne za Kipindi cha Kikristo. Analiona Kanisa la Mwisho la Kikristo, yaani, Kanisa ambalo litamlaki Bwana atakapokuja mara ya pili.
Naye Yohana analieleza hivi kanisa hilo.
"Joka akamkasirikia yule mwanamke [kanisa],
akaenda afanye vita juu ya wazao wake WALIOSALIA, WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, na KUWA NA USHUHUDA WA YESU" (Ufunuo l2:17). "JOKA" hapa anamwakilisha Shetani. "MWANAMKE" analiwakilisha Kanisa la Kristo.
"WAZAO WAKE WALIOSALIA" huhusu Kanisa mpaka mwisho kabisa wa dunia, Kanisa litakalokuwako wakati wa kuja mara ya pili kwa
Kristo.
 Hapa Kanisa linaonyeshwa kuwa lina tabia za pekee mbili: 
Kwanza, LINASHIKA AMRI ZA MUNGU; pili, LINA KARAMA YA UNABII [ROHO YA UNABII]  ambayo ndiyo USHUHUDA WA YESU
(Ufunuo 19:10).
 
Kanisa hili la mwisho litakuwa ni KANISA LINALOSHIKA SABATO, kwa maana kwa kweli isingeweza kusemwa kamwe juu ya kanisa lo lote ambalo halishiki Sabato kuwa lilizishika amri za Mungu. 
Kanisa linalozishika amri za Mungu tisa tu ni kanisa
linalovunja amri za Mungu.
Kanisa hilo la mwisho ni Kanisa lishikalo amri zote 10, ikiwemo na Sabato.
Tena Yohana, akiangalia mbele kupita karne zote, anauona ujumbe ule wa mwisho wa injili ukihubiriwa kwa '"Kila taifa na kila kabila na lugha na jamaa."
Anaueleza ujumbe huo katika sura ile ya kumi na nne ya Ufunuo. 
Ujumbe huo ni wa aina tatu, na hapo utakapotimizwa, ndipo Kristo ATAKAPOONEKANA akija na mawingu ya mbinguni kuvuna mavuno ya nchi (Ufunuo 14:14,15). 
Kwa hiyo huo lazima uwe ni ujumbe wa mwisho kutolewa kwa wanadamu.
Yohana pia anawaona watu wale watakaoutoa ujumbe huo, naye anaeleza hivi habari zao: "Hapa ndipo penye subira ya WATAKATIFU, hao WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU na
IMANI YA YESU" (Ufunuo 14:l2).
Kwa hiyo katika Agano la Kale na Jipya Mungu anaonyesha wazi kwa mwanafunzi wa Biblia ya kwamba KILA MKRISTO ANAWAJIBIKA KUSHIKA KILA SEHEMU YA SHERIA YAKE TAKATIFU.
Katika siku hizi za mwisho Sheria hii itakuwa KIPIMO CHA IMANI ya watu wa Mungu. 
Na wale ambao kwa uaminifu WATASHINDA katika jaribio [Kipimo] hilo wanapewa ahadi hii: "Heri wale wazishikao amri Zake, wawe na haki kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake" (Ufunuo 22:14, Tafsiri ya King James Version)

Sunday, February 23, 2014

JE! MBINGUNI WANAABUDU SIKU GANI?

Tumeona kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia siku mbalimbali kwajili ya ibada Ijumaa, Jumamosi, Jumapili, Jumatano na nyingine nyingi. Lakini swali ni hili, je tutakapoenda mbinguni ni siku gani tutakayoabudu kati ya hizi? Je, Biblia inasemaje kuhusu hili? Isaya. 66:22,23 “Kama vile MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO hata SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU ASEMA BWANA.” 

Mungu anasema katika Neno lake kuwa katika mbingu ambayo ameifanya kwajili ya watakatifu wake WOTE, kwamba watakuwa WANAMWABUDU katika kila siku ya SABATO yaani siku ya Jumamosi.
Ni ukweli kuwa Mungu atakuja kuchukua watakatifu wake “hao wazishikao AMRI za Mungu na imani ya Yesu”.
Ufunuo.14:12 Kamwe hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. 

Si ndiyo? Sasa biblia inatoa maana rasmi ya neno dhambi katika 1 Yoh3:4, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwakuwa DHAMBI NI UASI.”
Hivyo dhambi ni uasi wa sheria za Mungu, yaani waasi wote wa sheria hawataingia mbinguni.
Pia amri kumi za Mungu zapaswa kushikwa kwa ukamilifu wake zote kama zinavyoelezwa katika Kutoka. 20:3-17. Na kuvunja amri moja tu, ni sawasawa umevunja amri zote kumi. Yakobo2:10,11 inasema “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
Maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue.
Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekua mvunja sheria.” 

