Ujumbe wa malaika wa pili ni huu: “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule
ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya
uasherati wake” (Ufunuo 14:8). Babeli lilikuwa ni taifa katika Agano la
Kale ambalo liliishambulia Israeli, yaani, watu wa Mungu, na kuwachukua
mateka. Babeli lilikuwa ni taifa lililojaribu kuifutilia mbali ibada
ya Mungu wa kweli wa mbinguni na mahali pake kuweka miungu ya kipagani.
Na hivyo Babeli ikawa ishara iliyowakilisha majeshi
yote yatakayowapinga watu wa Mungu katika siku za mwisho. Kwa hiyo
malaika huyu wa pili anasema kwamba Babeli umeanguka kwa sababu
umeyafanya mataifa yote ya dunia kunywa mvinyo ya uasherati wake, yaani,
hiyo ni njia ya kusema kwamba majeshi yanayopigana na Mungu katika siku
hizi za mwisho yatajaribu kumlazimisha kila mmoja kutoa utii wake kwa
majeshi hayo kuliko kwa Mungu. Imewakilishwa kama “uasherati,” au
uzinzi. Kutokumtii Mungu kunaonyeshwa katika Biblia kama uzinzi wa
kiroho, jambo hili lote linatufikisha kwenye hoja ya utii.
No comments:
Post a Comment