Saturday, September 22, 2018

USIMCHOKOZE MTOTO WAKO

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Wakolosai 3:21.

Changamoto nyingi za watoto zinatokana na wazazi/walezi wengi kuwachokoza watoto wao. Mtoto anahitaji malezi mema, huduma zote za msingi kama mavazi, chakula, malazi bora n.k. Mtoto anatakiwa kufundishwa maisha na kuishi vizuri na watu wengine.

Makosa yanayofanywa na wazazi na walezi wengi, kumtukana mtoto pindi akikosea..hii inatafsiliwa ni sawa na kuchokoza mtoto. Mtoto anapaswa kuonywa na kukemewa pindi akikosea na siyo kutukanwa.

Unavyomwambia mtoto wako mbwa wewe, kichwa chako kinafanana na ng'ombe, muone kwanza unatembea kama gari bovu, bongo lala, mlafi wewe n.k. Hayo ni maneno ya laana yanayotamkwa na wazazi wengi..unaweza kujiuliza ikiwa mtoto ni mbwa maanayake mzazi ndiye mbwa mkubwa, kitendo cha kumfananisha mtoto wako na vitu visivyo na uhai na kumfananisha na wanyama na vinyago, ni kumchokoza mtoto na kuharibu tabia yake, ni kupandikiza tabia mbaya kwa mtoto wako.

Wazazi na walezi wengine wameshindwa kuwalea na kuwalinda watoto wao, wengine wanawafanyia watoto vitendo vya ukatili, vitendo viovu na adhabu zisizo za kibinadamu. Mtoto wako akikata tamaa ni hatari sana.

Tabia mbaya huaribu ubongo wa mtoto, wazazi/walezi msiwalawiti, kubaka, kuwaonyesha picha chafu watoto wenu. Mtoto anapaswa kulindwa, kupendwa na kuthaminiwa.

Msaidie mtoto wako muelekeze njia bora ya kufanya kazi, kuwa mwalimu mzuri nyumbani. Mfundishe mtoto wako kufanya usafi wa mazingira, kusafisha nyumba, mavazi yake na usafi wa mwili wake. Mfanye mtoto wako kama rafiki yako wa karibu.

Yale unayomtendea mtoto wako ndo huwa tabia yake ukubwani.

Mungu akubariki unapotafakari somo hili.

Usimchokoze mtoto wako..!!

TAVE'S BLOG

KANISA LA KWANZA

Kwa kipindi cha miaka 2500 ya kwanza ya historia ya mwanadamu,hapakuwepo ufunuo ulioandikwa. watu waliokuwa wamefundishwa na Mungu walipitisha elimu yao kwa wengine, na ilirithishwa kwa mwana na baba kutoka kizazi hadi kizazi. 

Maandalizi ya neno liloandikwa yalianza wakati wa Musa. Kisha mafunuo yenye uvuvio yaliunganishwa kwenye kitabu kilichovuviwa. Kazi hii iliendelea kwa muda miaka 1600 Kuanzia kwa Musa mwana historia ya uumbaji na sheria hadi mpaka Yohana mwandishi wa kweli kuu za injili.

Biblia inamtaja kuwa Mungu ndiye mwandishi wake lakini iliandikwa kwa mkono wa wanadamu na katika mitindo tofauti ya uandishi wa vitabu vyake mbalimbali. Aliwapa ndoto, njozi, vielelezo na mifano na wale walionyeshwa ukweli huo, waliyaunganisha mawazo yenyewe katika lugha za kibinadamu.

Amri kumi zilinenwa na Mungu mwenyewe, ziliandikwa na Mungu mwenyewe yeye ndiye mmiliki na hazikutungwa na mwanadamu.
Kanisa la Mungu linaanzia Edeni na kumalizikia Edeni. Neno Kanisa limetokana na neno Ekklesia’ ikimanisha walioitwa.