Yaani ukishika amri za Mungu tisa tu, ukaacha kuishika sabato ya Jumamosi UMEKUA MVUNJA SHERIA.
Na kwa wale ambao wanashika sabato tu na kuvunja zingine amekuwa mvunja sheria pia bali usalama upo katika kushika amri zote za Mungu ikiwemo sabato.
Kurani nayo inasema katika suratun Nahl(16) kifungu cha 124 kuwa, “Hakika (adhabu ya kuvunja taadhima ya) Jumamosi iliwekwa juu ya wale waliohitilafiana kwa ajili ya hiyo (Jumaamosi), na kwa yakini Mola wako atahukumu baina yao siku ya kiama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana .” 

Hivyo hata kurani inatoa onyo kwa wavunja sheria ya Mungu hasa wavunja sabato ya BWANA yaani siku ya Jumamosi. 
Je wavunja sabato ya BWANA wote watapotea hata wanaovunja sabato wakati wanatenda miujiza? Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo NITAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ONDOKENI KWANGU NINYI MTENDAO MAOVU.” 
Mungu anasema kwamba kuna watu watamwendea wakimsihi waingie katika ufalme wake lakini atawakataa kwa maana hata wakati wanatenda miujiza hiyo hakuwajua maana hawakutii mapenzi ya Mungu.
Lakini tumaini lipo, Yesu alisema “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sautiyangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, nay eye pamoja name.” 


Ufunuo.3:20 Pia alisema kwakua “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na SAUTI YANGU WATAISIKIA; KISHA KUTAKUWA NA KUNDI 1 NA MCHUNGAJI MMOJA

CHAKULA NA ATHARI ZAKE KWA BINADAMU

JE! CHAKULA KINAWEZA KUATHIRI AKILI YAKO?
(SOMA DANIELI 1 YOTE)
 
