Saturday, November 22, 2014

JE AMRI KUMI ZIMEANZIA MLIMA SINAI AU KABLA YA SINAI?

Kuna kuchanganyikiwa kukubwa kuhusu Amri hizo Kumi hivi leo
katika mazingira ya kidini. Wengine bila kufikiri hata kidogo
wanasema kuwa Amri Kumi zilianza na Musa na kukoma Yesu
alipokufa [pale msalabani].
Sheria ya Mungu, ambayo watu wote
huiita Amri Kumi, kimsingi ni ya milele kama Mungu mwenyewe
alivyo. Umilele wake unashuhudiwa na Maandiko hayo
yaliyovuviwa. Amri Kumi KATIKA MFUMO WAKE WA ANDIKO juu ya mawe
huanzia Sinai. Lakini Amri zile [Kumi] zilikuwako muda mrefu
sana kabla ya Mlima Sinai, kama vile Kristo alivyokuwako kabla
ya kuja kama mwanadamu hapa duniani.

Kuthibitisha neno hilo
----- yaani, kujua kama Amri Kumi zilikuwako kabla tu ya
kutokea tukio lile lililouzunguka Mlima Sinai ----- unapaswa
kujiuliza tu swali hili:

"Je! dhambi [uvunjaji wa Amri Kumi]
ilikuwako kabla ya wakati ule?"

Na wewe, bila shaka, utapaswa
tu kuuliza swali hilo ili kupata jibu lako hili

. "Dhambi
[uvunjaji wa Amri Kumi] haihesabiwi isipokuwapo Sheria [Amri
Kumi]." Warumi 5:13. "Maana pasipokuwapo Sheria [Amri Kumi],
hapana kosa [dhambi]." Warumi 4:15. "Kwa kuwa singalijua
kutamani, kama torati [Amri Kumi] isingalisema, Usitamani
[Kutoka 20:17]." Warumi 7:7.

Je, hivi Adamu alitenda dhambi [alivunja Amri Kumi - Yak.
2:10-12]?

Biblia inasema hivi:
"Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja
dhambi [uvunjaji wa Amri Kumi] iliingia ulimwenguni, na kwa
dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa
sababu wote wamefanya dhambi [wamevunja Amri Kumi]." Warumi
5:12.Fungu hili linazungumza juu ya Adamu.

Je, Kaini alitenda
dhambi [alivunja Amri Kumi]? Soma Mwanzo 4:7.

"Kama ukitenda
vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko [uvunjaji
wa Amri Kumi upo], inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,
walakini yapasa uishinde."

Kwa nini Mungu aliuangamiza
ulimwengu wote wa kizazi kile kabla ya Gharika? Kwa sababu ya
dhambi [uvunjaji wa Amri Kumi - Mwa. 6:1-8]. Kwa ukware wao
[uasherati wao mkubwa], na ukatili wao wa kinyama, daima
walikuwa wameivunja Sheria yake [Amri Kumi].

BIBLIA HUTOA MAANA YA NENO DHAMBI
"Dhambi ni
uvunjaji wa Sheria [Amri Kumi]." 1 Yohana 3:4, AJKK. Mahali
pale ilipo dhambi, Sheria ya Mungu [Amri Kumi] ipo.

IBRAHIMU alizijua SHERIA, AMRI NA MAAGIZO YA MUNGU[Mwanzo 26;5] miaka mingi kabla ya kizazi cha israeli.
wanawaisraeli WALIZIJUA AMRI KUMI, SHERIA ZA MUNGU NA AMRI YA SABATO kabla hawajafika mlima sinai walipopewa MBAO MBILI ZA AMRI KUMI[kutoka 16;28-32]

No comments: