Hakuna familia isiyo na mapungufu, Hatuna wazazi wasio na mapungufu,
sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu,
kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu.
Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.
Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.
Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu.
Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa
ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo,
kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe
hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.
Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo
endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia
mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia
inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali
pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu.
Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu, huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.
No comments:
Post a Comment