Kanisa katika Bustani Edeni (Mwanzo 1-2)
• Baada ya Uumbaji liikuwa na waumini wawili Adamu na Hawa
• Mchungaji wa kanisa hili alikuwa Mungu
• Lilikuwa na maagizo ya kufanya na kufuata
• Katika bustani hii Bwana aliweka miti ya kila aina kwa ajili ya matumizi na uzuri, kulikuwa na miti iliyosheheni matunda tele yaliyojaa harufu nzuri na yenye ladha ya kupendeza ambayo Mungu alipanga yawe chakula kwa ajili yawana ndoa hawa watakatifu Adamu na Hawa Katika Edeni.
Wanandoa hawa watakatifu walikuwa na furaha sana wakiwa katika Edeni. Mungu aliwapa utawala usio na mpaka katika kila kitu chenye uhai. Simba na Mwana kondoo walicheza pamoja kando yao kwa amani na bila kudhuriana au walilala miguuni pao. Ndege wa kila rangi na kila aina walirukaruka miongoni mwa miti na maua na kuwazunguka Adamu na Hawa.
Siku ya kwanza, Iwe nuru, ikawa nuru, Mchana na Usiku – mstri 2-3
Siku ya pili Anga likatengwa na maji, mbingu ikapewa jina – Mstr 6-7
Siku ya tatu, Nchi kavu, bahari, matunda na mimea Mstr 10-12
Siku ya nne, Jua na mwezi viwe dalili ya majira, iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka (14-15)
Siku ya tano Viumbe wa baharini/majini na ndege wa angani
Siku ya sita- Wanyama na Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu
Siku ya Saba, Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe.

Ibada katika kanisa hili.
Ibada ilikuwepo na siku ya ibada ilikuwa ni siku ya SABA YA JUMA. Wakati huu hata majina ya siku yalikuwa hayajakuwepo. Siku ya saba ilikuwa ni siku maalumu ambayo Mungu mwenyewe aliitenga. Lakini pia Mungu aliendelea kutoa mahubiri ndani ya kanisa hili. Mungu aliwakusanya malaika ili wapate kuchukua hatua ya kuzuia uovu uliokuwa uantishia kutokea. Iliamuliwa katika baraza la mbinguni kuwa malaika watembelee Edeni na kumwonya Adamu kuwa alikabiliwa na hatari kutoka kwa adui yule Malaika waliwapa Adamu na Hawa kisa cha kuhuzunisha cha uasi na anguko la Shetani.
Sheria pia zilikuwepo ndani ya kanisa hili.
Katikati ya bustani karibu na mti wa uzima ulisimama mti wa ujuzi wa mema na mabaya Mungu aliuumba mti huu mahususi kwa ajili yao ili kutoa ushahidi wa utii, imani na upendo wao kwake. Bwana aliwaamuru wazazi wetu wa kwanza kutokula matunda ya mti huu wasije wakafa. Aliwaambia kuwa waweza kula matunda ya miti yote ya bustani isipokuwa mmoja tu na ikiwa watakula matuda ya mti huu watakufa
Vitu vitakatifu katika kanisa hilli
Vitu vitakatifu katika kanisa hili vilikuwa ni Siku ya Saba ya juma (Siku ya Ibada) na ndoa. Hivi ni vitakatifu kwa sababu mwanzilishi ni Mungu Mwenye na vilitengwa kwa ajili ya mambo matakatifu.

Dhambi kipindi hiki ilikuwa haijaingia na walikuwa hawana mavazi yoyote kuuvika mwili kwani walifunikwa na utukufu wa Mungu. Nyumba yo ilikuwa Bustani ya edeni. 
Katika kanisa hili kazi ilikuwa ni Baraka walifanya kazi siku sita, kazi ya kutunza bustani na kulima. Walipewa jukumu la kutawala kila kitu Mungu alichokiumba.