Amini usiamini, chakula kinaweza kuathiri akili yako, na afya yako ya kimwili na
kiroho. Chakula cha daraja la kwanza ambacho Mungu alimpa mwanadamu kilikuwa cha
nafaka, kokwa na matunda (Mwanzo 1:29). Dhambi ilipoingia ilileta laana sio tu kwa
viumbe vyote bali hata kwa ardhi. Kwa hiyo Mungu akamwongezea mwanadamu mboga
za majani katika lishe yake ya awali (Mwanzo 3:18). Gharika ilikaa juu ya nchi kwa miezi
mitano au siku 150 na kuharibu mimea yote (Mwanzo 7:24). Kwa hiyo Mungu
akamwongezea mwanadamu katika lishe yake "nyama" kutoka kwa wanyama safi tu
(Mwa. 8:3,4 imebainishwa na Law. 11:1-47; Kum. 14:1-21). Injini ya petroli hutumia
petroli tu; injili ya dizeli ni dizeli tu. Ukitaka gari lako life weka dizeli katika injini ya
petroli au petroli katika injini ya dizeli. Mtengenezaji ndiye anayejua gari lake litatumia
mafuta gani, sio mtumiaji. Vile vile, Mungu anajua chakula kinachofaa kwa mwili wa
mwanadamu, sio mwanadamu kujichagulia cho chote kuwa chakula. Wabishi wataharibu
injini za magari yao (miili yao).
Mungu aliumba wanyama safi na wanyama najisi juma lile la kwanza la uumbaji.
Kifo cha Yesu msalabani hakikuwa kwa kusudi la kuwabadilisha wanyama najisi kuwa
wanyama safi, bali wanadamu wenye dhambi kuwa watakatifu. Wale wanaotaka kuwa
watakatifu watajiepusha kula nyama inayotokana na wanyama najisi; lakini wale wasiotaka
utakatifu wataswaga kila kitu (Law. 11:41,43,46,47; Kum. 14:1-4). Mungu hamlazimishi
mtu, kama vile mtengenezaji wa injini ya gari asivyomlazimisha mtu kutumia mafuta
aliyopendekeza. Lakini matokeo mwilini ni ya hakika.
Kisa cha Petro katika Matendo 10:9-16 kimetafsiriwa chini yake katika fungu la 25
hadi 29. Hayo yalikuwa ni maono tu, si kitu halisi; hata hivyo Petro alikataa katakata
kuchinja na kula wanyama najisi ingawa ni Mungu mwenyewe aliyemwamuru kufanya
hivyo mara tatu. Mungu hana kigeugeu; alisema wanyama najisi wasiliwe, basi, hawawezi
kuliwa milele (Mal. 3:6; Zab. 89:34). Watu wanamsingizia bure Petro wanapochinja
wanyama najisi na kula; yeye alikataa katakata. Lakini kuna adhabu kali sana kwa wale
wanaoendelea kula nguruwe, panya, na machukizo yote ya Mataifa (wapagani). Soma
Isaya 65:2-6; 66:15-17).
Pombe haikuwa sehemu ya kinywaji ambacho Mungu alimpa mwanadamu; maji
safi na salama ndicho kinywaji bora kuliko vyote kwa mwanadamu (Mithali 20:1; 23:29-
35). Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Kor. 6:9,10; Gal. 5:21). Kuna wengi
wanaosema, "Mimi nakunywa sana, lakini silewi." Tatizo la pombe sio kulewa tu, bali ni
zile athari zinazotokana na kunywa pombe ambayo ina sumu mbaya ya alkoholi. Sumu
hiyo huathiri vibaya moyo, mishipa ya fahamu, nyama za mwili na kadhalika. Mungu
atamharibu mtu ye yote anayeuharibu mwili wake kwa makusudi kwa njia yo yote ile -----
pombe, tumbako, madawa ya kulevya, na kadhalika (1 Kor. 3:16,17). Pia kuna vinywaji
vinavyopendwa na watu wengi aina ya 'Cola', Kahawa, na Majani ya Chai ambavyo
huidhuru mishipa ya fahamu, ubongo na mwili. Viepukwe.
Asomaye Na Afahamu - 4
Hebu sasa na tuwaangalie wale vijana wanne wa Kiebrania, mateka kutoka
Yerusalemu, wakiwa katika jiji lile la Babeli mwaka ule wa 606 au 605 K.K. Walikuwa na
umri kati ya miaka 18 na 20. Kutokana na hekima yao walichaguliwa kujiunga na vijana
wengine wa Babeli katika Chuo cha Kishenzi [Kipagani] cha Babeli kwa mafunzo ya miaka
mitatu. Wakapewa majina ya miungu ya Babeli ----- Danieli akaitwa Belteshaza, Hanania
akaitwa Shadraka, Mishaeli akaitwa Meshaki, na Azaria akaitwa Abednego (Dan. 1:6,7).
Mfalme akaamuru wale chakula cha mfalme ili wanenepe na kuwa na akili nyingi. Kusudi
lake lilikuwa zuri sana. Lakini, je! chakula kile cha mfalme ambacho kilikuwa na nyama
najisi, kilikolezwa kwa viungo vingi vinavyodhuru mwili, na huenda kilikuwa na vileo
kingeweza kuleta afya bora na akili safi? (Dan. 1:1-5). Vijana hao wanne wa Kiebrania
walikuwa wamelelewa katika mazingira tofauti. Walifuata kanuni za afya na chakula
ambacho Mungu aliwapa wanadamu kula. Walijiepusha na nyama ya aina yo yote ile
pamoja na divai (maji matamu ya zabibu) kwa vile wao walikuwa wanadhiri wa Bwana
(Hesabu 6:1-5). Kwa hiyo agizo hilo la mfalme kwao likawa mtihani mgumu sana.
"Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme,
wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa
asijitie unajisi" (Dan. 1:8). Ni ujasiri ulioje! Ombi lake halikuwa rahisi kukubaliwa na
msimamizi yule kwa vile angekatwa kichwa kama wangeonekana wamekondeana (Dan.
1:10). Basi Danieli akamwambia, "Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku
kumi; na watupe mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tule, na maji
tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula
chakula cha mfalme..." (Dan. 1:13). Akawakubalia ombi hilo. Je! mambo yalikuwaje
kiafya baada ya siku zile kumi tu? "Nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi [wanawake
wanaohangaika na vipodozi vinavyodhuru afya wangezingatia hilo], na miili yao ilikuwa
imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule
msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula [cha mfalme], na ile divai waliyopewa
wanywe, akawapa mtama [nafaka, kokwa, mboga za majani, matunda] tu" (Dan. 1:15,16).
Chakula cha matajiri au wafalme tunachokitamani sana hakileti afya mwilini.
Chakula rahisi cha mimea na maji safi na salama ni lishe bora. Kwa akili safi na mwili
wenye afya, ulionenepa kiafya sio kwa ugonjwa, tumia vyakula vya mimea na maji safi na
salama, na kufuata Kanuni zile 8 za Afya. Wana sayansi wamegundua kuwa wale
wanaokula vyakula vya mimea bila nyama wanaishi maisha marefu sana kuliko wanaokula
nyama. Danieli naye aliishi zaidi ya miaka 80 kufikia kipindi cha utawala wa Koreshi (Dan.
1:21; 10:1). Hebu tuwafuatilie vijana wale wanne mwisho wa mafunzo yao ya miaka
mitatu. Mfalme Nebukadreza aliwaonaje?
"Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana
waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria... Na katika kila jambo la
hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa wanafaa mara kumi zaidi
ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake" (Dan.1:19,20).
Kwa nini tuhangaike sana na suala la afya ya mwili wetu, je! maisha ya kiroho si
bora zaidi? "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako
[kimwili], kama vile roho yako ifanikiwavyo" (3 Yohana 2). Wahenga walisema, "Akili
timamu katika mwili wenye afya." Ni shauri la kuzingatiwa sana. Kanuni ya Biblia ni hii:
"Basi, mlapo, mnywapo, au mtendapo neno lo lote fanyeni yote kwa utukufu wa
Mungu" (1 Kor. 10:31). Tunawajibika kuitunza miili yetu katika hali ya afya nzuri kadiri
iwezekanavyo (l Kor. 6:19,20; 1 Pet. 1:18,19; Rum.12:1,2). Suala la afya linahusu
wokovu wetu. Mungu anaweza kututumia kama Danieli (Dan. 1:17).