Watu wa kanisa hili waliendelea kwa kipindi kirefu bila dhambi na waliendelea kuwa wawili kabla ya dhambi na walikuwa hawajapata watoto. Sheria ya mungu ilitunzwa. Ibada ilikuwani yashukrani.
Mpango wa Mungu ulikuwa ni kuupanua ufalme wake na kuifanya dunia kuwa koloni la mbingu. Hii ilimanisha kuwa adamu na hawa walipaswa kuakisi tabia za mbinguni, utamaduni wa mbinguni na lugha ya mbinguni. Hata mfumo wa maisha ulikuwa wa kimbingu. Uwezo wa akili ulikuwa mkubwa sna maana aliweza kuita majina kila kiumba ambacho bwana aliipitisha kwake.
Maisha yalikuwa mema na matakatifu yenye furaha kubwa , na walikuwa wakihudumiwa na Mungu mwenyewe pamoja na malaika.

By Yusuph Bigurube.
 
BIBLIA BARUA YA MUNGU KWETU

Mungu amejifunua kwetu kwa njia nyingi, mojawapo ni njia kupitia uumbaji au njia ya asili. Tunapoona kila kitu katika dunia hii ni kazi yake. Maana hata sisi tu kazi yake, sio tu kazi yake bali pia tumeumbwa kwa mfano wa sura yake na hata vitu vingine alisema na vikafanyika, mwanadamu akaumbwa kwa Mungu kuushika udongo na kuufinyanga na kutuwekea pumzi ya uhai iliyotoka kwake.

Sehemu ya pili Mungu amejifunua kupitia neno lake yaani Biblia.

Biblia nini? kwa nini tuiamini Biblia? hivi kweli ni sauti ya Mungu, hivi kuna mambo ambayo hatupaswi kuyatii? hivi tunaweza kuyatii yote? Kati ya Neno la Mungu na kile viongozi wangu wanachoniambia nitii kipi? Dini yangu na biblia kipi kiko juu?
Biblia inaonyesha nia ya Mungu, inafunua hali ya binadamu jinsi ilivyo, njia ya wokovu, kuangamia kwa mwenye dhambi na furaha ya waaminio. kanuni zake ni takatifu, amri zake haziepukiki, historia zilizomo ni za kweli, na uamuzi wake kamwe haubadilshwi.

Uisome ili kuwa na hekima, uisome ili usalimike na tenda isemavyo ili uwe mtakatifu.
Biblia ni ramani na mkongojo wa msafiri, ni fira ya nahodha, upanga wa askari na mkataba wa mkristo. Mbingu inafunguliwa na inabainisha milango ya jehahanamu waziwazi.
Kristo ndio kiini kikuu cha biblia. ndiye daraja la kutuunganisha na baraka za Mungu.

Biblia inapaswa ijae akilini, iutawale moyo na iongoze miguu.Uisome mara kwa mara tena kwa maombi. Ni mgodi wenye utajiri bustani iliyojaa utukufu wa Mungu. Mungu amejifunua kupitia hapa ili kila mmoja aweze kumfahamu Mungu. Itawatia hatiani wale wote wanaodharau na kutoyatii maandiko matakatifu.
2Tmetheo 3: 15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki

Tunapaswa kutii kila neno lililopo ndani yake na wala sio tu baadhi ya sehemu fulani fulani kama ambavyo wengi tunafanya. 

Mfalme Daudi naye anasema yakuwa katika zaburi 119:115 neno lako ni taa ya miguu yangu na Mwanga wa njia zangu... yatupasa kuwa kuwa ndio iwe kiongozi wetu kila wakati.
2Petro 1:19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Mungu aliamua kuwasiliana na wanadamu kwa kutumia akili za mwanadamu, kalamu ya mwandamu na lugha ya mwanadamu lakini hapa Petro anasema waliongozwa na Roho mtakatifu kuweza kuuandika ujumbe huu. Ujumbe wa biblia haukuletwa na mwanadamu bali ni Mungu kupitia mwanadamu. Lakini pia haupaswi kutafsiria ujumbe huu kama sisi tupendavyo na wengi wetu tumefanya hivi na hivyo wengi wamepotoshwa. Lazima tuombe kabla ya kusoma ili tuweze kupewa tafsiri sahihi kama Mungu alivyokusudia.
Bwana akubari tunapooanza katika mfuulizo wa masomo ya Biblia. 

Endelea kutembelea blog hii tujifunze pamoja juu ya biblia.

By Yusuph Bigurube

KESHO NI FUMBO

Kwakuwa lipo tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa); Mhubiri 9:4 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Mhubiri 3:19 
 
MUHIMU: Kuishi sawa sawa na neno la Mungu..maana uhai wa kila kiumbe upo mikononi mwake. 
 
ZINGATIA: Mwanadamu anakufa sawa sawa na mnyama ila liko tumaini kwa mwadamu ikiwa tu atayatoa maisha yake kwa Yesu.. Huyu Yesu ndo mwenye uwezo wa kukufanya uishi tena baada ya kifo inamaana yeye ni ufufuo na uzima. KUMBUKA: Mwanadamu anamzidi mnyama kwa kuwa amenunuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo.. Mchague Yesu sasa na umfanye kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. 
 
HAKIKA: UTAISHI TENA.
 
Kwakuwa lipo tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa); Mhubiri 9:4 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Mhubiri 3:19 MUHIMU: Kuishi sawa sawa na neno la Mungu..maana uhai wa kila kiumbe upo mikononi mwake. ZINGATIA: Mwanadamu anakufa sawa sawa na mnyama ila liko tumaini kwa mwadamu ikiwa tu atayatoa maisha yake kwa Yesu.. Huyu Yesu ndo mwenye uwezo wa kukufanya uishi tena baada ya kifo inamaana yeye ni ufufuo na uzima. KUMBUKA: Mwanadamu anamzidi mnyama kwa kuwa amenunuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo.. Mchague Yesu sasa na umfanye kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. HAKIKA: UTAISHI TENA.

Make Google view image button visible again: https://goo.gl/DYGbub

Sunday, September 16, 2018

MOYO WA SHUKURANI

Kunakisa katika biblia, huwa nashangaa sana..bwana Yesu katika pita pita yake alikutana na watu 10 wenye ukoma wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! ...akawambia enendeni mkajionyeshe kwa makuhani. Wakiwa njiani ndipo muujiza wa uponyaji ulitimia. Viungo vyao vikarejea sawasawa. 
Luka 17:12-19 
 
Sitaki nielezee saana mtu mwenye ukoma yukoje..nataka tujifunze thamani ya kushukuru. Watu 10 waliponywa ukoma lakini ni mmoja pekee ndiye alikumbuka kurudi kushukuru..! Kitu ambacho kilimshangaza sana Yesu, (..hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi?) Unaweza kudhani pengine wamesahau maumivu na athali za ugonjwa wa ukoma. 
 
Wapendwa, naomba tujifunze kitu kutoka kwa yule mmoja (msamalia) aliyekumbuka kurudi kushukuru. Kushukuru ni kutambua thamani ya fadhira ulizotendewa..kushukuru ni kumpa moyo yule aliyekusaidia, kushukuru ni kuonyesha utu. Kushukuru ni kutambua msaada uliofanyiwa. 
 
Kumbuka kuwashukuru waliokusaidia ulipoumwa, ulipotingwa na jambo fulani. Kumbuka kuwashukuru waliokulipia ada yako ya masomo hadi ukamaliza masomo yako. 
 
 Kunawatu wamekuwezesha kwenye biashara yako hadi ikasitawi, acha dharau, usiwasahau ukadhani ni kwa juhudi zako, kumbuka kuwashukuru waliokusapoti hadi biashara yako ikasitawi. Hata kwenye familia hatulingani, yupo aliyebeba familia, anajitoa kwa hali na mali..mtieni moyo na kumshukuru. 
 
 Ipo nguvu kwenye kushukuru, tujifunze kushukuru kwa kila jambo.